Bible Mysteries: Q source iko wapi

Bible Mysteries: Q source iko wapi

Sifurahi kujadili vitabu vya dini maana karibu vyote huwa na vidosari vidogo vidogo although huwa vimeandikwa kwa coding maalum zenye kuweza ku curse au tuseme huwa ina maneno maumbo ambayo ni maneno marahisi tu lakini nyuma yake hushikwa na certain holy spirit kutokana na hidden special codings
viewpoint nzuri ,sana lakini sio vidosari vidogovidogo ni dosari kubwa hiyo.
 
Hili swali la msingi sana, lingejibiwa vizuri kama tungekuwa na wanahistoria wabobezi humu ndani.
 
Umeingia kulinganisha Biblia na vitabu vya watu wengine badala ya kumjibu muuliza swali
Ok hiyo common source usilazimishe. Hiyo ipo kwenye dini nyingine. Yesu alijua kusoma na kuandika na alipokuwa anaondoka aliaga vizuri sana na aliacha maagizo kibao. Lakini hakuyaandika na alijua mapungufu ya mitume wake hata yeye mwenyewe walimzingua sana.

Common source ndio kushushwa. We acha ilivyo kama ilivyo.

Kwa taarifa yako hata hao wenye common source wana contradiction. Sababu wewe ni mwanazuoni tumia intanet ikusaidie utaona hao wenye common source pia wana contradiction.

Sasa hiyo ni balaa wakidai source yao ni Mwenyezi Mungu mwenyewe halafu wana contradiction.
 
Uzuri wa hapa hulazimishwi kujadili unaweza kupita kimya kimya, nyuzi ziko nyingi sana.
Halafu vitabu vyote vya dini tofauti sio sawa ni tofauti sana, kusema vyote huwa na dosari ndogo ndogo haina maana yoyote.
Sifurahi kujadili vitabu vya dini maana karibu vyote huwa na vidosari vidogo vidogo although huwa vimeandikwa kwa coding maalum zenye kuweza ku curse au tuseme huwa ina maneno maumbo ambayo ni maneno marahisi tu lakini nyuma yake hushikwa na certain holy spirit kutokana na hidden special codings
 
Uzuri wa hapa hulazimishwi kujadili unaweza kupita kimya kimya, nyuzi ziko nyingi sana.
Halafu vitabu vyote vya dini tofauti sio sawa ni tofauti sana, kusema vyote huwa na dosari ndogo ndogo haina maana yoyote.
It touch beliefs sasa kukosoa kosoa imani za waaminio jambo fulani ok....😛😛
 
Kwenye jamii zilizostaaribika kwa kiwango cha juu mijadala ya kukosoa na kuonyesha jinsi gani imani fulani haina mashiko ni jambo la kawaida sana. Inasaidia pia kuepusha utapeli wa kiimani na majanga kama ya kibwetere au Kinjekitile.
It touch beliefs sasa kukosoa kosoa imani za waaminio jambo fulani ok....😛😛
 
Habari za jioni wana JF, ni muda mrefu kidogo sijaweka mada humu ila leo tupate wasaa kidogo tukumbushane mambo machache kuhusu Bible.

NB: Angalizo hii mada ni purely objective tusiiweke kidini na kuanza kashfa, matusi na kejeli kwa imani fulani. Natamani iwe hoja juu ya hoja ili wote tujifunze.
View attachment 1703065

Utangulizi
Kumekua na contradiction sana kwenye vitabu vya gospel hata kwa vitu vidogo tu mfano tarehe ya Yesu kuzaliwa na kufa ama Story ya wale wafungwa pembeni ya Yesu msalabani n.k. Na huu mkinzano unawapa fursa watu kuiona Biblia kama nadharia tu au hadithi za kufikirika (Myhtology) na sababu kuu ni taarifa kadhaa kukinzana.

Kutokuwepo kwa vyanzo halisi vya injili nayo imekua changamoto na inafikia wakati watu wanahoji uhalisia wa matukio ya kipindi cha Yesu. Yaani yalikua verified wapi ama version ipi ya vitabu vya injili ni credible zaidi. Ili kusolve haya yote wanatheolojia walijaribu kujikita katika kutafuta vyanzo vya vitabu vya injili.

