Biblia kitabu cha Ajabu Sana

Hapa ndio unaona kwanini uislamu unang'ang'ania hapo Yerusalemu,wakati hapawahusu,mudi aliapatamani sana

Hapo ni mji wa Daudi ,mwana wa Yese mwana wa Obedi ,ukoo wa Yuda

Kupitia Yeye ndipo tunampata Yesu

Mungu alimuapia Daudi ,hutakosa mtu wakukaa kiti chako milele

Yesu anatajwa kama mwana wa Daudi, ndiye anakaa milele

Mungu kwa alivyompenda sana Daudi ,huko mbinguni Kuna mji wa Daudi umepewa Jina Yerusalemu mpya au Sayuni

Mungu alimpenda Daudi Hadi kampa mtaa huko mbinguni ,
 
Acha shobo na kukurupuka dogo. Wapi kasema na kuthibitisha uwepo wa Mungu wa Israel?

Pumbavu. Huwa mnaboa sana.
Hakuna Mungu wala wewe hauna uwezo wa kuthibitisha chochote zaidi ya porojo na makasiriko tu mkuu🤔🤔🤔
 
Umeandika maelezo marefu pumba tupu.
Leta dondoo kama hii hapa kuhusu Mji wa Ninawi ,Hadi Leo upo na haijajengwa sawa sawa na maneno ya manabii kwenye biblia

Soma hapa ujionee ,kuliko kupaniki ,waislamu kwanini hamtaki kutoka nje ya box muone mlibyodanganywa?


Unabii wa kuangamizwa kwa Ninawi ulitolewa hasa katika vitabu vya Nabii Nahumu na Sefania katika Biblia. Nabii Nahumu alitabiri kwamba Ninawi, mji mkuu wa Dola ya Ashuru, ungeangamizwa kwa ghadhabu ya Mungu kutokana na dhambi zake, ikiwa ni pamoja na udhalimu, ukatili, na ibada ya sanamu (Nahumu 3:1-7).

Kulingana na Biblia:

1. Kuangamizwa kwa Ninawi: Nahumu 1:8-9 na 3:19 inasema Mungu angeleta "gharika" dhidi ya Ninawi na kwamba maangamizi yake yasingekuwa na tiba. Hii ilitokea mnamo mwaka wa 612 KK wakati Dola ya Ashuru iliposhambuliwa na majeshi ya Babeli na Wamedi. Walitumia nguvu na moto kuharibu mji.


2. Kutojengwa Tena: Nahumu 3:7 inasema, "Kila mtu atakayeona maangamizi yako atakukimbia, na kusema, 'Ninawi imeangamia! Nani atamwonea huruma?'" Ninawi haikuwahi kujengwa tena baada ya kuharibiwa.

Ushahidi wa Akiolojia:

1. Ugunduzi wa Magofu ya Ninawi: Magofu ya Ninawi yaligunduliwa mnamo karne ya 19 (miaka ya 1840) karibu na mji wa Mosul, Iraq. Wanaakiolojia kama Austen Henry Layard waligundua mabaki ya mji huu, ikiwa ni pamoja na mabaki ya kuta, majengo, na maandiko ya kiashuru yaliyoandikwa kwenye vibao vya udongo.


2. Uthibitisho wa Maangamizi: Uchunguzi wa akiolojia umeonyesha tabaka za mabaki ya moto, zikiwa ni ushahidi wa kuharibiwa kwa Ninawi kama Biblia ilivyosema. Hii inathibitisha kuwa mji ulianguka ghafla kwa shambulio kubwa.


3. Kutokujengwa Tena: Tangu kuangamizwa kwake, Ninawi haijawahi kujengwa tena kama mji mkuu wa dola. Magofu yake yanabaki kuwa kumbukumbu ya unabii wa Nahumu.


Kwa hiyo, kwa kutumia Biblia na ushahidi wa akiolojia, tunaona kuwa unabii wa kuangamizwa kwa Ninawi ulitimia kikamilifu, na mji huo haujajengwa tena hadi leo.
Umeandika maelezo marefu pumba tupu.
 
Hakuna Mungu wala wewe hauna uwezo wa kuthibitisha chochote zaidi ya porojo na makasiriko tu mkuu🤔🤔🤔
Ushauri tu kwako
Jitahidini kuheshimu imani za watu. Pia msiwe mnawakwaza wengine kwa kuingiza mabishano yasiyo na maana. Mleta uzi kaleta habati za Mji wa Yerusalemu we unaleta udwanzi. JF kuna majukwaa na nyuzi nyingi, someni na wekeni nyuzi zenu zinazopinga uwepo wa Mungu na sio kila uzi kuleta ujuaji.
 
