Bifu la P-Funk na Wasafi Litafikia Kikomo?

kama hakuongea kwa fact na akajibiwa bila fact,zinakuwaje intrest za lebel???

iliyoshutumiwa ni lebel nzima,anajibu sallam.
Salam kakosea kumlipua mwamba kwa vitu personal lakini pia P Funk hakupaswa kujibiwa kwa kuwa yeye ni nani ajibiwe, mtu anaepaswa kujibiwa ni yule ambaye mhusika anapolalamika kwa watu au kupitia social media.

P Funk alitakiwa atoe udhibitisho kwa kuwa yeye ndio anaetoa tuhuma na sio kujibiwa
 
kama hakuongea kwa fact na akajibiwa bila fact,zinakuwaje intrest za lebel???

iliyoshutumiwa ni lebel nzima,anajibu sallam.
Ulitaka ijibu label asijibu mtu aliye kwenye label? Label ni watu na Sallam is part and parcel katika WCB.
 
kwenye iyo kesi P Funk alilipwa hela kutokana na mdundo(beat) sio nyimbo nzima
Midundo ambayo Prof J aliipia, vipi waliotia vinanda yule Mrundi Bizimana(Bizzman) na mtengeneza midundo Chief Rumanyika walipata kiasi gani kwenye hayo malipo? Intellectual rights zao walizipata kwa huo mdundo kutumika?
 
-Unaweza kuwa sahihi kuwa P Funk ana ushahidi lakini hata Sallam anaweza kuwa na ushahidi wa jinsi naye alivyomnyonyaji.
-Naamini kama yawezekana kuwa P Funk si kichaa hali kadhalika yawezekana pia Sallam naye si kichaa anajua asemacho na yuko sahihi kama alivyo sahihi Majani.
 
Hii sio hasira ya kawaida
 
Hawajui, wasanii walikuwa wanapigwa makofi mbele za watu, na mitusi juu, unataka kutoka hutaki.
 
Disney walitumia nyimbo ya Chameleon Bomboclat, sio nikusaidiaje ya professor Jay… beat ni mali ya producer na sio msanii, labda utoe mpunga mrefu kulinunua… unajua Pfunk alitumia kiasigani kuwalipa composers mbali mbali kwenye hilo beat?

Mfano aliyepiga kinanda yaweza kuwa bizman, soggy akaweka set ya drums, mixing majani mwenyewe na mastering chizan brain… nimetolea mfano tu….tatizo bongo ngoma ikitoka watu wanamjua muimbaji tu…

Muziki ni professional kama nyingine tu, hapo bado suala la ufuatiliaji wa hiyo hela kuanzia kwa Chameleon mpaka huko Disney nani alofanya na kwa gharama zipi?

Cheki hizo attached pics ndio utajua kuwa bongo nyoso… licha ya dre kuwa producer mkubwa hiyo beat imegongwa na Scott Storch, Jay z akaandika mashairi… Credit zimeenda kwa wahusika bila hofu yeyote… Pfunk alitaka kulita huo mfumo toka zamani kwa kushirikisha watu mbalimbali kwenye kazi za wasanii, mfano ile beat ya Ngwear she got gwan Soggy ana mkono wake mkubwa tu, tatizo hao wa cartel wa game bongo ndio hawataki Maendeleo ya sanaa zaidi ya Maendeleo yao binafsi kwanza.

Watu wamesacrifice mengi, imagine pfunk angefocus kwenye taaluma (uwezo ulikuwepo) hao watoto wa mbwa kala mbwanda ungewajulia wapi sijui… same with master Jay na yule mzungu Mika
 

Attachments

  • 98C77E1E-29C9-4A38-A8E9-CABECEE9FBEB.jpeg
    64.1 KB · Views: 10
  • 654798E6-7C2A-4D63-B031-A49CE34FC9B0.png
    36.6 KB · Views: 9
Hawajui, wasanii walikuwa wanapigwa makofi mbele za watu, na mitusi juu, unataka kutoka hutaki.
Enzi za majani mdosi ndio alikuwa anapiga hela ndefu, wao walikula kwenye show zaidi, mfano ugali ya Nature- kumbuka hapo Fella yule yule wa wasafi akiwa ndio boss wa Juma nature huku akila na cartels wa media hasa Joseph kusaga (Kumbuka kisa cha mtoto Iddi kumdhurumu hadi Joseph kusaga mpaka akawa anatafutwa alilipe deni alilokopa kwa bwana Joe) ….

Majani na ngoma za Tip top kuanzia kwa Madee, achilia mbali kina Pingu na Denso ile ngoma ya Joanita na kina keisha wote walikuwa chawa wa Abdul Bonge na Tale huyu huyu wa Wasafi… Infact wezi wa wasanii wapo clouds asili na usafini…. No wonder kote wapo hao hao….. Pfunk was just a victim kama Mika mwamba, MJ, Kameta, Ngwear and so forth, sema wengine vifua vya ku-come out of the closet hawana
 
Majani ni sawa na ule msemo wa Kiswahel usemao NYANI HAONI KUNDULE.. wakati huo akiwa ndio producer anayevuma aliwanyanyasa na kuwanyanyapaa mno wasanii
 
Kwa hiyo Msanii kama Mboso kuwa WCB ananyonywa ama anafaidika?.

Maana ni vyema tujue mapema kabla naye hatujasikia kesho anasema hayo hayo.

Wale wenzake waliokuwa naye Yamoto Band wako wapi? huko walipo ni kheri kuliko alipo Mwenzao Mboso pale WCB?...kwa hiyo akija Beka au Enock akamwambia Mboso "toka huko unanyonywa njoo huku nilipo" Mboso atatoka na kumfuata Beka?.

Ninachokiona mimi ni kuwa kuna elimu kubwa inayohitajika kwa Wasanii haswa ukizingatia wengi wanatokea kwenye mazingira magumu yanayowapa nafasi finyu ya kuwa na uchaguzi sahihi haswa kwenye upande wa kusaini mikataba.

Hayo yanayowaliza Wasanii leo vipi kama wangepambana nayo kabla yakusaini?...tumeona hapa juzi kati kuna Mchezaji kutoka nje na aliyezua gumzo nchini tunaambiwa walitumia karibia siku nzima kujadili mkataba kabla ya kukubali kuusaini maana anajua fika akishasaini hatokuwa na uchaguzi tena zaidi ya kutekeleza masharti ya mkataba.

Pia ni vyema Wasanii wawe na tabia ya kujikumbusha mikataba yao mara kwa mara kujua wapo kwenye mazingira gani kabla hawajaamua kufanya maamuzi yanayowalazimisha kuomba huruma ya Wananchi.
 
Anawaonea wivu WCB akae kwa kutulia watu watengeneze pesa.
 
Master Jay yupo vizuri pili jamaa ana degree ya Electrical Engineering kutoka Uholanzi plus Sound Engineering, elimu inasaidia na ndio mana wasanii weliosoma miaka ya nyuma pamoja mziki kuwakataa il bado wapo vizuri.
Kasomea Zion collage ya uko uholanzi

Angekuwa kichwa angegusa UDSM
 
Kasomea Zion collage ya uko uholanzi

Angekuwa kichwa angegusa UDSM
Ndio tabu ya kuklemisha vipi walio soma Oxford au MIT sio vichwa.

Master Jay husimchukulie poa mama yupo UN kitambo,so hivyo vitu kwake vidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…