Biblia ni Kitabu cha Vitabu (The Book of Books). Sababu hizi hapa:

Biblia ni Kitabu cha Vitabu (The Book of Books). Sababu hizi hapa:

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
1. Imesambazwa kwa wingi kushinda vitabu vyote duniani.

Zaidi ya nakala bilioni 5 za Biblia zimechapishwa na kusambazwa ulimwenguni kote. Rekodi hii haijafikiwa na kitabu chochote kingine.

2. Imetafsiriwa zaidi ya kitabu chochote duniani.

Biblia nzima imeishatafsiriwa katika lugha zaidi ya 740
Agano Jipya pekee: lugha zaidi ya 1,600
Sehemu za Biblia (kama Injili au Zaburi): lugha zaidi ya 3,600

Hakuna kitabu kingine duniani kilichofikia kiwango hiki cha tafsiri.

3. Biblia inatoa tumaini la milele kwa kila mtu.
Watu wa kila kabila, kila taifa, na kila kizazi wanaweza kupata tumaini la kweli kupitia ujumbe wake wa wokovu.

4. Inabadilisha maisha ya watu kwa nguvu ya ajabu.
Kwa kusoma Biblia, wameokoka watu waliokuwa wanywaji wa pombe, wachawi, waasi, na wauaji kwa sababu Roho wa Mungu anatenda kazi ndani yake. Kitabu chenye maneno ya kutungwa na watu hakiwezi kuleta mabadiliko hayo makubwa ya maisha.

5. Biblia ina umoja wa ajabu wa ujumbe.
Imeandikwa na watu zaidi ya 40 katika kipindi cha takriban miaka 1,500, lakini haina mgongano wa ujumbe. Ujumbe wake unatuelekeza kwa Mungu mmoja na wokovu mmoja unaopatikana kwa njia ya Yesu Kristo pekee.

6. Biblia imetabiri matukio mengi yaliyotimia kihistoria.
Unabii kuhusu kuzaliwa kwa Yesu Kristo, kuanguka kwa mataifa kama Babeli na Tiro, na kurudi kwa taifa la Israeli ni nabii zilizotimia kwa usahihi wa ajabu.

7. Inatoa mwongozo wa maadili wa juu zaidi duniani.
Haina upendeleo wa kijinsia, kijamii, au kikabila. Inafundisha upendo, haki, unyenyekevu, msamaha, na uadilifu wa kweli.

8. Ina uwezo wa kuwapa watu hekima ya kweli.
Biblia huwafungua watu macho ya rohoni, huwapa busara ya kushinda vishawishi, na kuwajengea maisha ya utulivu wa ndani na maamuzi yenye msingi.

9. Inafunua vita ya kiroho kati ya nuru na giza.
Biblia haitufichi adui yetu, shetani. Inatufunulia hila zake na kutufundisha jinsi ya kumshinda kwa imani katika Kristo.

10. Biblia ina historia ya mwanadamu isiyo na upotoshaji.
Inaeleza kwa ufasaha asili ya dunia, dhambi, wokovu, na mwisho wa ulimwengu, na habari zote zimeungana vizuri sawasawa na mpango wa Mungu.

11. Biblia ni Kitabu chenye ufunuo wa mapenzi ya Mungu aliye hai kwa wanadamu. (2 Timotheo 3:16).

12. Inaendelea kuwa hai na kusikika kwa wote wanaoisoma kwa imani.
Tofauti na maandiko ya kale ambayo hufa na kusahaulika, Biblia ni hai kila wakati (Waebrania 4:12), na sauti yake huendelea kugusa roho za wanadamu kizazi baada ya kizazi.

Ukipenda unaweza kuiita Biblia the King of Books. Kwa sababu ndani yake kuna habari za Mfalme wa Wafalme - YESU KRISTO
 
Biblia inapingwa vikali na shetani kwa sababu ni taa ya kuonyesha njia ya wokovu. Shetani anaichukia sana. Anafanya kila juhudi kuhakikisha watu hawaisomi, ili wabaki gizani. Anatumia mbinu nyingi kuwafanya watu waidharau na kuona kama ni kitabu cha hekaya tu kisicho na maana.

Na wengine wanaichanganya na mafundisho ya watu. Wanakwepa kuisoma, kwa kisingizio cha muda au uchovu. Mapepo nayo hayaachi kuwaletea usingizi watu wanaojaribu kuisoma.

Usikubali kudanganywa! Biblia ndiyo njia ya kufahamu kweli ya Mungu, kujua hatima yako, na kuushinda uongo wa shetani. Anza kuisoma leo kwa moyo mnyoofu, utashangaa jinsi maisha yako yatakavyobadilika.
 
Ni hakika mkuu.
 
Kama ulipitwa na uzi huu
 
Hakika
Biblia ni Neno La Mungu Mwumba Mbingu na Nchi na vyote viujazavyo:
 
Halafu ukiweka tu mada kuhusu Biblia muzlims wa kwanza kubisha:
Mbona wa dini nyingine wanatulia tu:
Wewe weka andiko lolote la kwenye Biblia waislamu watalipinga:
Au tuwaite wapinga Biblia ?
 
Back
Top Bottom