Biblia kwa Jicho Jingine

mbona unakwepa hili swali ambalo hata mimi nilikuuliza? Mungu ninani? ukiweza kujibu hilo tu na hayo mengine yanajijibu yenyewe.
Mbona nimejibu kirefu katika ulichokinukuu?

Unajua kusoma?

Soma tena hapa.

Mungu ni wazo lililo katika vichwa vya baadhi ya watu, ambalo halina uhalisi zaidi ya kuwa wazo tu.

Wazo hili halina uhalisia(zaidi ya kuwa wazo tu) kwa sababu lina contradictions zisizotatulika, kuanzia ngazi ya wazo tu, na hivyo haliwezi kuwapo katika uhalisi.

Contradiction kubwa ni ukweli kwamba, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, kaumbaje ulimwengu unaoruhusu mabaya mengi, wakati alikuwa ana uwezo, ujuzi na upendo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya siyo tu hayawezekani kufanyika, bali pia hayawezekani hata kufikirika kwa sababu hayapo kabisa?

Mungu huyu ni sawa na wazo la "Pembetatu yenye pembe nne" katika Euclidean geometry planes.

Unaweza kuwaza wazo hilo.

Lakini ukweli kwamba unaweza kuwaza "pembetatu yenye pembe nne" haufanyi pembe tatu yenye pembe nne iwepo kwenye uhalisia.
 
Hivi brother Kiranga unashida gani na Mungu mbona unamuandama hivi kakunyima nini labda? Maana mara nyingi nakukuta kwenye nyuzi hizi kulikoni na huyu Sir God?
 
Hivi brother Kiranga unashida gani na Mungu mbona unamuandama hivi kakunyima nini labda? Maana mara nyingi nakukuta kwenye nyuzi hizi kulikoni na huyu Sir God?

Kama ningekuwa mtu wa kuamini Mungu, ningeweza kusema kanijaalia vingi sana, labda kaninyima uwezo wa kwendambele na nyuma katika muda tu.

Lakini siamini. Na kutoamini hakuji kwa sababu naona nimenyimwa hiki au kile. Fikra hizo ni za ubinafsi, na mimisitaki ubinafsi.

Hizi nyuzi zingine hata nikiwa nimelala, nikiamka asubuhi nakuta watu wame ni tag wanataka nichangie.

Huwa napata mialiko maalum, kwa hiyo ni watu wanapenda maneno yangu yanayowafungua macho.

Shida yangu kubwa na dhana ya kuwepo Mungu, ni kwamba dhana hiyo ni ya uongo, na mimi sipendi uongo.

Dhana hiyo ni ya uongo, kwa sababu ina contradictions kwa namna ambayo haiwezi kuwa kweli.

Ina contradictions kwa namna ambayo dhana hiyo haiwezi kuwa kweli kwa sababu, Mungu - mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote, na upendo wote - haiyumkiniki aumbe ulimwengu ambao unawezekana kuwa na mabaya kama huu.

Kuumba hivyo, wakati ana uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani, ingekuwa ni roho mbaya.

Na Mungu huyo mwenye upendo wote, kinadharia si tu hana roho mbaya. Hawezikuwa na roho mbaya. Akiwa na roho mbaya atakuwa si Mungu wa upendo wote. Mungu wa upendowote hawezi kuwa na roho mbaya.

Hivyo, ama ulimwengu wenye mabaya unawezekana kuwepo kama Mungu huyo hayupo, ama Mungu huyo yupo na ulimwengu wenye mabaya hauwezi kuwepo.

Tunaona kwamba ulimwengu wenye kuruhusu mabaya upo, ndio huu tunaoishi.

Hilo linaonesha ukweli kwamba Mungu huyo hayupo.

Kama unabisha, unaruhusiwa kubishana nami kwa kuthibitisha Mungu huyo yupo.
 
