Shukurani.
Umeuliza swali zuri sana, linaloonesha unapenda tafakari, unafuatilia mambo kwa undani.
Definitions za mambo, katika mjadala wowote, nikitu cha awali kabisa. La sivyo, mnaweza kuzozana hata kama mnasema kitu kimoja, kwa majina tofauti tu.
Ndiyo maana hata Bertrand Russell katika insha yake "Why I amNot A Christian", hajaanza kueleza kwa nini yeye si Mkristo, kaanza kuelezea anaposema Mkristo anamaanisha nini.
Why I Am Not a Christian by Bertrand Russell - The Bertrand Russell Society
Tatizo labda hujapata muda wa kunisoma vizuri tu. Na siwezi kukukosoa kwa hilo, kwa sababu huenda ndiyo unaanza kunisoma karibuni.
Kama tukiendelea kujadiliana kwa umakini huu wa kuanza kum define Mungu, kabla ya kulumbana,t unaweza kunufaishana hata kama hatukubaliani.
Kila ninapoandika kuhusu Mungu, najitahidi sana kum define Mungu gani ninayemuongelea, ili kusudi kusiwe na mtafaruku usio na tija.
Kwa sababu kuna watu wanasema Beyonce ni mungu wao, kwa definition ya kuweza kucheza muziki na kuuza rekodi za muziki. Sasa watu hawa na definition yao hiyo ya kwamba Beyonce ni mungu siwezi kuwabishia kwamba mungu Beyonce yupo.
Mara nyingine narudia definition mara nne katikapost moja, kwa msisitizo.
Ninapoongelea Mungu, naongelea "Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote". Kama umenisoma hapo nyuma utakuwa umeona kwamba ninapoongelea Mungu, najikita kuanzia na huyu Mungu.
Kwanikimbunga na tetemeko haviathiri wanayama?
Kwani wapi nimesema kukata miti na kuchinja wanyama si uovu?
Nimeeleza hapa kwamba, kifo ni uovu. Kwa kiumbe chochote. Mtu, mnyama, mti, bacteria etc.
Na kifo kipo, kama reality of nature. Mnyamahuyu anahitaji ale ili aishi, anamuua mwingine anamla. Hana jinsi. Akisema asile mnyama, atakula mmea, kaua kiumbe pia.
Akisema asile mnyama wala mmea, atakanyaga mjusi. Kaua kiumbe.
Huu ni uovu. Kuua kiumbe chochote ni uovu.
Kwa sababu ninadra sana kukuta kiumbe kinataka kufa, na kikitaka kufa huo ni ubaya pia.
Sasa sawali langu ambalo sijajibiwa nihili, kwa nini Mungu kaumba ulimwengu ambao kifo kinawezekana, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao kifo hakiwezekani.
Ulimwengu ambao hauna tsunami litakalomuua mtu au samaki.
Kwa nini hakuumba hivyo?
Alitaka ila hakuweza? Kama alitaka ila hakuweza, je nikweli ana uwezo wote?
Ama aliweza ila hakutaka? Kama aliweza ila hakutaka, je nikweli ana upendo wote?
A perfect world is one without evil. Dunia hii inafikirika, kama unaaminiMungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendowote yupo.
Lakini, ukifikiria kisayansi, kifizikia, kwa kutumia hesabu za entropy, any existence is deviation fromperfection.
The only perfection is non existence.
Yani hata huyo Mungu anayesemwa kuwa yupo, kuwapo kwake tu niimperfection.
The only perfection fromthe perspective of entropy, is nothingness.
Hapo ndipo nakuja kwenye proof yangu kwamba Mungu hayupo.
Perfectin (by entropy) = nothingness
God = perfection
But since perfection = nothingness
God = nothingness
Therefore, God does not exists
QED.