Bidhaa toka Tanzania na Uganda zapandishiwa Tozo nchini Kenya

Bidhaa toka Tanzania na Uganda zapandishiwa Tozo nchini Kenya

Mpinzire

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2013
Posts
7,503
Reaction score
13,463
Bidhaa zinazoingia nchini Kenya kutoka nchini Tanzania na Uganda hasa Vitunguu Maji na Mayai vimeongezewa tozo katika bajeti iliyoanza kutekelezwa jana July 1 2021.

Licha ya makubalino ya Rais Samia na Rais Kenyata miezi michache iliyopita walikubaliana kuondoa vikwazo vya kila aina katika biashara za nchi hizi mbili.

Kenya wanarufundisha nini?
Screenshot_20210702-193834.jpg
 
Ni kama nchi za ulaya kuwekewa vikwazo na marekani kwa sababu ya nguvu za kiuchumi, na Kenya inapita mulemule, 😂😂😂

Watanzania kazi yetu ni kulialia
 
Akiweka ugoko wewe weka jiwe, mnyonge atalia a akimaliza atatafuta namna ya kusolve
Kikwete aliweza very smoothly 😃😃
 
Ukiona Adui analishangilia ni jiulize wapi umekosea lakini ukiona kanuna basi umempiga sio maneno yangu ya mzee hayo
Mam akae chin ajiulize
Na bado maana Kenya ndio nchi pekee barani Afrika ambayo kila mwenye inda na nchi huitumia kushinikiza nchi nyingine kukubaliana na matakwa yake.
 
Katika jumuiya ya Afrika Mashariki hakuna nchi ambazo raia wake huwa wanatuona watz maboya kama Kenya na Rwanda. Hawa kiboko yao ilikuwa Magufuli tu, huyu mama hawawezi kabisa, Wakenya ndio pumbavu kabisa.Mkumbuke kuwa kwa ushenzi huu huu Mwalimu Nyerere zilikuwa haziivi na Jommo Kenyatta.
 
Wakati sisi tukiwauzia Gesi yetu badala ya kuhakikisha kwamba wananchi wanaipata hiyo nishati Kwa bei nafuu.
Hiyo gesi bado sana mkuu, si Kenyatta wala Samia ataiona ikitiririka kuelekea huko.

Hiyo wanaiita ni 'MOU', hatua za mwanzo kabisa.

Lakini kama watalazimisha iharakishwe, ili hiyo gesi iwazalishie umeme wa bei nafuu Kenya ili watengeneze bidhaa nafuu za kutuuzia sisi, huku tukipeleka mali ghafi zetu kwao watengeneze vitu vyenye thamani kubwa, basi ubwege wetu utaendelea kujionyesha ulivyo.

Sasa hivi tunawauzia pamba (ghafi) watengeneze nguo . Kenya wamelishika vizuri sana soko la Marekani chini ya mpango wa AGOA, kuuza nguo huko, sisi maneno mareeeefu sana, hakuna chochote tunachouza huko Marekani ambacho ni cha maana. sana.

Tunawauzia mbao, wanatengeneza Samani, wanakuja kuuza hapa.

Mama anafurahi saaana hadi atapiga muruzi na kuimba "Nafungua Nchi", huku wenzake wakichekelea!

Inaudhi na kuumiza roho sana.
 
Back
Top Bottom