Q Source
Msimamo uliopo kwenye ulimwengu wa kitheolojia na imani ni kwamba kitabu cha kwanza kuandikwa ni Marko maana ushahidi ni kwamba Mathayo na Luka wamenakiri masuala mengi kutoka injili ya Marko. LAKINI kuna maandiko yaliyopo katika Mathayo na Luka ILA hayapo kwenye injili ya Marko. Hiko chanzo cha pili kikapewa nickname ya Q yaani Quelle source.
View attachment 1703067
Chanzo hiki kina nadharia mbili kwanza; ni simulizi za moja kwa moja walizosikia hao waandishi wa Mathayo na Luka kutoka kwa Yesu na wanafunzi wake. Nadharia ya Pili ni kwamba ni maandiko yaliyoandikwa yakiwa na yamenakiriwa original kabisa kutoka kwa Yesu ama wanafunzi wake.

Kupitia nadharia ya pili swali linakuja.... Je Q source iliandikwa na nani?

Q source kwanini isingekua kitabu kabisa kwenye Biblia?

Je kilifichwa ili kuondoa ukweli wa taarifa fulani?

Kuondoa Sintofahamu
Ikumbukwe kma Q source ni original script yenye uhalisia zaidi. Ingesaidia kuondoa sintofahamu hasa kwa kukinzana kwenye masuala kadhaa ya kibiblia mfano nitoe

Mathayo 2:1 inaonyesha Yesu alizaliwa kipindi cha Herode (4 BC) ila Luka 2:2-3 inaonyesha Yesu alizaliwa kipindi cha Governor Quirinius (6 AD). Ila kungetumika source moja tu mfano hyo Q source ingesaidia kuondoa discrepancy zote zilizopo na kuweka msimamo mmoja wa Injili.

Mat 12:39 Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona

Marko 8:12
12 Akaugua rohoni mwake, akasema, Mbona kizazi hiki chatafuta ishara? Amin, nawaambieni, Hakitapewa ishara kizazi hiki.

Mfano hapa je mtu wa kizazi kile ataamini kipi? Yesu alitoa ishara ama hakutoa yoyote? Je haiwezi mchanganya mtu kiimani?
View attachment 1703066
Hitimisho
Nimeleta mada ili tujadili hapa je Q source ipo? Na kama Ipo Iko wapi? Je ingeweza kusaidia kuondoa ukinzano? Je ukinzano huu wa injili hauondoi credibility ya Biblia kma kitabu kitakatifu (maana tunaamini imeandikwa kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu)

Karibuni kwa mjadala
Mada ni juu ya Biblia. Unasema mada ni purely objective tusiiweke kidini. Unawezaje kuzungumzia Biblia bila kuzungumzia dini ya Kikristo?
 
Kwenye jamii zilizostaaribika kwa kiwango cha juu mijadala ya kukosoa na kuonyesha jinsi gani imani fulani haina mashiko ni jambo la kawaida sana. Inasaidia pia kuepusha utapeli wa kiimani na majanga kama ya kibwetere au Kinjekitile.

1000 Mistakes in the Qur’an​

FROM BOOK “1000 MISTAKES IN THE QURAN”
Tafuta kitabu hiki ukisome
 
Mada ni juu ya Biblia. Unasema mada ni purely objective tusiiweke kidini. Unawezaje kuzungumzia Biblia bila kuzungumzia dini ya Kikristo?
Udini ni pale unaposhambulia mada au mtoa mada kwa ubishano wa kidini (kulinganisha na dini nyingine); mfano kuna mtu hapo juu kanizodoa kwamba ''mtume'' wangu alikua hajui kusoma wala kuandika!!

Yaani kukashifiana kidini badala ya kujenga hoja ndio ambacho napinga
 
zitto junior ukiisoma Biblia kwa kuongozwa na roho wa Mungu hautaona contradiction yoyote kwa sababu utaisoma kwa ufahamu kutoka juu, lakini ukiisoma kwa hiki unachokiita objectivity pekee utapotea, kama wengi walivyopotea.

