Bibi Titi Mohammed: Historia, harakati na wasifu wake

Sheikh Mohamed Said tupe kidogo juu ya Kambona na Bibi Titi ukaribu wao ulikuweje
Kiatu...
Katika TANU kulikuwa na wasemaji kwa maana ya wahutubuaji wakubwa
wawili nao walikuwa ni Nyerere na Bi. Titi Mohamed.

Hawa wawili ndiyo walikuwa vinara wa harakati.

Kambona alikuja baadae katika TANU na yeye alikuwa na uwezo mkubwa
pia lakini hakumzidi Bi. Titi katika kukibeba chama.

Kwa kipindi kile cha kudai uhuru Bi. Titi alikuwa juu zaidi aking'ara zaidi ya
Kambona.

Kambona
alikuja kuwa juu baada ya uhuru kwani haukupita muda Bi. Titi
na Nyerere wakakuruzana mwaka wa 1963 Nyerere alipoonysha dalili za
kutaka kuifungia East African Muslim Welfare Society (EAMWS).
 
Lizabon sijui kama anamfahamu huyu bibi titi RIP bibi titi sisi tuliokupe miaka hiyo tunajua mchango wake
 
Asante je ni hisia au ilikuwa kweli Bibi Titi aliungana na wale wana mapinduzi maana kama ilifikia hatua ya kuchukua Mali zake alipokuwa kizuizini je ni kitu gani kilikuwa nyuma ya pazia
 
Asante je ni hisia au ilikuwa kweli Bibi Titi aliungana na wale wana mapinduzi maana kama ilifikia hatua ya kuchukua Mali zake alipokuwa kizuizini je ni kitu gani kilikuwa nyuma ya pazia
Kiatu...
Mimi Bi. Titi alipata kuniambia kuwa hakuhusika na ile mipango aliyotuhumiwa.

Akanambia pia aligombana na Nyerere mwaka wa 1963 ndani ya Halmashauri
Kuu ya TANU kwa sababu ya EAMWS pale Nyerere alipotaka ndani ya TANU NEC
aungwe mkono kuivunja jumuia hiyo,

Katika watu waliompinga alikuwa Bi. Titi na ilifikia kutoleana maneno makali.

Bi.Titi alikuja akaeleza ugomvi huu katika mahojiano aliyofanya na gazeti la Rai
la 29 Desemba 1994.

Baada ya ugomvi ule Nyerere akamchukia Bi. Titi na akaanza kupanga njama
za kumuangamiza yeye na Tewa kwa kuwa wote wawili walikuwa viongozi wa
EAMWS.

Ilipofika uchaguzi wa 1965 ndipo Bi. Titi na Tewa wote wakabwagwa katika
majimbo yao kwa njama.

Hata hivyo haya mimi nilikuwa tayari nilishaelezwa zamani na Mzee Tewa na
Mzee Bilal Waikela.
 
Asante kwa ufafanuzi mkuu
 
Sina la kusema zaidi ya kukupongeza Mzee wangu, Muhammad ibnu Saidi.
ALLAH akulipe zaidi na akujaalie afya njema, akuondolee kila aina ya fitna juu ya hili la kuileta Historia ya ukweli iliyofichwa kwa makusudi.
AMIN
 
Namfahamu Bibi Titi kama mmoja wa wanaharakati waliosimama kidete kupigania uhuru wa nchi hii. Alikuwa mwanamama shupavu ambaye ametajwa mara kadhaa katika historia ya kupigania uhuru wa Taifa hili. Ni bahati mbaya kwamba wanaharakati kama hawa huwa hawapewi umuhimu mkubwa katika nchi yetu. Hata wakati anaumwa serikali ilishindwa kumpeleka nje ya nchi akajikuta anafia ktk hospitali ya Hindu Mandal. Umuhimu wa mwanamama huyu unapuuzwa sana na wanasiasa kama vile wanavyopuuza umuhimu wa hayati Abdu Jumbe ambaye naye alifia nyumbani kwake kigamboni baada ya serikali ya CCM kugoma kumpeleka akatibiwe nje ya nchi. Inauma sana.
 
Hivi huyu Mama ni (alikuwa) Bi (kama haja (ku) olewa) au Bibi (ame/li olewa)?
 
Mkuu bibi Titi,alifia hospitalin Johannesburgh Africa kusini
 
Kama sitakosea niliwahi simuliwa na mzee wangu kuwa bibi huyo aliwekwa kizuizini ktk kijiji cha gumbiro barazani songea vijijini karibu na madaba akiwa kama bibi maendeleo.watu wa gumbiro ya zamani wanamfahamu sana bibi huyo
Alikuwa mpananaji huyuuu
 
Kumbe haya mambo ya kususiana yalianza zamani? Ukipingana na mawazo ya wakubwa hata kwa mema ni janga!
 
Mbona kuna baadhi ya thread zina maandishi madogo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…