Big Brother Africa 2009: The Revolution

Big Brother Africa 2009: The Revolution

Mimi nadhani hawa twins watamweka mahali pabaya sana Elizabeth, kwani watamchukulia kama adui wao. Nadhani unafuu kwa Elizabeth ni kutolewa kwa twins. Pia nadhani Namibia wataamua kumsave Rene na kuwatosa twins. Binafsi simpendi Rene kwasababu kapinda (amezidi uchizi/huenda anapata hata unga) pia hana urafiki na Elizabeth lakini pia haonyeshi madhara kwa Elizabeth. On this case ni bora angalau mmoja kati ya twins akatoka kama si wote.
 
Kosa la Tawana BBA3, hakuwa consistent. Naweza kusema alikuwa cha wote. Alipoingia alikuwa attracted kwa Munya, lakini Munya alikuwa anamtaka Lucie. Tawana akajikuta anajibamiza kwa TK (Zambia), akampa BJ mara moja na ndiyo ikawa mwanzo na mwisho. Aliporudi toka Dampo aliishia kuwa frustrated kwa kuwa TK alishaamua kuwa na Sheila (Kenya), Tawana akajikuta ana hang hana pa kwenda. Baada ya Lucie kutolewa, Tawana alimtongoza Munya kwa makubaliano kwamba no strings attached, na kwamba mambo yataishia humo humo ndani. Yule dada nadhani ana matatizo, maana kwake ngono ndio dawa ya kumuondolea frustration na alikuwa anaonekana kwamba asipofanya muda mrefu anachanganyikiwa na aliwahi kumwambia Big Brother kwamba yeey anataka mtu wa kumpa dose tu. Munya alipoenda Finniland, huku nyuma Tawana akagawa denda kwa Ricco na hao marafiki 2 wakawa wanamzunguka wote wanamshughulikia bila yeye kujua kwamba anazungukwa na watoto wa mjini. Hilo ndio lilikuwa kosa la Tawana. Kilichomsaidia akafika mbali ni kwamba alishinda HoH nyingi nadhani kuliko housemates wengine wote na pia baada ya kutoka Dampo hakuwahi kuwa nominated for eviction.

Kosa la Tawana ni sawa na kosa la Kweku T (Ghana - BBA2), jamaa kalikuwa ka-kasanova flani nadhani aliwatokea wadada 3 au 4 kama sikosei, na wote aliowatokea walikuwa kwenye kundi moja wakati wanaanza. Siku alipopanda kwenye eviction hakurudi ndani ya Jumba, ndio ilikuwa kimoja.

Kila la heri kwa Hannington na Mzamo, wanaweza kutengeneza kapo ambayo iko independent, tofauti na JEMMA ambayo ninaona inaingiliwa na influence ya headmistress (Paloma). Sikutarajia kumsikia Emma akisema ham-trust Jeremy eti kwa kuwa Jeremy amekuja kwa malengo ya game, je, hao aliowataja kwamba ana wa-trust wao wameenda kucheza makida makida? Hoja hiyo imetolewa na Paloma na Emma ameichukua na kuimeza kama ilivyo bila kufikiria. Yaani mtu umgawie denda na bado useme hum-trust, sasa hao wengine anaowa-trust wana nini ama wamempa nini? Emma anafuata msimamo wa Paloma ambaye ameishaapa kwamba hatakuwa na mahusiano yoyote, so anataka Emma awe na msimamo kama wake ili ikifika siku ya kumtoa kafara Jeremy iwe ni rahisi, kwa kigezo kwamba Jeremy nae ni mshindani.

Umenikumbusha mbali sana hii story ya Tawana nimejikuta nacheka, maana siku ile alipokuwa nominated kamuomba jamaa uroda eti waagane, ikapigwa mchana na jua kali live live, duu yule mtoto tungekuwa tunasali kule kwa nanii tungesema ana pepo la ngono.

