Biblia inaonesha kurejea vitabu vingi ambavyo havipo: Je, kuna siri imefichwa?

Biblia inaonesha kurejea vitabu vingi ambavyo havipo: Je, kuna siri imefichwa?

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,151
Reaction score
4,277
Katika mambo yanayoshangaza ni namna Biblia inavyoonesha kurejea vitabu vingi ambavyo havipo ndani yake. Swali la kujiuliza ni je vitabu hivyo vimetajwa tu havipo au vimeondolewa? Na kama vimeondolewa ni kwa nini? Ni nani anafaidika na kutokuwepo kwa vitabu hivyo?

Angalia namna maandiko haya yafuatayo yanayoonesha uwepo wa vitabu vingine zaidi ya vilivyozoeleka:

2 Mambo ya nyakakati 12:14&15 " Naye akatenda yaliyo maovu, Kwa kuwa hakuutunza moyo wake amtafute BWANA. 15 Basi mambo yake Rehoboamu ya kwanza na ya mwisho je hayakuandikwa katika tarehe za Shemaya nabii na Ido mwonaji kwa jinsi ya kuandika nasaba?....Hapa inaonesha mambo ya Yeroboamu aliandikwa na kama yaliandikwa na yalipaswa kuwa katika makundi mawili ,Yeroboamu wa kwanza na Yeroboamu wa pili. Yaliandikwa katika tarehe za Shemaya. Je kitabu cha Shemaya kipo wapi? Nabii Ido mwonaji Je?...( Hapa kuna maarifa yamefichwa mahali).

Joshua 10:13 Ndipo jua likasimama na mwezi ukatulia, Hata Hilo Taifa lilipokuwa limekwisha jipatiliza juu ya adui zao. Hayo je hayakuandikwa ndani ya kitabu cha Yashari?...Tujiulize je yaliyoandikwa yalikuwa yapi? Na tungeyajua yangetusaidia kujifunza nini? Je kitabu cha Yashari kilichorejelewa kipo wapi? Hapa kuna maarifa tuliyopaswa kuyafahamu ila yamefichwa kwa maslahi fulani ya wachache wenye lengo fulani.

1Wafalme 14:19 Na mambo yake Yeroboamu yaliyosalia, ya kupigana na ya kutawala, tazama yameandikwa katika kitabu cha tarehe cha wafalme wa Israeli. Jiulize na wewe hiki kitabu cha tarehe cha wafalme wa Israeli linaonekana kuwa na siri za kupigana (vita) na kutawala lakini kwa nini hakipo katika Biblia zetu? Kuna kitu watu wachache wanakifahamu kwa faida yao ila wengi wetu tunapapasa tu " exoteric knowledge"

1 Wafalme 14: 29 Na mambo yake Rehoboamu yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! hayakuandikwa katika kitabu cha tarehe cha wafalme wa Yuda? (Hiki kitabu cha tarehe cha wafalme wa Yuda kipo wapi). Kwa nini kisiwekwe wazi tukajifunza mambo ya Yeroboamu?

Najiuuliza tu ni kwa nini Biblia ambayo ni kitabu kitakatifu kinatutajia vitabu ambavyo havipo ndani yake?.Swali hili ni zito sana kwangu ila nina hakika kuwa haya yote yapo Kwa kusudi fulani na kuna watu wanafadika na hali ilivyo.

1 Wafalme 16:20 Na mambo yote ya Zimri yaliyosalia na fitina yake aliyoifanya, je! hayakuandikwa katika kitabu cha tarehe cha wafalme wa Israeli?. Huyu Zimri ni nani? alifanya fitina gani? Hiki kitabu cha wafalme wa Israeli kinaonekana kuwa na mambo muhimu sana ila ndiyo hivyo kimefichwa.

1Wafalme 11:41 Nayo yaliyosalia ya Sulemani mambo yake na yote aliyoyafanya, na hekima yake, je! hayo siyo yaliyoandikwa kitabuni mwa mambo yake Sulemani? .Je kuna kitabu kinachoeleza mambo yote aliyoyafanya Sulemani? Kama yapo ni kitabu kipi? Je Mithali na Muhubiri vinatosha kuwa vitabu vya mambo yote na hekima yote ya Sulemani?. Kuna kitabu cha Sulemani hapo kimefichwa mahali.