Kwa mfano hicho unachokisema kama ni contradiction kati ya mathayo 2:1 na Luka 2:2-3 hakipo hivyo,

Angalia.
Mathayo 2:1 "Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode..."

ni Kwamba Herode alikuwa ni Mfalme wa wayahudi kama walivyokuwapo wengine huko nyuma kama kina Daudi, Suleiman etc alikuwa anatawala hayo maeneo tunayaita Israel + leo

Na
Luka 2:1 "Siku zile Amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba iandikwe orodha ya watu wote wa ulimwengu, Orodha hii ndiyo ya kwanza iliyoandikwa hapo kirenio alipokuwa liwali wa shamu. watu wote wanaenda kuandikwa, kila mtu mjini kwao

Hapa anazungumziwa Kaisari Augusto aliyekuwa Mfalme wa Roma. ambaye wakati huo alikuwa anatawala ulimwengu mzima.

sasa hapo contradiction ni nini?
 
Hivi hao walioadika biblia walikuwa wanafunzi WA yesu?.na walikuwa wote na yesu?
SHALOM! Zitto Jr.

Kwanza Kabisa pongezi kwako kwa Utafiti na uchunguzi wa Maandiko!
Vitabu vya Injili vyote - Four Gospel kwa jina moja vinajulikana kama Synopsis kutokana na Ujumbe zilioubeba unafanana kwa ukaribu sana.

Mathayo - Amejikita katika katika Ukoo wa Yesu.
Luka - ameeleza Maisha ya Yesu kwa Ujumla wake bila Kubakiza.
Marko - inakazia matendo,Uthabiti na Uimara wa Misheni ya Yesu
hasa hasa mwishoni mwa maisha yake.
Yohana - Anamweleza YESU kwa Nafasi ambayo injili zote hazijamueleza kabisa,Yaani Ukuu na Uungu wa YESU,Mamlaka na Nafasi yake Katika Utatu Mtakatifu - Kifupi Inaeleza Mamlaka Makuu ya YESU kama MUNGU.

Nani aliviandika Vitabu haina Maana sana kwangu Mimi niungane na Mchangiaji mwenzangu aliyepita - Kikubwa ni Ujumbe Mahususi uliobebwa hapo.

Hiyo unaoiiita Q Theory ni Nadharia ya Watu wadadisi ambao hauwezi kujibiwa kwa urahisi kiasi hicho - Mtu katengeneza Swali ambalo ni uhakika linatokana na Utofauti wa maneno machache sana ambayo hayapotezi maana ya Msingi (Intellectual arguments).

Mfano :- Mathayo 2:1 inaonyesha Yesu alizaliwa kipindi cha Herode (4 BC) ila Luka 2:2-3 inaonyesha Yesu alizaliwa kipindi cha Governor Quirinius (6 AD). Ila kungetumika source moja tu mfano hyo Q source ingesaidia kuondoa discrepancy zote zilizopo na kuweka msimamo mmoja wa Injili.

JIBU:- YESU alizaliwa Wakati wa Utawala wa WARUMI,Rumi iliitawala Yerusalemu na kuweka Indirect Rule ili kutosababisha Sintofahamu za utofauti wa Mila na Desturi za Wayahudi na Warumi ( HAWACHANGAMANI KABISA NA MATAIFA - GOYIM). Ndio maana wakaruhusu awepo Mtawala anayejua Mambo yao HERODE.
Hivyo kwa mantiki hiyo hakuna Utofauti hapo - Herode alikuwepo na Warumi walikuwepo - Overlapping.

Mwisho - Yapo mambo mengi yenye Utofauti kwa Mfano Kwenye Mathayo 7:7 ... Yesu ametumia mfano wa JIWE na MKATE, kwenye Marko akiyarudia Maneno yale yale ametumia Mfano wa YAI na NGE. - Maneno Tofauti Maana Ile ile.
No big Deal here.

Ikumbukwe hayo yalioandikwa ni machache sana ya yale yaliyotukia katika Maisha ya YESU - Biblia imelisema hili vema kabisa,kuwa iwapo yote yangeliandikwa isingetosha...

Asante .
 
