sky walker
JF-Expert Member
- Feb 3, 2018
- 1,160
- 831
Moto wa maneno makali kati ya 50 Cent na Floyd Mayweather Jr umeendelea kuwashwa na wawili hao kwa mara nyingine tena kwa kudhalilishana kifedha.
50 Cent na Mayweather Jr
Floyd Mayweather ndiye aliyekuwa wa kwanza kumtupia maneno makali kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo aliufananisha utajiri wa 50 Cent na gharama ya saa yake aina ya “The Billionaire Watch” yenye thamani ya dola milioni $18 .
“Hautakiwi kuanzisha bifu na mimi inatakiwa uanzishe kwanza na saa yangu. Mimi na wewe ni level mbili tofauti,“ameandika Mayweather na kuweka picha ya zamani ya 50 Cent enzi hizo akiwa na maisha duni.
Hata hivyo, 50 Cent naye hakuwa nyuma amemjibu mwanamasumbwi huyo kuwa saa hiyo ambayo anaitumia sio yake anawadanya watu kuwa amenunua lakini sio kweli huku akidai kuwa Mayweather kwa sasa pesa zote ameshahonga na muda sio mrefu ataanza kurudi mtaani kupiga vimeo.
“Naomba muikumbuke posti hii nawambia huyo bingwa wa ndondi duniani hawezi kununua saa ya gharama kama hiyo anadhani watu ni wajinga. Kama kuna ukweli atuletee hiyo saa aache kuizungumzia zungumzia tu. Kamali na mademu wamemmaliza kila kitu. Nadhani muda si mrefu atarudi kuwa MC kwenye sherehe za watu huko mitaani.“ameandika 50 Cent.
Wawili hao wameanza kurushiana maneno toka mwezi Juni mwaka huu ambapo 50 Cent alimuita Floyd Mayweather mpumbavu namba moja duniani kwa kununua saa ya mabilioni.
Je, kwa maoni yako unadhani hii ni kiki ya kumrudisha 50 Cent kwenye ramani au ni bifu la ukweli?