Bible Mysteries: Q source iko wapi

Mathayo 2:1 inaonyesha Yesu alizaliwa kipindi cha Herode (4 BC) ila Luka 2:2-3 inaonyesha Yesu alizaliwa kipindi cha Governor Quirinius (6 AD). Ila kungetumika source moja tu mfano hyo Q source ingesaidia kuondoa discrepancy zote zilizopo na kuweka msimamo mmoja wa Injili.

Hii paragraph imebishangaza,

BC - Before Christ, kabla Yesu kuzaliwa
AD - Anno Domino, baada ya Yesu kuzaliwa

Mleta mada tujadili kwanza uhalali wa hii paragraph kabla ya kujadili mashaka uliyonayo kuhusu biblia

NB: zingatia kuweka ushahidi ama marejeo ya kwenye kitabu husika pia
 
Ahaaaa, mbona unanifanya nicheke?

Tafiti zimefanyika na mpaka sasa hakuna exact date inayojulikana lini Jesus Christ alizaliwa.

Ndio maana mpaka sasa jibu sahihi ni yapata miaka 2000+ iliyopita.

Ila assumptions ni 4 BC mpaka 6 AD. Hapa ndipo kuna simulizi za Herod na Austus Ceasar.

Kuna mpya toka kwa Zitto Snr?
 
Watafasiri hawajakosea. Fuatilia utapata ukweli.
 
Mkuu dating ya Yesu kuzaliwa imewekewa point say Miaka 2021 iliyopita.

Sasa kukatokea nadharia mbili kwamba ule mwaka unaodaiwa Yesu alizaliwa according to Luka ni wakati wa Sensa ya Quirinius ambayo ilitokea miaka 6 zaidi ya ule mwaka unaodaiwa alizaliwa ko ndio maana inakuwa 6 AD

Same applies tu 4 BC kwamba mwaka uliokua proposed na Dionysis unapunguzwa kwa miaka 4 ili uendane na wakati ambapo Herode alikua bado yupo hai kma mathayo inavyosema.

Hope imeeleweka

NB: Kwenye radiometric dating huwa wanasema +/- n Years.
 
Mkuu hapa mjadala sio Yesu alizaliwa mwaka gani issue ni kwanini Biblia inakinzana kipindi alichozaliwa Yesu

Je ni wakati wa sensa au wakati wa uhai wa Herode?

Embu jibu hili mjadala ufungwe
 
Mkuu hapa mjadala sio Yesu alizaliwa mwaka gani issue ni kwanini Biblia inakinzana kipindi alichozaliwa Yesu

Je ni wakati wa sensa au wakati wa uhai wa Herode?

Embu jibu hili mjadala ufungwe
Mkuu kuna mahala bible imetamka lini Yesu alizaliwa?
 
Swali langu linalenga hizo annotations ambazo ni BC na AD, ikiwa zinarejea kabla au baada ya yesu kuzaliwa, ni kwa vipi tena biblia iseme yesu alizaliwa mwaka fulani kabya ya yesu kuzaliwa, ama yesu alizaliwa miaka flani baada ya yesu kuzaliwa?

Sijui umenielewa bro?
 
Nimefuatilia nimegundua proposed era za Yesu kuzaliwa zinakinzana na ndio maana nimeleta mada je ipi ni sahihi? Mathew au Luka? Mind you kuna contradiction zingine hatujaanza zi debunk!!
Hakuna mahala zinakinzana. Bali mnachanganya mambo. Hakuna exact date lini Yesu alizaliwa. Assumptions ni kati ya 4 BC na 6 AD.
 
Biblia haijawahi tamka AD ama BC ila hiyo ni kalenda ya Papa Gregory ndio ambayo inadai leo ni mwaka 2021 toka Yesu azaliwe!!

Sasa ukipiga hesabu za nadharia ya Mathayo/ Luka/Flavius Josephus utagundua kwamba kuna contention kuwa ni miaka 4 nyuma ama miaka 6 zaidi ya tarehe iliyokua proposed hapo awali na kina Dionysis.
 
Nimefuatilia nimegundua proposed era za Yesu kuzaliwa zinakinzana na ndio maana nimeleta mada je ipi ni sahihi? Mathew au Luka? Mind you kuna contradiction zingine hatujaanza zi debunk!!
Hakuna mahala zinakinzana. Bali mnachanganya mambo. Hakuna exact date lini Yesu alizaliwa. Assumptions ni kati ya 4 BC na 6 AD.
Yes ndio kipindi cha Herode au Quirinius?
Mbona unazidi kuchanganya mambo?
 