Safi sana umeanza vizuri tu ila mwisho umekuja kuharibu kwa kutaka tubishane mimi lengo langu kuelimishwa tu mkuu wangu Kiranga.
Naomba tu kujua kwa imani yako wewe unaamini vipi juu ya uumbaji huu wa ulimwengu na vilivyomo vimekujaje kwa bahati mbaya au kuna nguvu flani(Mungu) ilihusika kuumba?
 

Unaponisoma ni vizuri kuzingatia kwamba kila neno ninalotumia lina uzito wake, limewekwa katika mizani kabla ya kuandikwa.

Mwisho hapo nimeandika "Kama unabisha".

Sijakutaka tubishane.

Nimejiwekea nafasi kwamba, mimi naweza kuwa nimekosea, na wewe ukawa na elimu kubwa zaidi yangu, ukawa na hoja za kunibishia, ningependa kuzisikia pia.

Nimekataa kujiwekea ukubwa wa mawazo kiasi kwamba, nitakachosema mimi ndiyo mwisho wa mjadala, na wewe huna cha kunibishia.

Sijakutaka ubishane, nimekueleza kwamba, kama una hoja za kubishana, nazikaribisha.

Kuhusu imani, sitaki kuamini, nataka kujua.
 
Hapo ndipo unapokosea unatanguliza sana ushindani badala ya kutoa elimu. Mimi shida yangu kufahamu juu ya kile unachokijua wewe juu ya ulimwengu huu na vilivyomo na sio kupingana wewe unajua kipi juu ya mwanzo wa ulimwengu na mwanadamu kwa ujumla nataka kufahamishwa mkuu.
 
kama Mungu ni wazo inamaanisha na hiki unachojibu ni wazo lako.
ndio mwisho wako wa kufikir.
 
kama Mungu ni wazo inamaanisha na hiki unachojibu ni wazo lako.
ndio mwisho wako wa kufikir.
Umeishia kuona "wazo".

Kwa sababu hapo ndipo mwisho wa uwezo wako wa kufikiri.

Hujaweza kuelewa zaidi ya hapo.
 
Umesema Mungu ni wazo na halina uhalisia lina contradictions,ila hausema wazo hilo ni wazo la nini au kuhusu nini?
 
Maria alipata ujauzito kwa nguvu za Mungu say Yesu ambaye mtoto alikuwa ni yeye mwenyewe,sasa je Yesu binadamu ni mtoto wake mwenyewe au ni clone 🤔
 
Kuna contradiction nyingi halafu mzungukobukifika sehemu flan hujui ulipo tokaa uliize wapi lakin nakupongeza sio kazi ndogo pamoja na contradiction uko poa sana
 
Mnajua ya kwamba inasemekana jina la yesu halikuwa hivo kuna spelling zimetoka na Zingine kuongezwa
umenisisimua mahali
ndiyo maana nikawa nashangaa Y? ukitaja jina la YESU mapepo na mambo mabovu yanakimbia/kuweweseka?
lakini nikawa najiuliza Y? ukitaja jina la Mtume (Saw) yaani hata mapepo haya ropoki
asee hapo NIMEPATA kitu
 
Nimeamua kuandika makala hii kwa heshima ya Jukwaa hili lakini pia kwa ajili ya kuchochea udadisi lengo likiwa k
Umejitahidi Kuandika kwa kirefu sana Nikupe Hongera na hapo hapo kwenye hayo maelezo yako ya kirefu yoote upo wrong kwa asilimia zoote 100!
Uko wrong kivipi?

1.Umemjadili Mungu kwa namna alivyo kwa kutumia Utashi wako,Elimu yako na uelewa wako na Sio narudia tena Sio Maneno yake mwenyewe Mungu katika maandiko matakatifu yaani Biblia .Ukitaka kumuelewa Mungu usitumie vijitabu vingine kando kando ya maandiko yake mwenyewe aliyoyaandika kupitia mitume na manabii wake kajielezea vizuri sana humo kama ukisoma nje ya hapo utapata makinikia tu na sio Ukweli halisi wa MUNGU ndiomaana hujaweka hata kifungu kimoja cha maandiko matakatifu kusimamisha hoja yako! umejiandikia tu uonavyo wewe kutoka kichwani mwako mtu wa watu!