Emma hakustuka kuwa Paloma ni Nyoka, lakini sasa naanza kuhisi kuwa huenda Elizabeth alishashtuka kuwa Paloma hafai, na huenda ameshamchukia kwa characters zake kwa hiyo ameamua kumtosa kweli. Anyetakiwa kutoka sasa baada ya Paloma nadhani awe Emma naye anakimdomo domo sana, kama ulivyosema hajiamini, Ukimuangalia Jerremy sio wa kutokuaminika kihivyo nadhani Emma ameonyesha kutokuwa na msimamo. Kwenye Forum watu wansema anamtaka Hannington sasa sijui kama ni kweli hii.
 
Mimi nadhani hawa twins watamweka mahali pabaya sana Elizabeth, kwani watamchukulia kama adui wao. Nadhani unafuu kwa Elizabeth ni kutolewa kwa twins. Pia nadhani Namibia wataamua kumsave Rene na kuwatosa twins. Binafsi simpendi Rene kwasababu kapinda (amezidi uchizi/huenda anapata hata unga) pia hana urafiki na Elizabeth lakini pia haonyeshi madhara kwa Elizabeth. On this case ni bora angalau mmoja kati ya twins akatoka kama si wote.
No no lile ni game tu as the head of the house lazima amchague mtu so shaka ondoa hakuna uadui pale
 
ni vizuri watu wawe na tabia nzuri bwana.mana pale jamii inaona,washiriki wakienda wanajisahau kama vile hawatatoka?maisha ya nje yako tofaut
 
No no lile ni game tu as the head of the house lazima amchague mtu so shaka ondoa hakuna uadui pale

lakini mkuu wapiga kura kwenye nchi uliyomtosa mtu wako lazima wakumwage tu, si ulioona mwaka jana Mimi aliwatosa wanaigeria, ilipokuaja yeye walimumwaga vibaya mno ingawa ni ECOWAS mwenzao, haya mambo huwa yanavisasi sana. Nasubiri kuona kama kutakuwana HoH atakayekuwa na ujasiri wa kusema sireplace mtu na mimi niwekwe kwenye nomination for possible eviction, hakuna anayejiamini hapo ha ha Patakuwa patamu.
 
ni vizuri watu wawe na tabia nzuri bwana. mana pale jamii inaona, washiriki wakienda wanajisahau kama vile hawatatoka? maisha ya nje yako tofaut

Tabia nzuri ni relative term, to some of us inaanzia kwenye mavazi, lugha anayotumia, na hata usafi wa kwake mwenyewe. Paloma ambaye anaonekana kuwa kinara wa kurekebisha tabia, ni mtukanaji mkubwa, hachelewi kumwambia mtu stupid, hakuna tusi dogo wala kubwa, yote ni matusi tu. Kwa hiyo hata Paloma mwenyewe ana tabia mbaya ya kuwadharau wenzake na kuwatukana na kuwaona kama wajinga, esp wale ambao hawakubaliana na misimamo/maoni/mawazo yake.

Washiriki wote wako above 20, hakuna aliye under age. Kila mshiriki amekulia kwenye mazingira tofauti na mila tofauti. Kwa wengine hata kuvaa vivazi vya kuogelea ni sawa na kuwa uchi, niambie siku ile Elizabeth na Emma wanapigana (mchezo) kwenye bwawa la tope, mbona maziwa yalikuwa almost yanataka kuchomoka kwenye bra zao, hapo utasema ni kosa la mshiriki?

Kinachotakiwa ni namna gani mshiriki anaweza kuchangamana na watu tofauti wenye background tofauti, na akaweza kuishi nao bila ya mikwaruzano mikali. Siyo kazi ya mshiriki kuanza kuwaelekeza/kuwa-command kwamba wanatakiwa kuishi namna gani, ni juu ya watazamaji kuamua kwamba hii show inafaa kuangaliwa au la na ndiyo maana ni show ya watu wa miaka 18 na kupanda juu kwa kuwa humo ndani kuna lugha za matusi na wakati mwingine mambo mengine yako wazi sana.
 
Mimi nadhani hawa twins watamweka mahali pabaya sana Elizabeth, kwani watamchukulia kama adui wao. Nadhani unafuu kwa Elizabeth ni kutolewa kwa twins. Pia nadhani Namibia wataamua kumsave Rene na kuwatosa twins. Binafsi simpendi Rene kwasababu kapinda (amezidi uchizi/huenda anapata hata unga) pia hana urafiki na Elizabeth lakini pia haonyeshi madhara kwa Elizabeth. On this case ni bora angalau mmoja kati ya twins akatoka kama si wote.