Original source is Original, Roho Mtakatifu ni MKWELI na Msafi hawezi acha Ujumbe Mahususi upotoshwe au uharibike.
Nashukuru kwa hoja yako Ingawa official dating ya kuzaliwa Yesu sio conclusive mpaka leo yaani its either 4 BC au 6 AD ikimaanisha hakuna straight fact to prove one date is indeed right.
So tunachojiuliza sensa ilifanyika kipindi cha Quirinius ambapo alikua anaitawala Judaeah directly bila kupitia kwa Herode/mwakilishi yeyote. So far sensa ilifanyika 6 AD je Herodius alikuwepo?

So tuachane na 1 AD tujikite kwenye sensa ya 6AD ndio mzizi wa contradiction

2. Kuhusu fact kupotoshwa nmetoa mfano hapo juu kwamba wezi wawili wamezungumziwa tofauti na hizo gospels. Mmoja anadai Wezi wote walimkejeli Yesu pale msalabani, ilihali mwingine anadai Mmoja alimkiri Yesu na mwingine alimkejeli. Fact kma hii kupindishwa huoni inaharibu mafundisho kwamba Yesu at a breaking point bado alikua na huruma/msamaha kwa mwanadamu?

Natanguliza shukrani
 
zitto junior ukiisoma Biblia kwa kuongozwa na roho wa Mungu hautaona contradiction yoyote kwa sababu utaisoma kwa ufahamu kutoka juu, lakini ukiisoma kwa hiki unachokiita objectivity pekee utapotea, kama wengi walivyopotea.

Kwa mfano hicho unachokisema kama ni contradiction kati ya mathayo 2:1 na Luka 2:2-3 hakipo hivyo,

Angalia.
Mathayo 2:1 "Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode..."

ni Kwamba Herode alikuwa ni Mfalme wa wayahudi kama walivyokuwapo wengine huko nyuma kama kina Daudi, Suleiman etc alikuwa anatawala hayo maeneo tunayaita Israel + leo

Na
Luka 2:1 "Siku zile Amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba iandikwe orodha ya watu wote wa ulimwengu, Orodha hii ndiyo ya kwanza iliyoandikwa hapo kirenio alipokuwa liwali wa shamu. watu wote wanaenda kuandikwa, kila mtu mjini kwao

Hapa anazungumziwa Kaisari Augusto aliyekuwa Mfalme wa Roma. ambaye wakati huo alikuwa anatawala ulimwengu mzima.

sasa hapo contradiction ni nini?
Mkuu wakati Herodius yuko hai haikuwahi fanyika sensa ila Quirinius akiwa Governor wa Syria (inadaiwa cheo cha Herode kilifutwa by then na Walikua wanatawaliwa moja kwa moja) ndipo sensa ilifanyika.

Ssa swali ni kwamba Yesu alizaliwa kipindi cha utawala wa Herodius (indirect rule) au Quirinius (Direct rule) mind you sensa ilifanyika kipindi cha direct rule ambapo Herodius aliyekuepo alishakufa!!?

Hpa ndio mtihani ulipo
 
Okay, hii ni issue ya calenda sasa, kumbuka Biblia haitumii kalenda iliyotumika kuandika historia unazofanyia reference mkuu.
 
Mkuu wakati Herodius yuko hai haikuwahi fanyika sensa ila Quirinius akiwa Governor wa Syria (inadaiwa cheo cha Herode kilifutwa by then na Walikua wanatawaliwa moja kwa moja) ndipo sensa ilifanyika.

Ssa swali ni kwamba Yesu alizaliwa kipindi cha utawala wa Herodius (indirect rule) au Quirinius (Direct rule) mind you sensa ilifanyika kipindi cha direct rule ambapo Herodius aliyekuepo alishakufa!!?

Hpa ndio mtihani ulipo
Tupe ushahidii wa kibiblia ukionyesha Herodius unayemsema alikuwa ameshakufa wakati sensa inafanyakika. Na alifariki miaka mingapi huko nyuma kabla ya sensa.

Je, uwekaji kumbukumbu kwenye historia kwa kutumia matukio unakiwa uwe exactly? Namaanisha kuweka tarehe kwa kutumia matukio.
 
Back
Top Bottom