Hiyo gesi bado sana mkuu, si Kenyatta wala Samia ataiona ikitiririka kuelekea huko.
Hiyo wanaiita ni 'MOU', hatua za mwanzo kabisa.
Lakini kama watalazimisha iharakishwe, ili hiyo gesi iwazalishie umeme wa bei nafuu Kenya ili watengeneze bidhaa nafuu za kutuuzia sisi, huku tukipeleka mali ghafi zetu kwao watengeneze vitu vyenye thamani kubwa, basi ubwege wetu utaendelea kujionyesha ulivyo.
Sasa hivi tunawauzia pamba (ghafi) watengeneze nguo . Kenya wamelishika vizuri sana soko la Marekani chini ya mpango wa AGOA, kuuza nguo huko, sisi maneno mareeeefu sana, hakuna chochote tunachouza huko Marekani ambacho ni cha maana. sana.
Tunawauzia mbao, wanatengeneza Samani, wanakuja kuuza hapa.
Mama anafurahi saaana hadi atapiga muruzi na kuimba "Nafungua Nchi", huku wenzake wakichekelea!
Inaudhi na kuumiza roho sana.