Elizabeth hakuwa na jinsi, maana yeyote yule ambaye angempendekeza bado angekuwa amejenga uadui na mshiriki mwenyewe na pia nchi husika.

Kwangu mimi wote walio up for eviction naona wanafaa kutoka kwa sababu zifuatazo:

Rene ni kweli amepinda sana na ninaona kwamba ameshindwa kabisa kuendana na wadada wenzake na alishasema yuko open minded na anaweza kujiunga na alliance yoyote ile, given that mtu asije kumwambia nani awe nominated, kwa kifupi hataki dictatorship.

Paloma ni dictator kwa ajili ya interest zake, anataka maoni yake yasikilizwe, yaheshimiwe na yatekelezwe. Kila mshiriki anatakiwa awe na independent strategy ambayo inaendana na ya group lake. Kuwa kwenye alliance haimaanishi kwamba members wako sio washindani. Paloma alikuwa anatumia Girl Power kama njia ya yeye kutokuwa nominated, na sasa bado anapiga mahesabu kwamba imekuwaje akawa nominated, ilhali alijua ndani ya Jumba ana numbers.

Kwa upande wa twins, sioni kama ni haki wote 2 wakaendelea kuwa ndani ya Jumba, kwa kuwa bond yao ni kubwa sana na wanaaminiana sana. Kwa hiyo akitoka mmoja siyo vibaya.

Lakini ukiniuliza nani atoke kati ya hao wanne, jibu langu ni simple, PALOMA. Huyu dada anavuruga sana independent strategies za wenzake na hata kitendo cha Elizabeth kumpandisha Erastus in maamuzi ya Paloma. Lakini je, twins waki-save wote, huoni kama ni kasheshe kwa Elizabeth? Hilo ndiyo linalonifanya nione kwamba Paloma hafai, anaweza kumtumia Elizabeth na baadaye akaja kum-dump.
 
What I didnt like about her nomination was putting all three Namibians to the eviction raw. The results is that whatever will happen, she will stand to face the Southern Alliance which iz Zimbabwe, South Africa and Namibia minus Botswana.

The girls' alliance of thinking that by nominating the twins, they are paving the way for their victory which our Elizabeth has bought won't work.
 
Paloma sio mnafiki anaishi maisha halisi sio muigizaji. Baadhi yetu tunapenda sana kuishi artficial life has tunapofukuzia demu au dili fulani, kwa mfano mabrother watajifanya hata kupika ukitembelewa na kidosho but baada ya kuona au kumlamba, unang'aka jikono siingii.

Paloma anaishi kama alivyo. She is a real African woman wdo do what her heart and mind tell her. Wengine kuanzia kiingereza mpaka kujipodoa, kula na mengineyo ni artificial life. Sana na jamaa wa Botswana anaishi maisha yake halisi kama alivyo.
 
Tabia nzuri ni relative term,

.

I agree with yu bra!!

Anayesema wanajisahau, wanajisahau kwa lipi? kwani huku mitaani watu hawa-date, hawa-kiss au kubanjuana? kwani watu wanaogopa kwenda guest houses/hotels? mbona tunaona watu kibao tu wanaingia na kutoka na tukijua fika wametoka kubanjuana na tunaona kuwa ni sawa? au reality show kwako ni kitendawil?
 
Future of Girl Power and Non-smokers Alliance

Mpaka dakika hii Girl Power imeishakwenda na maji. Nimemuona Liz akilalamika kwamba wasichana sasa wameamua kuwa na opinion za kwao independently (which is right), na kwamba hawasikilizi tena maoni yao (Liz na Paloma). Kwamba wakiguswa they shout back. This is a good sign so far. Kristal alishaonyesha kuwa more independent tangu mwanzo na hakuwa anabanwa na maamuzi ya Paloma + Liz on who they should nominate, japo Paloma na Liz bado wanamhesabu kama ni mwenzao. Kwa kifupi ni kwamba ninaona dalili zote za Girl Power kufikia tamati. Jana ndio ilikuwa ni mwanzo wa kusambaratika baada ya viongozi wa Girl Power kuwa nominated for eviction, hiyo ilikuwa ni clear msg kwamba kumbe hakuna tena Girl Power. Watu wameamua kuwa na misimamo yao peke yao na hapo ndipo ninapomuona Rene kama shujaa aliyeamua kuwa independent tangu mwanzo badala ya kufuata mkumbo bila kuelewa unafanya nini na kwa faida ya nani.