2.Hoja yako yoote imekaa kwenye kitu kinaitwa UTATU (TRINITY)yaani Mungu BABA,Mwana na Roho mtakatifu.kwamba Mungu kagawanyika katika hizo sehemu tatu kiutendaji halafu bado ni mmoja!!! Hakuna mahali popote pale kwenye maandiko matakatifu kuna hicho kitu kimeandikwa sijui mwenzetu umetoa wapi!??? yaani nimejaribu kutafuta sijaona na mzizi wa hoja zako zoote umeanzia hapo na uko wrong from the beginning kitu ambacho kinafanya hoja yako yooote iporomoke na isiwe na Mashiko unless uwe umeamua kumjadili Mungu kwa kutumia vitabu vya kihistoria pamoja na akili zako mwenyewe!!
Next time ukitaka kumjadili Mungu mdadavue kwenye maneno yake mwenyewe kuliko ukaja na hoja hapa ya kupotosha watu au njoo na hoja ya kuuliza maswali hapa uwe kama unataka kujua then utapata sana Mafundisho kuliko kuja na hoja ambayo bni ya kupotosha na kudanganya watu either kwa kujua au kuto kujua kumbuka utatolea hesabu kila ulilolinena hapa duniani
 
Sasa ww ndo wale wale unadhani vitabu vya din ni viwili tu au kimoja yan quarn na bible. Kwenye iyo bible yako ina maana vile vitabu vilivyotolewa kwenye bible eg enoch havikuandikwa na mungu. Then hujui kama bible ina mkangaiko mkubwa
 
Sasa ww ndo wale wale unadhani vitabu vya din ni viwili tu au kimoja yan quarn na bible. Kwenye iyo bible yako ina maana vile vitabu vilivyotolewa kwenye bible eg enoch havikuandikwa na mungu. Then hujui kama bible ina mkangaiko mkubwa
1.Kwakuwa mimi ni mkristo kitabu ni kimoja tu cha dini ninachokiamini ambacho ni biblia na biblia ninayoisoma mimi ina vitabu 72 maana yake vitabu 6 zaidi ya ile biblia ya vitabu 66 ,kwahiyo hivyo vitabu unavyodhani mimi sivisomi navisoma pia kama sehemu ya biblia yangu na ninaamini viliandikwa na Wanadamu kwa msaada wa Mungu mwenyewe,

2.Sijui kama biblia inamkanganyiko ungeuweka hapa hadharani labda tungeanzia hapo ila ukisema tu maneno matupu bila kuuonyesha huo mkanganyiko unakuwa haueleweki weka hoja zako hapa kwa maandiko unayodhani ni mkanganyiko,ila ninachojua mimi Mungu mwenyewe kasema yeye sio mwandishi wakuleta mkanganyiko (1 Corinthians 14:33) na pia maandiko ya kwenye biblia huwezi yajua kwa akili yako ya kibinadamu mpaka kuwepo na msaada wa Roho mtakatifu au ufundishwe na mtu mwenye roho mtakatifu otherwise utaona ni mkanganyiko! ila Mungu kashasema yeye sio muandishi wa kuleta mkanganyiko!
 
E 1:3-5 On the first day, God created light, then separated light and darkness.
GE 1:14-19 The sun (which separates night and day) wasn't created until the fourth day.

GE 1:11-12, 26-27 Trees were created before man was created.
GE 2:4-9 Man was created before trees were created.

GE 1:20-21, 26-27 Birds were created before man was created.
GE 2:7, 19 Man was created before birds were created.

GE 1:24-27 Animals were created before man was created.
GE 2:7, 19 Man was created before animals were created.

GE 1:26 Man is to have dominion over fish, birds, cattle, and all wild animals, yet--
GE 2:15-17 It is wrong to be able to tell good from evil, right from wrong.

GE 1:26-27 Man and woman were created at the same time.
GE 2:7, 21-22 Man was created first, woman sometime

Baahadhi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…