Bidhaa 10 ambazo huruhusiwi kuziingiza Tanzania

Bidhaa 10 ambazo huruhusiwi kuziingiza Tanzania

. SANAMU ZA NGONO (SEX TOYS)
Kama ilivyo katika nchi nyingi za Afrika, Tanzania pia inakataza kuingiza sanamu za kufanyia ngono kama vile uume bandia (dildos, vibrators), vinyamkera mahaba n.k

PONOGRAFIA
Bidhaa kama vile majarida, vitabu, mikanda ya video/audio au maudhui ya ngono yaliyo katika mfumo wowote, haviruhusiwi kuingizwa Tanzania aidha kwa biashara au matumizi binafsi


Unazungumzia Tanzania hii hii🤔🤔⁉️‼️
 
Hiyo Taser km ikija kuruhusiwa kuingia nchini,Mimi nitakuwa wa Kwanza kumiliki ili nikomae na watoto wa keko maeneo ya bandari

Jamaa wanakaba sn mitaa ya bandari pale kuanzia saa moja usiku alafu Mzee samtaimz napiga night shift..dawa Yao ni kuwapiga shoti Tu Hadi mtu ana freeze

Siku moja walivamia gari la dada mmoja wwkakomba kila kitu walichokikuta ndani,dada wa watu akapiga sn kelele lkn hakuna aliyethubutu kunyanyua mguu wake kwenda kumsaidia me mwenyewe sikuthubutu,Walikuwa na mapanga ya kutosha ,makondakta na madereva daladala wanaangalia tu dah!
Agiza pepper spray nadhani ni legal,, walinitiaga viwembe maeneo ya keko machungwa pale nikaipataga,, nasubiria siku waje tena
 
Hiyo Taser km ikija kuruhusiwa kuingia nchini,Mimi nitakuwa wa Kwanza kumiliki ili nikomae na watoto wa keko maeneo ya bandari

Jamaa wanakaba sn mitaa ya bandari pale kuanzia saa moja usiku alafu Mzee samtaimz napiga night shift..dawa Yao ni kuwapiga shoti Tu Hadi mtu ana freeze

Siku moja walivamia gari la dada mmoja wwkakomba kila kitu walichokikuta ndani,dada wa watu akapiga sn kelele lkn hakuna aliyethubutu kunyanyua mguu wake kwenda kumsaidia me mwenyewe sikuthubutu,Walikuwa na mapanga ya kutosha ,makondakta na madereva daladala wanaangalia tu dah!
Stun gun zinazuruhusiwa,wanachotska Tanganyika Arms ni Barua ya dhamana pamoja na picha nne,kazi inakua imeisha.
 
Habari WanaJF,

Kuna orodha ndefu ya bidhaa ambazo ni marufuku kusafirishwa kuja Tanzania kwa mujibu wa sheria za nchi na sheria za kimataifa.

Hivyo, tunashauri kabla hujaagiza bidhaa yoyote ni vyema ukafahamu sheria hizo vizuri kuepuka usumbufu, hasara na matatizo na mamlaka.

1. SANAMU ZA NGONO (SEX TOYS)
Kama ilivyo katika nchi nyingi za Afrika, Tanzania pia inakataza kuingiza sanamu za kufanyia ngono kama vile uume bandia (dildos, vibrators), vinyamkera mahaba n.k.

Bidhaa hizi zimekatazwa kwa sababu za kimaadili na kitamaduni.

2. DAWA ZA KULEVYA
Tanzania hairuhusu uingizaji na usafirishaji wa aina yoyote ya Dawa za Kulevya na madawa yote yaliyopigwa marufuku kwa mujibu wa sheria za kimataifa na sheria za Tanzania mfano heroini, kokeini, bangi n.k.

3. PONOGRAFIA
Bidhaa kama vile majarida, vitabu, mikanda ya video/audio au maudhui ya ngono yaliyo katika mfumo wowote, haviruhusiwi kuingizwa Tanzania aidha kwa biashara au matumizi binafsi.

4. VITU BANDIA
Bidhaa feki na zile za magendo hutakiwi kuziagiza kuja Tanzania. Zitazuiliwa kwenye ukaguzi au zitateketezwa kwa mujibu wa sheria na taratibu bila fidia yoyote.

5. MATAIRI CHAKAVU
Kuagiza na kuingiza matairi ya magari binafsi au ya abiria ambayo yameshatumika ni marufuku kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Matairi yasiyotoka moja kwa moja kiwandani hayatakiwi. Ni jitihada za kupunguza ajali za barabarani nchini.

6. SILAHA ZA MOTO
Sheria na taratibu haziruhusu kuingiza silaha za moto kiholela nchini Tanzania. Silaha hizi ni pamoja na bunduki, risasi na mabomu.

7. MIFUKO YA PLASTIKI
Tanzania ilitangaza marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki kote nchini kuanzia Juni 1, 2019.

Watalii na wafanyabiashara; epukeni kuleta mifuko ya plastiki nchini. Haina kazi tena!

8. SUMU
Ni marufuku kuagiza na kuingiza sumu ya aina yoyote. Sumu za kemikali, vimiminika na unga unga zinazoweza kuhatarisha afya za watu na mazingira. Sumu na dawa zisizo na maelezo ya kueleweka hazitaruhusiwa kuingia nchini.

9. VILIPUZI
Bidhaa zinazoweza kulipuka wakati wa usafirishaji haziruhusiwi kuingizwa nchini kiholela. Hata sheria na taratibu za kimataifa (IATA) zimezuia usafirishaji wa bidhaa hizo hasa kwa usafiri wa Anga.

10. VIPODOZI
Bidhaa zote za vipodozi vyenye kemikali ya mercury kwa kiwango kikubwa haviruhusiwi kuingizwa Tanzania.

Inashauriwa kwa wajasiriamali na wafanyabiashara (hata watu binafsi) kusoma vizuri ingredients za vipodozi kabla hawajaagiza kuleta nchini.

NB: Baadhi ya bidhaa tulizozitaja na nyingine kama vile wanyama hai, mimea, madini na fedha hazijapigwa marufuku; bali zitahitaji vibali maalum kutoka kwa mamlaka. Kuagiza na kuingiza bidhaa hizo nchini bila vibali ni haramu na zitazuiliwa wakati wa ukaguzi.
Wanakataza lakini ndio zimejaa kama hawajakataza
 
Back
Top Bottom