Kevin na vijana wake bado wako kwenye shock na hawajui what is next. Maana non-smokers walidhani kwamba waki-team up na Girl Power wangeweza kufika mbali, lakini baada ya kuona Liz na Paloma wakiwa nominated, they are now insecure na hawajui nini kitatokea baadaye. Itai already ameishavunja kambi. Quinn alitegemea Mzamo awe kwao, lakini baada ya yale yaliyotokea jana usiku, sitegemei Mzamo am-back stab Hannington. Kwa hiyo wiki hii tutashuhudia new alliances na tusishangae yakaja makundi 3 au zaidi yakiwa na mchanganyiko wa players (wavulana na wasichana).

Sunday eviction inaweza kurudisha Jumba kwenye equilibrium ama ikalipeleka jumba kwenye disequilibrium. Ninasubiri kwa hamu kubwa sana eviction ya sunday. Mpaka dakika hii Namibia wanaongoza kwa goli 1 kwa 0 against Zambia. Sijaona watu wakimpigia debe/kampeni Paloma kwenye forums za BBA na blogs za Zambia. Lakini game ni dakika 90, tusubiri siku ya Jumapili maana bado iko mbali na lolote linaweza kutokea.
 
Paloma sio mnafiki anaishi maisha halisi sio muigizaji. Baadhi yetu tunapenda sana kuishi artficial life has tunapofukuzia demu au dili fulani, kwa mfano mabrother watajifanya hata kupika ukitembelewa na kidosho but baada ya kuona au kumlamba, unang'aka jikono siingii.

Paloma anaishi kama alivyo. She is a real African woman wdo do what her heart and mind tell her. Wengine kuanzia kiingereza mpaka kujipodoa, kula na mengineyo ni artificial life. Sana na jamaa wa Botswana anaishi maisha yake halisi kama alivyo.

Wote hapa duniani at one point huwa tunaishi artificial life ikitegemeana na uko na watu wa aina gani na una malengo gani. Kinachotakiwa ni mtu kutokwenda kwenye extremes (ku-overdo) na hicho ndio huwa kina wa-expose wengi na hatimaye kuumbuka.

Kwanza labda nikuulize, nini maana ya mtu mnafiki? Nini maana ya maisha halisi? Kusema kiingereza ni kuishi artificial life? Kula vyakula wanavyopewa na BB ni artificial life? Hata kama kwao alikuwa anakula pumba, kama haziko kwenye shopping list unataka aagize wapi? Kutumia vipodozi nayo ni nongwa?

Kwamba Paloma anafanya kile ambacho moyo na akili yake vinamtuma afanye, very true. Alienda kusaka dollar laki 2, kwa hiyo moyo na akili yake vinamtuma kwamba lazima apate hilo donge kwa njia yoyote ile na alisema tangu siku ya kwanza anaingia hapo ndani. Kama umesahau naomba pitia tena clips zao usikie maneno yake, alisema yuko tayari ku-back stab kama itamsaidia kushinda. She is the biggest pretender hapo ndani na nina hakika kuna wanaume wanamvutia, ila kwa kuwa anataka donge nono hana jinsi inabidi aishi artificial life.

A typical African Woman hawezi kuambiwa geuka tuone wowowo lako na akatimiza, hilo ni tusi kwa maadili ya kiafrika. Siku alipokuwa anaingia mashabiki walimuomba ageuke na aligeuka mpaka IK akamuuliza vipi? Akasema mashabiki wameomba nigeuke, huyo ndiyo unasema mwanamke wa kiafrika halisi ambaye yuko tayari ktingisha wowowo lake ili apate kura? Tuache game liendelee na tusije kuleta hoja ambazo hazina mashiko.

