kinyama nje
JF-Expert Member
- Jul 3, 2017
- 1,839
- 2,475
Watumi walijifungia nakutupa kitabu chenye mafumbo na kuondoa vitabu ambavyo havina contradiction
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ushauri tu, tunapoangalia historia ya kale, detai ndogo kama hii tunaweza kuikosa ikatusababishia tukakosa, mbingu. Luka alijua anachoandika na ili asimchanganye Theofilo mtukufu, aliyekuwa mlengwa wa vitabu vyote viwili, ilibidi aweke bayana kwamba Yesu alizaliwa kwenye ile orodha (sensa) ya kwanza na si hii ya pili ambayo ilikuwa inakumbukwa zaidi na wayahudi (maana ilifanywa na warumi kutumia askari wao ambao walikuwa machikozo kwa wayahidi maana walimwabudu Kaisari na ngao zao na bendera zilikuwa na sanamu).Kaka Zitto junior, Biblia haikinzani kwenye hilo. ili kupata majibu nitaanza na kitu rahihisi kabisa; Injili ya Luka na kitabu cha Matendo vyote vimeandikwa na Luka, sasa tuangalie mistari miwili moja ni hiyo Luka 1:1" In those days Caesar Augustus issued a decree that a census should be taken of the entire Roman world. 2(This was the first census that took place while Quirinius was governor of Syria.)" na mwingine ni Matendo 5:37, hapa Luka anaeleza jinsi kuhani mkuu alivyowaeleza wakuu wa Sanhedrin kwamba vitu ambavyo sio vya kimungu vinakufaga kifo cha kawaida, kama ilivyokuwa kwa huyo jamaa Yuda Mgalilaya ambayo ilifanyika wakati wa sensa. ukihitaji kupata ufafanuzi wa kuwepo kwa sensa mbili na kwanini Kirenio awe 'gavana' mara mbili soma andiko la kizuoni: Brindle, Wayne, "The Census and Quirinius: Luke 2:2" (1984). SOR Faculty Publications and Presentations. 73. The Census and Quirinius: Luke 2:2.
Kwa kifupi kwa wale ambao watashindwa kuisoma paper yote ni kwamba Kirenio (Quirinius) alikuwa Jemedari hodari aliyeweza kuzima uasi Jimbo la Asia hivyo alikuwa anashughulikia masuala ya kijeshi na usalama chini ya Gavana wa Syria aliyekuwepo, ambaye baadaye alimbadili na yeye kupewa hicho cheo 6-8 AD. Na kwa nini iRome ifanye sensa wakati mtawala ni Herode; rahisi tu: mwishoni wa utawala wa Herode mkuu, alifanya vitu vya kumkasirisha sana Kaisari, ambaye aliamuru sensa hiyo ifanyike, lakini haikufanyika kwa askari wa Rumi kutumika ila Herode mwenyewe chini ya shikizo la Rumi alifanya.
Mbona unaenda mbele na kurudi nyuma? Nilijua umefunga mjadala.Luka anasema enzi za Sensa yaani 6 AD
Mathayo anasema enzi za Herode yaani 4 BC
Embu jikite hapo kwanini wanakinzana?
Bwege tu hana lolote, anadhani wabongo weupe kichwaniZitto junior akili kubwa sana...nafatilia mjadala hapa...
Waliokichapa, waliokisafirisha je? Au Waliokiandaa hawajaingia gharama yoyote?Kabla hatujaenda mbali mm nilitaka kujuzwa kwann biblia ina copy rights ( haki miliki) je hiyo pesa ya copy rights huwa analipwa nan?
Nawasilisha!
Ingekuwa hatari kuuUsipate shida sana. Biblia imeandikwa na wanadamu kuna historia, unabii,mashairi, n.k. msingi mkuu ukiwa ni ujumbe maalum.
Sijui ingekuwaje kama ingesemekana ilishushwa, halafu ukute kuna vitu humo havijakaa sawa.
Nimeisoma paper nzima na sijaona popote panapo na conclusive evidence ya Kulink Quirinius na ''census'' ya 5 BC na ndio maana conclusion yake ni hii hapa.: Brindle, Wayne, "The Census and Quirinius: Luke 2:2" (1984). SOR Faculty Publications and Presentations. 73. The Census and Quirinius: Luke 2:2.