Umeandika maelezo marefu pumba tupu.
Leta mfano kama huu na ushahidi

Ugunduzi wa Maandishi ya Bahari ya Chumvi (Dead Sea Scrolls):

Ugunduzi wa Kihistoria: Maandishi haya yaligunduliwa mwaka 1947 kwenye mapango ya Qumran karibu na Bahari ya Chumvi. Yana vipande vya maandiko ya Agano la Kale (hasa Torati, Zaburi, na Isaya) yaliyoandikwa zaidi ya miaka 2,000 iliyopita.
 
Mkuu tayari nimeshakujua 😅😅😅 ila bado haujajibu hoja hapo unachokifanya nikunishambulia binafsi tu😅😅😅😅😅
 
Biblia yenyewe
Biblia ipi? Zipo biblia nyingi.
Biblia ya Mwanza
 
Biblia yenyewe
Biblia ya Mwanza
Mzee acha porojo ,ndio maana dini yenu inakosa uhalali kwa mtu mwenye tafakari , wengi wanaosoma vzr historia na Quran wanakuja kugundua ni utapeli tu, sasa badala ujibu hoja wewe unaudhalilisha uislamu unaonekana ni dini ya kuunganisha,dini inayotegemea uongo kujijenga


Nakupa mfano hapa uone jinsi ya kujenga hoja kwa kitabu chako ,Mimi najenga kutumia Biblia imetabiri Tawala zote Hadi ujio wa Yesu kupitia kitabu cha Daniel na yote yametolewa ,angalia hapa👇👇

Danieli anafasiri ndoto ya Mfalme Nebukadneza kuhusu sanamu kubwa yenye sehemu za metali tofauti, ambazo zinawakilisha falme tofauti zinazokuja.

Sehemu za Sanamu:

1. Kichwa cha Dhahabu:

Unabii: Kinawakilisha Ufalme wa Babeli (Babylon), ulioongozwa na Nebukadneza (Danieli 2:37-38).

Historia: Babeli ilikuwa falme yenye nguvu kati ya 605 KK - 539 KK, ikijulikana kwa utajiri na ustaarabu wake.



2. Kifua na Mikono ya Fedha:

Unabii: Kinawakilisha Ufalme wa Wamedi na Waajemi (Medo-Persia), ulioshinda Babeli (Danieli 2:39).

Historia: Falme hii ilitawala kutoka 539 KK - 331 KK chini ya mfalme maarufu kama Koreshi Mkuu.



3. Tumbo na Mapaja ya Shaba:

Unabii: Kinawakilisha Ufalme wa Ugiriki (Greece), uliokuja baada ya Wamedi na Waajemi (Danieli 2:39).

Historia: Ugiriki, chini ya Alexander Mkuu, ilitawala kutoka 331 KK - 168 KK, ikijulikana kwa ushawishi wake wa kitamaduni.



4. Miguu ya Chuma:

Unabii: Kinawakilisha Ufalme wa Rumi (Rome), uliokuwa wenye nguvu na wa kudumu zaidi (Danieli 2:40).

Historia: Rumi ilitawala kutoka 168 KK - 476 BK, ikiwa mojawapo ya falme kubwa zaidi duniani.



5. Vidole vya Miguu vya Udongo na Chuma:

Unabii: Kinawakilisha falme zilizogawanyika zilizokuja baada ya Rumi (Danieli 2:41-43). Udongo na chuma vinaonyesha udhaifu na nguvu za falme hizi.

Historia: Hii inahusiana na Ulaya ya kisasa, iliyokuwa na falme zilizogawanyika na zisizodumu.



6. Jiwe lililokatwa bila mikono:

Unabii: Jiwe hili linawakilisha Ufalme wa Mungu, ambao utaangusha falme zote za wanadamu na kuwa wa milele (Danieli 2:44-45).

Historia: Ufalme huu ni unabii wa kuja kwa Yesu Kristo na ufalme wa milele unaotajwa katika Biblia.
 
Biashara matangazo, hata Afrika kuna sehemu nyingi interesting na zenye historia kubwa kuanzia Misri mpaka kusini mwa jangwa la Sahara.

Walichotuzidi wenzetu sanasana ni kuandika mambo yao tangu zamani wakati huku Afrika watu waliweka oral tradition.

Kuna sehemu nyingi zenye interesting histories, ndefu kuliko ya Biblia, huko Europe, Oceania, Asia, North, Central na South America lakini hazipo kwenye Biblia.
 
Natamani sana kufika israel ipo siku nitafika hapo ukweli ukienda israel imani yako itakua sana maana utasoma biblia na kuona kwa macho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…