Bifu la Emelda Mwamanga wa Bang magazine na Reginald Mengi

Bifu la Emelda Mwamanga wa Bang magazine na Reginald Mengi

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Mwanamama mjasiriamali, na managing director wa jarida maarufu nchini , Bang magazine , aitwaye Emelda Mwamanga amefunguka kuhusu bifu lake na mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi, kupitia kwenye moja ya mahojiano ya kwenye kipindi maarufu cha Tv Hapa nchini .

Mbali na kuelezea experience yake kwenye biashara yake, pia alizungumzia changamoto mbali mbali anazokabiliana nazo kwenye biashara zake, moja ya changamoto alizozielezea ni ile ya kushtakiwa na mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi, ambaye ni mume wa aliyekuwa miss Tanzania, Jackline Ntuyabaliwe maarufu kama K-Lyn.

Akielezea chanzo cha kushtakiwa, mwenyewe anadai ni kuvujishwa kwa picha za mfanyabiashara huyo akiwa na familia yake, kitendo ambacho mfanyabiashara huyo hakukipenda hivyo aliamua kumshtaki mwanamama huyo kama adhabu na fundisho.

Akielezea kwa masikitiko mwanamama huyo alielezea jinsi ya picha hizo zilivyosambaa mitandaoni, ambazo zilipigwa mahsusi kwa ajili ya kupambwa kwenye jarida maarufu la mwanamama huyo, hata hivyo inasemekana baadhi ya wahariri wa jarida hilo walizivujisha picha za Mengi huyo kwenye mitandao ya kijamii either kwa bahati mbaya au kwa kukusudia , kitendo kilichomkera Mengi na kuamua kumshtaki.
 
Emelda mwamanga
 
Attachments

  • 1433184840701.jpg
    1433184840701.jpg
    44.7 KB · Views: 1,600
Haya wambea wenzangu akina shakoor jongo na mnaly na mwenzio imelda mtema, mwenzenu yamemkuta uko nyie jishaueni sasa kuweka picha ya muheshimiwa muone, mimi mwenyewe mpaka nimeogopa kuweka picha yake maana maisha nayapenda sana, asiyemjua mengi aka google tu ataona picha yake mi majanga sitaki sasa ivi
 
Hahahahahaha binamu bado unajipenda
 
Kama zilivuja basi alikuwa na kosa, inabidi afanye kazi kwa jinsi anavyoahidi watu.

Nimeshangaa hadi leo hajui zilitokaje kuvuja inaelekea haweki mambo vizuri katika biashara yake haswa kwa wafanyakazi na anaoingia nao kama mkataba wa kufotoa picha.

Atakuwa amejifunza.
 
Naona alitaka kulifanyia promo jarida lake ikam cost
 
Yeah, tell me if you know

or you saying you too curious to know? sikukupata vizuri hii lugha ya malkia

km ndo zile za harusi jamani namuonea huruma...na ajifunze pia huyo emelda na wengine pia wajifunze..
 
Alieshitaki ni mrs mengi that y imelda kalalamika kua mengi alikua na uwezo wa kumzuia bibie asishtaki mwisho wacku ndo kamsapoti
 
Back
Top Bottom