Cc
Kiranga cha Ndenga Sakala Kandumbwa
Nimemjibu chini hapo.
Hata hajui msingi mbovu wa swali lake, sio tu nimemjibu swali, nimemuonesha pia kwamba swali limejengwa katika msingi mbovu.
Kuelewana na watu wengine kazi sana hapa.
Mimi nasema hivi.
Ikiwa ili mji A uwe mji mkuu wa nchi B, inabidi mji A uwe ndani ya nchi B.
Nairobi haipo Tanzania, ipo Kenya.
Hivyo Nairobi haiwezi kuwa mji mkuu wa Tanzania.
Mtu ananiuliza, kwani unaweza kuushika upepo ukatuonesha huu upepo?
Kwani mimi nimesema chochote kuhusu kuishika Nairobi nikakuonesha hii Nairobi?
Objection yangu kuhusu uwepo wa Mungu ni ya kifalsafa, ni ya kuhusiana na contradiction ya "the problem of evil".
Haina uhusiano wowote na Mungu kuonekana au kutoonekana, after all, unaweza kuona kitu ambacho hakipo. Kwa hiyo hata kuonekana kitu si uthibitisho kwamba kipo.
Ukienda jangwani unaweza kuona maji kwa mbali, ukikaribia unakuta hamna maji, ni mwanga tu unaonesha kama maji kwenye joto la jangwani, unatoa mirage. Mauzauza ya maji kuonekana sehemu ambayo hakuna maji.
Lakini huyu anayetaka habari ambazo mimi sijazisema anasumbuliwa na elimu ndogo.
Hajui mirage ni nini.
Hajui kitu kinaweza kuonekana kipo, lakini kisiwepo.
Hajui kitu kinaweza kuwa hakionekani, lakini kikawepo.
Hajui nakataa uwepo wa Mungu kwa sababu kubwa kuliko sababu ya kuonekana na kutoonekana.
Aana utapiamlo wa ubongo, hajui kusoma kwa ufahamu.
Kubishana na watu wenye ukosefu wa elimu ya msingi ni kazi kubwa sana.
Mimi nitapinga uwepo wa Mungu kwa sababu ya contradiction ya "the problem of evil", kitu ambacho naona hajawahi kukisikia, yeye atafikiri na ku conclude bila hata kuuliza, atachukulia kwamba mimi napinga uwepo wa Mungu kwa sababu haonekani.
Uharisho mtupu.