Mkuu hakuna anayepinga uwepo wa sensa mbili nachopenda utufahamishe ni hikiLuka alijua anachoandika na ili asimchanganye Theofilo mtukufu, aliyekuwa mlengwa wa vitabu vyote viwili, ilibidi aweke bayana kwamba Yesu alizaliwa kwenye ile orodha (sensa) ya kwanza na si hii ya pili
Paper uliyoweka inakiri kuwa sensa ya kwanza haikua documented popote. Can u adress this?Kwa hiyo Yesu alizaliwa wakati wa sensa ya kwanza na Herode alikuwa hai, no contradictions!
Hakuna tofauti kwa maana Kaisari ndio kiongozi mkuu na Herode alikuwa chini ya Kaisari.SHALOM! Zitto Jr.
Kwanza Kabisa pongezi kwako kwa Utafiti na uchunguzi wa Maandiko!
Vitabu vya Injili vyote - Four Gospel kwa jina moja vinajulikana kama Synopsis kutokana na Ujumbe zilioubeba unafanana kwa ukaribu sana.
Mathayo - Amejikita katika katika Ukoo wa Yesu.
Luka - ameeleza Maisha ya Yesu kwa Ujumla wake bila Kubakiza.
Marko - inakazia matendo,Uthabiti na Uimara wa Misheni ya Yesu
hasa hasa mwishoni mwa maisha yake.
Yohana - Anamweleza YESU kwa Nafasi ambayo injili zote hazijamueleza kabisa,Yaani Ukuu na Uungu wa YESU,Mamlaka na Nafasi yake Katika Utatu Mtakatifu - Kifupi Inaeleza Mamlaka Makuu ya YESU kama MUNGU.
Nani aliviandika Vitabu haina Maana sana kwangu Mimi niungane na Mchangiaji mwenzangu aliyepita - Kikubwa ni Ujumbe Mahususi uliobebwa hapo.
Hiyo unaoiiita Q Theory ni Nadharia ya Watu wadadisi ambao hauwezi kujibiwa kwa urahisi kiasi hicho - Mtu katengeneza Swali ambalo ni uhakika linatokana na Utofauti wa maneno machache sana ambayo hayapotezi maana ya Msingi (Intellectual arguments).
Mfano :- Mathayo 2:1 inaonyesha Yesu alizaliwa kipindi cha Herode (4 BC) ila Luka 2:2-3 inaonyesha Yesu alizaliwa kipindi cha Governor Quirinius (6 AD). Ila kungetumika source moja tu mfano hyo Q source ingesaidia kuondoa discrepancy zote zilizopo na kuweka msimamo mmoja wa Injili.
JIBU:- YESU alizaliwa Wakati wa Utawala wa WARUMI,Rumi iliitawala Yerusalemu na kuweka Indirect Rule ili kutosababisha Sintofahamu za utofauti wa Mila na Desturi za Wayahudi na Warumi ( HAWACHANGAMANI KABISA NA MATAIFA - GOYIM). Ndio maana wakaruhusu awepo Mtawala anayejua Mambo yao HERODE.
Hivyo kwa mantiki hiyo hakuna Utofauti hapo - Herode alikuwepo na Warumi walikuwepo - Overlapping.
Mwisho - Yapo mambo mengi yenye Utofauti kwa Mfano Kwenye Mathayo 7:7 ... Yesu ametumia mfano wa JIWE na MKATE, kwenye Marko akiyarudia Maneno yale yale ametumia Mfano wa YAI na NGE. - Maneno Tofauti Maana Ile ile.
No big Deal here.
Ikumbukwe hayo yalioandikwa ni machache sana ya yale yaliyotukia katika Maisha ya YESU - Biblia imelisema hili vema kabisa,kuwa iwapo yote yangeliandikwa isingetosha...
Asante .
Tukubaliane jambo moja kwamba Luka alikuwepo karne ya kwanza, aliandika kitabu chake wakati mashahidi wa haya yaliyotokea walikuwa hai, alichoandika kuhusu uwepo wa Kirenio kama "hégemoneuó" ambayo Strong ana define kama - "to command" na watafsiri wameitafsiri kama liwali au Gavana haitupi conclusion kwamba Luka alikosea au alichakachua kwa makusudi. Jambo la muhimu hapa ilikuwa kuonyesha uwezekano wa Kirenio kuwa na "comanding position" huko Syria wakati Herode akiwa mfalme. Kuhusu ushahidi ni kuwa very unfare ukitaka proff ya jambo ambalo witness ni watatu tu: Luka, Josephus, na Tacitus. Kukosekana ushahidi sio proof ya kutokuwepo tukio halisi. ni miaka 2020 na ushee imepita tangu hayo yatukie, kuna vitu sisi leo tunaweza kuviona ni muhimu ila kwa yule aliyeandika enzi zile wala hakuona ni kitu cha kufafanua maana kilikuwa wazi au trivial enzi hizo.Paper uliyoweka inakiri kuwa sensa ya kwanza haikua documented popote. Can u adress this?