2 Wafalme 16:11 Na tazama mambo yake Asa ya kwanza na ya mwisho, angalia yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli. Hiki kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli kipo wapi?.

Kupitia maandiko hayo machache niliyoyarejelea Biblia inaonesha wazi kuwa ilikuwa na vitabu vingi zaidi na walioviondoa kwa kujua au kutojua waliacha kufuta maandiko yaliyorejelea vitabu walivyoviondoa kwa maslahi yao.

Siyo ajabu leo kutokana na kufichwa kwa maarifa jamii kubwa ya wanadamu ikafanywa vyovyote na watu wachache sana wanaoelewa maarifa halisi na yasiyoeleweka kwa wengi. Na hapa niaiona safari ndefu gizani.
 
Umezungumzia suala la kuvutia sana kuhusu vitabu vilivyopotea vya Biblia. Ni kweli kwamba Biblia inataja vitabu vingine ambavyo havipo ndani yake, na hii imeleta maswali mengi na mjadala kwa karne nyingi.

Maswali yanayojitokeza:

Je, vitabu hivi vilivyopotea vilikuwa na maudhui gani?

Kwa nini viliondolewa kwenye Biblia?
Nani anayehusika na kupotea kwao?

Je, upotezaji huu unaathirije uelewa wetu wa Biblia na Ukristo?

Nadharia kuhusu vitabu vilivyopotea:

Kuna nadharia mbalimbali kuhusu hatima ya vitabu hivi vilivyopotea. Baadhi ya watu wanaamini kwamba viliharibiwa kwa bahati mbaya au vilipotea kwa muda.

Wengine wanaamini kwamba viliondolewa kwa makusudi na viongozi wa kidini kwa sababu waliona maudhui yao kuwa ya kukera au yenye utata.

Wengine bado wanaamini kwamba vitabu hivi bado vipo na vinaweza kugunduliwa na kurudishws siku moja.

Athari ya upotezaji wa vitabu hivi:

Upotezaji wa vitabu hivi vya Biblia unaacha pengo katika uelewa wetu wa historia na teolojia ya Kikristo. Vitabu hivi vilivyotajwa vinaweza kuwa vimetoa maelezo zaidi kuhusu matukio fulani, watu, na mafundisho yanayokumbukwa kwa ufupi katika Biblia tuliyo nayo leo. Hii inaweza kusababisha tafsiri tofauti za maandiko na hata itikadi tofauti za kidini.

Bila shaka, hatuwezi kujua kwa uhakika kilichotokea kwa vitabu hivi vilivyopotea vya Biblia. Hata hivyo, maswali na mjadala unaozunguka suala hili unaonyesha nguvu na umuhimu wa Biblia. Ukweli kwamba bado tunauliza maswali kuhusu maandiko haya baada ya karne nyingi unaonyesha kina na utata wake.

Ni muhimu kutambua:

Hakuna makubaliano ya kidini kuhusu uwepo au umuhimu wa vitabu hivi vilivyopotea.

Wataalamu wengi wa Biblia wanaamini kwamba Biblia tuliyo nayo leo ni kamili na inatosha kwa imani ya Kikristo.

Ingawa upotezaji wa vitabu hivi unaleta maswali, haimaanishi kwamba Biblia haiaminiki au haitumiki.

Ikiwa ungependa kujifunza zaidi kuhusu vitabu vilivyopotea vya Biblia, unaweza kutafiti mada zifuatazo:

Apocrypha
Gnostic Gospels
Dead Sea Scrolls
The History of the Bible
Kuna vitabu na makala nyingi zinazopatikana kuhusu mada hii, na unaweza kupata mitazamo tofauti kutoka kwa wataalamu wa Biblia na wanahistoria.

Ni muhimu kukumbuka kuwa utafiti huu unapaswa kufanywa kwa nia ya wazi na nia ya kujifunza zaidi, sio kwa nia ya kutilia shaka au kudhoofisha imani ya mtu.

Nawasilisha mkuu
 
Back
Top Bottom