Biden kushinda tena uchaguzi wa Marekani

Biden kushinda tena uchaguzi wa Marekani

ward41

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2022
Posts
749
Reaction score
2,533
November Biden na Trump wanaingia tena kwenye Uchaguzi wa Uraisi kama Wagombea kwenye vyama vyao.

Uchaguzi wa 2020, Biden alimshinda Trump kwa kura nyingi tu. Trump alikuwa raisi wa muhula mmoja

Safari hii wanakutana tena na Biden bado anaonekana kumshinda Trump. Takwimu zinaonesha hivyo

Raisi Biden amefanya vizuri sana kwenye Uchumi. Vilevile Biden kafanya vizuri kuhandle Vita ya Ukraine.

Wachumbuzi mbalimbali wa masuala ya siasa za Marekani wanasema Biden anashinda tena uchaguzi wa mwaka huu
 
Biden kweli atashinda kwasababu uchumi unaimarika na anacreate kazi nyingi kila mwezi. Sasa hivi Republicans wamekomaa na Immigration na afya ya Biden ndo turufu yao.

Ila natamani sana Trump ashinde lakini ndo hivyo tena. Trump ndo rais sahihi
 
Achana na kushinda, hata chama chake wakimsimamisha ntashangaa sana, Wamarekani hawawezi kumpa tena washamuona he is a joke, mtu Kila siku kuanguka, mtu anapoteza memory mpaka Kuna muda anasahau yupo wapi, umpe nchi tena, sema marekani inaongozwa na taasisi ingekua huku kwetu rais ana power kama Mungu sijui Hali ingekuaje

Ila huwezi kujua, Dunia sasa hivi inaongozwa na utawala wa shetani, utawala wa Biden umemwaga sana damu huenda wakawa bado wanapendezwa nae
 
Achana na kushinda, hata chama chake wakimsimamisha ntashangaa Sana, wamarekani hawawezi kumpa tena washamuona he is a joke, mtu Kila siku kuanguka, mtu anapoteza ...
Uko dunia gani. Biden tayari ni Mgombea. Unamchukulia poa wakati amefanya Mambo makubwa. Tatizo watu wameshika LA uzee bila kuangalia kazi alizofanya
 
Jihadists hawana kabisa cha kuongea kwenye mada kama hizi ambazo sio za ubaguzi wa kidini na wala ambazo hazina mihemko na zinazohitaji busara katika uchangiaji
 
Achana na kushinda, hata chama chake wakimsimamisha ntashangaa sana, Wamarekani hawawezi kumpa tena washamuona he is a joke, mtu Kila siku kuanguka, mtu anapoteza memory mpaka Kuna muda anasahau yupo wapi, umpe nchi tena, sema marekani inaongozwa na taasisi ingekua huku kwetu rais ana power kama Mungu sijui Hali ingekuaje

Ila huwezi kujua, Dunia sasa hivi inaongozwa na utawala wa shetani, utawala wa Biden umemwaga sana damu huenda wakawa bado wanapendezwa nae
Kwa Comment hii ni wazi umeathiriwa na mijadala ya vijiwe vya kahawa! Unazungumzia kushangaa kama chama chake kitamsimamisha ukimaanisha mchakato wa kupitisha wagombea bado haujaanza!? Mtu kuanguka ni ajabu kwako? Hujawahi kuanguka? Hao ambao bado wanamtaka (mashetani) ni stori za kahawani tu na hapo ndipo nilipokudharau zaidi.
 
Eti takwimu zinambeba Biden😁Biden atakuwa defeated kwenye swing states kama Georgia, Wiconsin, Nevada na Michigan,,hapo Uraisi Kwa heri
 
Biden kweli atashinda kwasababu uchumi unaimarika na anacreate kazi nyingi kila mwezi. Sasa hivi Republicans wamekomaa na Immigration na afya ya Biden ndo turufu yao.

Ila natamani sana Trump ashinde lakini ndo hivyo tena. Trump ndo rais sahihi

Mitandaoni, kama kawaida, bwana Donald Trump anatawala sana, na ndiye nyota.

Kiutendaji, Trump hana tofauti na Magufuli (tofauti yao ni rangi tu) ila wanafanana kila kitu, hususan "Ego". Tuliona jinsi Trump alileta mtifuano mkubwa sana kwenye awamu yake japo "majuha" wake wanamuona mtu wa maana kama ilivyo huku kwetu "majuha" wa hayati Magufuli.

Baba wa Demokrasia, yaani Marekani, kama Trump atashinda na kuwa Rais wa USA basi jua hata hapa Tanzania "Magufuli like" atashika madaraka tena.

Serikali ya Marekani inafanya kila njia ili Trump asiingie ikulu. Tatizo sio chama, tatizo ni "Trump". Wanamuita "Trash Talker".
 
Back
Top Bottom