Hii ndiyo Taarifa ya mwisho niliyoipata kuhusiana na Masalia ya Dinasour huyo?
WABUNGE Kumi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameanzisha kamati maalum ya kuhakikisha sehemu ya mapato ya utalii yanayotokana na mabaki ya mjusi mkubwa aliyeko katika jumba la makumbusho Mjini Berlin nchini Ujerumani yanarejeshwa hapa nchini. Mjusi huyo anatambulika kwa jina la DINOSAUR ambaye mabaki yake yalivumbuliwa zaidi ya miaka 100 iliyopita katika eneo la Tendaguru mkoani Lindi. Tangu kugunduliwa kwa mabaki hayo na hata kusafirishwa hadi mjini Berlin nchini Ujerumani hakuna kiasi chochote cha mapato kilichowahi kurejeshwa hapa nchini ikiwa ni faida inayotokana na utalii wa mjusi huyo hali iliwalazimu wabunge hao wakiongozwa na mwenyekiti Riziki Lulida kuanzisha kamati hiyo .