Kwa kifupi ni kwamba Paloma ame-copy na ku-paste strategy za Cherise (the winner of BBAI) ambaye alikuwa kama mlokole tangu day 1 mpaka siku anatoka and she kissed Mwisho only, tena siku ya mwisho kabisa. Advantage ya Cherise ilikuwa ni kwamba alikuwa mkimya hakuwa mpiga domo kama Paloma ambaye saa zote ni ku-discuss nominations na alliances, hana kitu kingine cha kufanya zaidi ya hivyo. Ofuneka (Nigeria BBA II) nae alijaribu ku-copy na ilim-save mara moja akaondolewa kwenye nominations kwa kigezo kwamba jiko lingechafuka maana ndio demu pekee aliyekuwa anajishughulisha na mambo ya usafi na kupika jikoni. Hazel (Malawi BBA 3) nae alikuwa hivyo mpaka akawa analalamika kwamba anafanya kazi nyingi na watu hawa-appreciate.

Wote hao niliowataja walikuwa wanapenda shughuli za jikoni na kujifanya wako poa kiaina, lakini hayo siyo maisha yao halisi. Wape ulabu kidogo uone kama hawajachanganyikiwa. Ofuneka alifanya maajabu wiki ya mwisho kabisa sababu ya pombe. Kuna siku Hazel alilewa akawa anajichekea ovyo ovyo na kuwakalia wanaume mapajani, lakini ukimkuta hajanywa pombe unaweza kusema umekutana na mwanamke wa kiafrika mwenye nidhamu ya kutosha na kumbe ni usanii mtupu.

BBA is just a game hakuna maisha halisi hapo ndani, lazima kuna sehemu watu wanaigiza. Maisha halisi tunayoyaona ni kasehemu kadogo sana ka maisha yao ya huko mtaani. Wengi wao wanaishia kuigiza tu na kujifanya wako hivi ama vile, lakini ukweli ni kwamba hawako hivyo ila wanafanya hivyo ili washinde na ndiyo maana kuna alliances na kuchunguzana na ku-pretend.
 
What I didnt like about her nomination was putting all three Namibians to the eviction raw. The results is that whatever will happen, she will stand to face the Southern Alliance which iz Zimbabwe, South Africa and Namibia minus Botswana.

The girls' alliance of thinking that by nominating the twins, they are paving the way for their victory which our Elizabeth has bought won't work.

Mkuu hapo juu umenigusa, ni kweli nimeanza kuona kosa la Elizabeth. Last year voting ilikuwa inaenda ki-kanda kanda, nina mashaka na mwaka huu inaweza kuwa hivyo. Lakini hiyo idea ya twins sidhani kama Elizabeth alishiriki ila alishawishiwa na Paloma, Liz na Emma kwamba ili twin mmoja atoke inabidi wote 2 wawe up for eviction. Dakika za mwisho kabisa mmoja aliuliza suppose kukiwa na more than two nominees? Hawakuwa na jibu na sijui kama waliendelea na discussion.

Advantage ya Big Brother ni kwamba anaona na kusikia kila kitu na hivyo ni rahisi kuvuruga moves za alliances kama alivyowavuruga this time. Sasa hivi nyumba ina joto kali sana (tense situation), maana wale waliokuwa wanahisi wako more secure, hawako salama tena. Thanks to Itai kwa ku-break ranks na Girl Power.

Very true, strategy ya Girl Power it wont work! Lakini ukweli unabaki pale pale Paloma amemtumia Liz kwa malengo yake binafsi na huo ndiyo unafiki wenyewe. Thinking ya Paloma ni kwamba Elizabeth is not a strong contender kwa hiyo wanaweza kum-deal siku yoyote na kumchinjilia mbali.
 
Umenikumbusha mbali sana hii story ya Tawana nimejikuta nacheka, maana siku ile alipokuwa nominated kamuomba jamaa uroda eti waagane, ikapigwa mchana na jua kali live live, duu yule mtoto tungekuwa tunasali kule kwa nanii tungesema ana pepo la ngono.

