Bidhaa zilizo expire zipo Mtaani, imenitokea hii nikiwa Salasala Kwa Mtenga, Dar, najiuliza hata wakibaini wanazipeleka wapi?

Bidhaa zilizo expire zipo Mtaani, imenitokea hii nikiwa Salasala Kwa Mtenga, Dar, najiuliza hata wakibaini wanazipeleka wapi?

Mliogwa

Member
Joined
Jun 6, 2024
Posts
37
Reaction score
37
Mamlaka zinazohusika na ubora wa bidhaa nadhani mnajisahau sana, mitaani kuna bidhaa nyingi ambazo kama hazija-expire, basi hazina expire date kabisa au expire date yake haionekani vizuri.

Hii ni hatari sana jamani, ni vile baadhi ya Watanzania tuna shida ya kutosoma ukomo wa bidhaa kwenye vifungashio vyake, hatari ya kupata madhara yanayotokana na hii tabia itatukumba wengi mbeleni.

Sina hakika na mamlaka inayohusika na udhibiti wa bidhaa za namna hii lakini nafikiri ni muhimu sana wahusika kusimamia na kuchukua hatua kali.

Jambo hili likanifanya nijiulize hizi bidhaa zinazoisha muda wake huwa zinapelekwa wapi? Kuna utaratibu gani wa vendors kurudisha au kuacha kuuza kabisa?
IMG-20250106-WA0018.jpg

IMG-20250106-WA0020.jpg

IMG-20250106-WA0019.jpg
 
Back
Top Bottom