Bifu la 50 Cent na Floyd Mayweather Jr lafikia pabaya

Bifu la 50 Cent na Floyd Mayweather Jr lafikia pabaya

sky walker

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2018
Posts
1,160
Reaction score
831
Moto wa maneno makali kati ya 50 Cent na Floyd Mayweather Jr umeendelea kuwashwa na wawili hao kwa mara nyingine tena kwa kudhalilishana kifedha.

image162.jpg

50 Cent na Mayweather Jr
Floyd Mayweather ndiye aliyekuwa wa kwanza kumtupia maneno makali kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo aliufananisha utajiri wa 50 Cent na gharama ya saa yake aina ya “The Billionaire Watch” yenye thamani ya dola milioni $18 .

“Hautakiwi kuanzisha bifu na mimi inatakiwa uanzishe kwanza na saa yangu. Mimi na wewe ni level mbili tofauti,“ameandika Mayweather na kuweka picha ya zamani ya 50 Cent enzi hizo akiwa na maisha duni.

Capture-47.jpg


Hata hivyo, 50 Cent naye hakuwa nyuma amemjibu mwanamasumbwi huyo kuwa saa hiyo ambayo anaitumia sio yake anawadanya watu kuwa amenunua lakini sio kweli huku akidai kuwa Mayweather kwa sasa pesa zote ameshahonga na muda sio mrefu ataanza kurudi mtaani kupiga vimeo.

“Naomba muikumbuke posti hii nawambia huyo bingwa wa ndondi duniani hawezi kununua saa ya gharama kama hiyo anadhani watu ni wajinga. Kama kuna ukweli atuletee hiyo saa aache kuizungumzia zungumzia tu. Kamali na mademu wamemmaliza kila kitu. Nadhani muda si mrefu atarudi kuwa MC kwenye sherehe za watu huko mitaani.“ameandika 50 Cent.

Wawili hao wameanza kurushiana maneno toka mwezi Juni mwaka huu ambapo 50 Cent alimuita Floyd Mayweather mpumbavu namba moja duniani kwa kununua saa ya mabilioni.



Je, kwa maoni yako unadhani hii ni kiki ya kumrudisha 50 Cent kwenye ramani au ni bifu la ukweli?
 
50 cent ndo alianza kumrushia maneno Floyd na sio Floyd ndo alianza ..fatilia Vizuri mkuu. .
 
wanatafuta kiki tu apo ,huenda 50 anataka kutoa nyimbo mpya,hao sio wakugombana kiivyo
 
Hiyo picha 50 cent si alijipunguza sababu ya movie ila acha yamkute yeye ndio alianza kumchokoza floyd mayweather
 
Hao wote wanapenda mipasho, utasikia baada ya mwezi bifu limeisha wameanza urafiki
 
ameandika Mayweather na kuweka picha ya zamani ya 50 Cent enzi hizo akiwa na maisha duni.
Capture-47.jpg

Nikukumbushe tu kwamba hiyo picha ya Fif sio kwamba kakonda kwa sababu ya maisha duni bali alijikondesha kwa sababu ya muvi......kwa sasa fif ni HollyWood Star anacheza muvi za maana tu...tafuta kitu inaitwa 'Power'
 
Wapande ulingoni wazipige, atakayepigwa akae kimiya...

50Cent alipe kodi alizokua anakwepa... Mayweather alipe wafanyakazi wake pesa zao...


Cc: mahondaw
 
Hiƴo ɓiashara mwisho watakutana ulingoni
 
Nliiangalia season one kile kidem kikali cheusi mumewe drug lord alikuwa anamtaka dereva sijui waliishia wapi
Nikukumbushe tu kwamba hiyo picha ya Fif sio kwamba kakonda kwa sababu ya maisha duni bali alijikondesha kwa sababu ya muvi......kwa sasa fif ni HollyWood Star anacheza muvi za maana tu...tafuta kitu inaitwa 'Power'
 
Back
Top Bottom