Pili luke 2:2 inadai Sensa ya kwanza Quirinius alikuwepo, ssa kivp tena sensa ya kwanza iwe enzi za Herode ilihali Krenio hakua governor?
Hii discrepancy ndio kiini cha debate
Shukrani kwa huu mchango wako uliopangiliwa wa hoja na maandiko.UNABII WA DANIEL UNAONESHA VZR ATABATIZWA,KUUWAWA KATIKA MIAKA 27B.C NA 31B.C, HIVO UTAWEZA KUJUA PIA ALIZALIWA LINI
Danieli 9:25 “Basi ujue na kufahamu, ya kuwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake…”
Yerusalemu ulianza kujengwa upya katika mwaka 457 KK kwa amri ya mfalme Artashasta
Unabii unasema kutakuwa na wiki 7 kujumlisha wiki 62 jumla 69 kutoka kujengwa Yerusalemu mwaka 457K.K. hadi kuja kwa masihi. Katika unabii siku moja ni sawa na mwaka mmoja (angalia Ezekieli 4:6 na Hesabu 14:34), hivyo wiki 69 ambazo ni sawa na siku 483 zinamaanisha miaka 483 halisi; ambayo ingepita tangu kujengwa upya kwa Yerusalemu hadi kuja kwa Masihi.
Hivyo ukichukua miaka 483 ukaijumlisha katika mwaka -457 KK ambao Yerusalemu ulianza kujengwa, utapata mwaka 27 BK (-457 483 = 27); ambao Masihi angetiwa mafuta.
View attachment 1709542
Je Mashi alitiwa mafuta mwaka 27 BK?
Matendo 10:38 “habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.”
Masihi = aliyetiwa mafuta.
Hivyo kulingana na unabii Yesu alibatizwa au kutiwa mafuta katika mwaka 27 BK mwishoni mwa wiki 69, na Luka anatuambia Yesu alikuwa na umri wa miaka 30 wakati anabatizwa 27 BK.
Luka 3:21, 23 “Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu zilifunuka; Roho Mtakatifu akashuka juu yake…Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa amepata umri wake kama miaka thelathini, akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, wa Eli,”
Hii ni kwa sababu Yesu hakuzaliwa 1 BK; kwani kalenda ilikosewa kama miaka 4.
Historia inasema Herode alikufa 4 KK, na tunajua Herode alitaka kumuua Yesu, hivyo Yesu alizaliwa 4 KK na katika 27 BK alipobatizwa alikuwa na umri wa miaka 30.
MWAKA -4 30 1 = Unapata hadi miaka 27 ya YESU anapobatizwa (Namba “1” ipo kwa ajiri ya mwaka “0”)
Hivyo Yesu alibatizwa mwaka 27BK. (majuma 69 au miaka 483) kutoka mwaka 457KK hadi 27BK. Hivyo unabii ulitimia kwa ukamilifu, kama ulivyotabiliwa kuwa tangu kujengwa Yerusalemu mwaka 457KK mpaka kuja kwake masihi kungekuwa na majuma 69 au miaka 483.
Kwa hakika Yesu mwenyewe alisema wazi kwamba unabii ulikuwa umetimia kikamilifu.
Marko 1:9, 14, 15 “Ikawa siku zile, Yesu alikuja kutoka Nazareti ya Galilaya, akabatizwa na Yohana katika Yordani…Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya Mungu, akisema, Wakati umetimia…”
Yesu alijua kwamba mwaka 27BK. unabii wa Danieli ulikuwa umetimia.
JE YESU ALIKUFA LINI?
TUMSIKILIZE TENA NABII DANIEL
Danieli 9:27 “Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja;…”
Yesu alipobatizwa ilikuwa ni wiki ya 69, hivyo katika wiki 70 zilizotolewa kwa ajili ya taifa la Israeli ilikuwa imebaki wiki moja tu muda wa rehema ya taifa lao uishe. Hivyo kwa muda wa juma hili moja lililobaki Yesu na wanafunzi wake waliitangaza Injili ya Mungu kwa Waisraeli pekee yao. Hawakutangaza Injili mahali pengine popote tofauti na Israeli. Yesu mwenyewe aliwaamru wanafunzi wake SOMA...