Hakuna mahala zinakinzana. Bali mnachanganya mambo. Hakuna exact date lini Yesu alizaliwa. Assumptions ni kati ya 4 BC na 6 AD.

Mbona unazidi kuchanganya mambo?
Luka anasema enzi za Sensa yaani 6 AD
Mathayo anasema enzi za Herode yaani 4 BC

Embu jikite hapo kwanini wanakinzana?
 
Ni vizuri kila kitu kikaonekana kama kilivyo. Ni nani huyo atakuwa na mamlaka ya kutengeneza standard moja. Kwenye dini kuna level mbili ule ufahamu wa kawaida ambao unajenga imani na utafiki wa kisomi ambao ni kazi ya wanazuoni. Kwa mfano; ili mtu aokolewe anahitaji kujiridhisha kwamba ni kweli Yesu alizaliwa, na kwamba ni kweli alitenda miujiza, na kwamba aliteswa, alikufa na kufufuka sawasawa na maandiko (unabii wa agano la kale). La mwisho lenye uzito mkubwa kuliko yote ni je kweli Yesu yu hai leo na anaweza kufanya yote ambayo injili (habari njema) inasema atamfanyia muumini? Kwa muumini wa kawaida anahitaji majibu ya maswali hayo iwe ni ndio.
Mungu amekusudia kuwaokoa wanadamu kwa kutii kuletwako na imani na si utafiti. Kwa hiyo utafiti unafanyika kwa sababu kadhaa; moja ni ubishi na kutokuamini, mbili ni wanazuoni wanapitaka kujibu maswali yanayojitokeza, tatu inaweza kuwa hali tu ya kutaka kujua (inqusitive attitude).
Kwenye lile la kwanza na la puli kunakuwa na nadharia kadhaa zinazojaribu kujazia vile ambavyo havijaelezwa kwenye maandiko. Maana maandiko hayajaandikwa ili sisi tuelewe na tuweze kuelezea kila kitu (maana hiyo itafanya sisi tuwe na uwezo wa ubongo kama wa Mungu). Hivi vimeandikwa ili sisi tuamini kwamba Yesu ni Kristo na kwa kufanya hivyo tuweze kuokolewa.
Basi kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu hiki. Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.
Yn 20:30‭-‬31 SUV
 
Mkuu hapa mjadala sio Yesu alizaliwa mwaka gani issue ni kwanini Biblia inakinzana kipindi alichozaliwa Yesu

Je ni wakati wa sensa au wakati wa uhai wa Herode?

Embu jibu hili mjadala ufungwe
Kaka Zitto junior, Biblia haikinzani kwenye hilo. ili kupata majibu nitaanza na kitu rahihisi kabisa; Injili ya Luka na kitabu cha Matendo vyote vimeandikwa na Luka, sasa tuangalie mistari miwili moja ni hiyo Luka 1:1" In those days Caesar Augustus issued a decree that a census should be taken of the entire Roman world. 2(This was the first census that took place while Quirinius was governor of Syria.)" na mwingine ni Matendo 5:37, hapa Luka anaeleza jinsi kuhani mkuu alivyowaeleza wakuu wa Sanhedrin kwamba vitu ambavyo sio vya kimungu vinakufaga kifo cha kawaida, kama ilivyokuwa kwa huyo jamaa Yuda Mgalilaya ambayo ilifanyika wakati wa sensa. ukihitaji kupata ufafanuzi wa kuwepo kwa sensa mbili na kwanini Kirenio awe 'gavana' mara mbili soma andiko la kizuoni: Brindle, Wayne, "The Census and Quirinius: Luke 2:2" (1984). SOR Faculty Publications and Presentations. 73. The Census and Quirinius: Luke 2:2.

Kwa kifupi kwa wale ambao watashindwa kuisoma paper yote ni kwamba Kirenio (Quirinius) alikuwa Jemedari hodari aliyeweza kuzima uasi Jimbo la Asia hivyo alikuwa anashughulikia masuala ya kijeshi na usalama chini ya Gavana wa Syria aliyekuwepo, ambaye baadaye alimbadili na yeye kupewa hicho cheo 6-8 AD. Na kwa nini iRome ifanye sensa wakati mtawala ni Herode; rahisi tu: mwishoni wa utawala wa Herode mkuu, alifanya vitu vya kumkasirisha sana Kaisari, ambaye aliamuru sensa hiyo ifanyike, lakini haikufanyika kwa askari wa Rumi kutumika ila Herode mwenyewe chini ya shikizo la Rumi alifanya.
 
Corona inaua chukua tahadhari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…