Hapo ndio tatizo lilipo mkuu kiranga, si kila jambo unasikiliza kwa ufahamu Wa kwenye ubongo.
Wewe usiyetumia ufahamu wa kwenye ubongo unatumia nini kufahamu vitu bila kuhusisha ubongo?
Yapo mambo mengi hautapata jawabu la kisayansi lakini moyoni unajua hili ndio jibu.
Jawabu lakisayansi ni lipi? Unajua Einstein's theory of Relativivy imekuwa confirmed experimentally toka 1919 na mpaka leowatu wanaihoji bado kuangalia kamaina mapungufu?
Labda nikuulize swali, unaamini kuwa mtu ana roho?
Sitakikuamini, natakakujua. Roho ni nini na unajuaje ipi si hadithi tu?
Kuna kitu chochote kinachotoka na kuondoka inapotokea mtu amefariki?
The second law of thermodynamics applies, in closed systems, with time, entropy move from low to high. High entropy eventually kill all systems.
Huhitaji roho hapo.
Nini hasa kinasababisha mtu afe?
The entropy of a biological system and its surroundings.
Unaelewakifokinaonesha Mungu hayupo, hakioneshiMungu yupo?
Mungu mwenye uwezowote, ujuzi wote na upendowote, angekuwepo, ulimwengu usingekuwa na kifo.
Kifokinatenganisha wapendanao, Mungu asingependa kuona viumbe wake wapendanao wanatenganishwa na kifo.
Mungu mwenye upendo wote angezuia kifo kisitenganishe wapendanao.
Tunaona kifo kipo. Kinatenganisha wapendanao.
Hivyo, Mungu huyo hayupo.
Bado sijaenda nje ya mada maana natamani ndugu uanze kuyatazama maisha kutoka ndani ya moyo wako. Yatosha sasa kwako kutumia tu ubongo ulio very limited.
Ndani ya moyowangu kuna damu na makutano ya mishipa, niyatazame maisha ndani ya moyowangu kivipi?
Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
Unaweza kuthibitisha roho ipo?
Unaweza kuthibitisha pepo ipo?