Mathayo 10:5, 6
Tumejua kwamba kwa juma moja Yesu angefanya agano na watu wengi, lakini Injili ingehubiriwa kwanza kwa Israeli pekee. Sasa Je juma moja linamaanisha nini?
Juma moja = siku 7. Katika unabii siku = mwaka, hivyo juma moja = miaka 7. Muda huu ulianzia mwaka 27BK alipobatizwa Yesu, na unaendelea mpaka 34BK (27+7 = 34).
Katikati ya juma.
Danieli 9:27 “…Na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu;…”
Juma zima = miaka 7, hivyo nusu ya juma ni miaka 3 na nusu (7 / 2 = 3.5). Ukihesabu miaka mitatu na nusu kutoka katika mwaka 27BK. aliobatizwa Yesu utapata mwaka 31BK. Hivyo Yesu angekomesha sadaka na dhabihu, au angesulubiwa msalabani, au “angekatiliwa mbali,” Dan. 9:26 katika mwaka 31BK. Kwa hiyo Yesu alifanya kazi yake ya utumishi kwa muda wa miaka 3 na nusu, tangu 27BK hadi 31BK aliposulubishwa msalabani.
Mathayo 27:50-51 “Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake. Na tazama pazia la hekalu lakapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;”
Pazia lilichanika kuonesha kwamba hatupaswi kutoa tena sadaka wala dhabihu kwa ajili ya msamaha wa dhambi na upatanisho; bali tunapaswa kumwangalia Yesu pekee kwa ajili ya vitu vyote hivyo.
Rehema kwa taifa la Israeli yaisha.
Juma moja la mwisho ambalo lilianza 27 BK lingeisha mwaka 34 BK, nusu ya juma ni miaka 3.5 ambayo Yesu alifanya kazi yake tangu 27 BK alipobatizwa hadi 31 BK aliposulubishwa. Hivyo katika juma la mwisho (la 70), ilikuwa imebaki nusu juma (miaka 3 na nusu) pekee ambayo ingeishia 34 BK; kwa ajili ya Wayahudi. Kama Wayahudi wangendelea kumkataa Mwana wa Mungu hadi 34 BK, ndipo Mungu angeuondoa ufalme kwao na kuwapa watu wa mataifa. Je Wayahudi walimkubali Yesu kabla ya mwaka 34 BK au waliendelea kuwa wakaidi? Wayahudi walithibitisha kuikataa kabisa rehema yao ya majuma 70 kwa kumwua Stefano katika 34 BK!
Matendo 7:56-59 “Akasema, Tazama? naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kuume wa Mungu. Wakapiga kelele kwa sauti kuu, wakaziba masikio yao, wakamrukia kwa nia moja, wakamtoa nje ya mji, wakampiga kwa mawe…stefano, naye akiomba, akisema , Bwana Yesu, pokea roho yangu.”
Yesu alipopaa mbinguni wanafunzi wake waliendelea kuhubiri Injili kwa Wayahudi. Lakini majuma 70 yalipoisha katika mwaka 34BK, Wayahudi waliukataa wazi wazi ujumbe wa Injili kwa kitendo cha kumuua Stefano. Hivyo unabii wa Yesu ulitimia, Wakanyanganywa ufalme wa Mungu nao wakapewa watu wa mataifa.
Mathayo 21:43 “Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake.”
Unabii ulitimia majuma 70 kwa ajili ya Wayahudi yalipoisha nao wakathibitisha kuikataa Injili, Mitume wakageukia kuhubiri kwa watu wa mataifa.
.View attachment 1709543
HITIMISHO;
YESU KAZALIWA MWAKA 4K.K, KABATIZWA MWAKA 27B.K AKIWA NA MIAKA 30,KAFA MSALABANI MWAKA 31B.K
Marejeo:
1. Kwa ushahidi kuhusu tarehe 457KK, ni mwaka wa saba wa kutawala kwake mfalme Artashasta, ambaye katika mwaka 457KK aliamuru mji wa Yerusalemu ujengwe; angalia, S.H. Horn na L.H. Wood, The Chronology of Ezra 7 (Washington, D.C.: Review and Herald association, 1953); na E.G.Kraeling, The Brooklyn Museum Aramaic Papyri (New Haven or London, 1953,) ukr. 191-193
MkuuMkuu Yesu alisema kwenye kitabu cha ufunuo kwamba watu wasiongeze au kupunguza kitu kutoka kwa maneno yake.
Ssa huo ukinzano wa baadhi ya mistari ya vitabu vya injili hauoni vinakiuka maagizo yake?
Je huoni ingetumika source moja kuu say Q source ingesolve changamoto hii?