Oya Tusepe
JF-Expert Member
- Aug 3, 2016
- 265
- 870
Matt 7:22-23
"Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako? na kwa jina lako kutoa pepo?, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?. Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu."
Andiko tajwa hapo juu ni zito sana, na litawapeleka wakristo wengi kwenye maangamizi mabaya sana. sio jambo jepesi na kwa mtazamo wangu naona kama linahitaji ufunuo mzito.
BWANA ANASEMA watakuja kwake (baadhi ya wakristo) na kumwambia kwamba walilitumia jina lake na wakatenda miujiza mingi,
Msingi wa kwanza hapa ni kwamba watu hawa walidhani mioyoni mwao kwamba walikuwa wanamtegemea Mungu na YESU na si vinginevyo,
Watakuwa wanajiamini kwamba wapo sahihi na watamuendea YESU kifua mbele lakini YESU atawakataa na atasema hakuwahi kuwafahamu kamwe katika kipindi chote.
SWALI
Hawa mabwana wanatenda miujiza kwa nguvu za nani ikiwa ni kweli walidhani wanamtegemea Yesu kumbe sivyo na pia kwa shetani hawapo maana mpaka wanapata Jeuri ya kumuendea YESU ni kwamba wanaamini pasi na shaka mioyoni mwao kwamba YESU atawapokea lakini sasa anawakana.
Je miujiza hii watu wanafanya kwa nguvu za nani? Je mwanadamu ana Nguvu za kutenda miujiza bila kumtegemea Mungu au Ibilis?
Hapa kuna kitu cha kujifunza.