Emma hakustuka kuwa Paloma ni Nyoka, lakini sasa naanza kuhisi kuwa huenda Elizabeth alishashtuka kuwa Paloma hafai, na huenda ameshamchukia kwa characters zake kwa hiyo ameamua kumtosa kweli. Anyetakiwa kutoka sasa baada ya Paloma nadhani awe Emma naye anakimdomo domo sana, kama ulivyosema hajiamini, Ukimuangalia Jerremy sio wa kutokuaminika kihivyo nadhani Emma ameonyesha kutokuwa na msimamo. Kwenye Forum watu wansema anamtaka Hannington sasa sijui kama ni kweli hii.

Tawana was gross, hafai kabisa. Akiwa Dampo aliwahi kumsimulia LaToya kwamba kule kwao ana orodha ya wanaume, akimpigia wa kwanza akajifanya yuko bize anampigia aliye available anakwenda anatoa huduma then biashara inakwisha. Kweli kabisa yule dada ana pepo la ngono, maana alivuka mipaka.

Emma alionyesha kwamba kama Jeremy angeonekana kuvuta miguu, basi angejisogeza kwa Hannington, hiyo ilikuwa kabla hawajaunganishwa. Kuna siku Emma alimwambia Hannington kwamba anatakiwa kujiweka soap soap, akate kucha za miguuni, na pia usafi wa nywele na ndevu. Nadhani ndevu za jamaa zina wa-irritate wanawake wengi walio ndani ya jumba.

Lakini je, Hannington atakubali kumwacha Mzamo? Advantage ya Mzamo ni kwamba yuko independent, tofauti na alivyokuwa kwenye alliance ya Girl Power. Jana usiku walipokuwa wana-kiss ilikuwa wazi wazi kila mtu aone na siyo kufunikana mashuka wanajifanya wanaongea na kumbe wana-kiss. Emma bado ana-influence ya Paloma na ndiyo maana hata uhusiano wao umekaa kiaina aina, kama wa Hazel (Malawi) na Thami (South Africa) mwaka jana.
 
Bad News

Jumapili wanaondoka washiriki 3, yaani hapo nimeishiwa nguvu kabisa na ninaona wapiga kura wameisha-panic na hawajui nini kifanyike. Kwa mwendo huu naona Paloma anaweza ku-save kwa sababu kugawa kura kwa housemates 3 ambao wanatoka nchi moja ni kazi ngumu na utata zaidi unaongezwa na mapacha. Nani apewe na nani anyimwe kura.
 
Mkuu hapo juu umenigusa, ni kweli nimeanza kuona kosa la Elizabeth. Last year voting ilikuwa inaenda ki-kanda kanda, nina mashaka na mwaka huu inaweza kuwa hivyo. Lakini hiyo idea ya twins sidhani kama Elizabeth alishiriki ila alishawishiwa na Paloma, Liz na Emma kwamba ili twin mmoja atoke inabidi wote 2 wawe up for eviction. Dakika za mwisho kabisa mmoja aliuliza suppose kukiwa na more than two nominees? Hawakuwa na jibu na sijui kama waliendelea na discussion.

Nadhani Eliza ameliona hili maana jana niliona anajichanganya na Kaone kijana wa Botswana. Nadhani ni strategy nzuri sana, maana kumsamehe Hannington ambaye atatolewa tu inampa kura ya Uganda, na kumleta Kaone ambaye bado haileweki kama ana nafasi kama akitoka mapema basi yeye atakuwa na kura ya Botswana atakuwa amewagawa jamaa wa kusini, watswana hawaaminiki laikni wana weza kuamua kumpigia kura Msouth afrika mzungu kuliko Mwafrika mwenzao. Lakini mpaka sasa naona move yake na strategy yake, which is a good move.

shida ni Mkimya mno, engeongeza kidogo tu, Hata hivyo nina matumaini makubwa sana naye.
 
Lakini hannington naye macahle yamemcheza, kuanza uhusiano na Mzamo kumemuongezea credit sana, wiki iliyopita alikuwa nazungumzwa vibaya sana, lakini jana watu wamegeuka ghafla wanampa maujiko. Jamaa naye kaona mbali sana, kwa hiyo sio weakest link kama tunavyodhani. Lakini mimi ningedhani akina Geradine na Nkenna kama hawapo vile na watu wanawasahau hawa ndio wa kuwamwaga mapema.
 
Siku zote watu wakimya huwa wanafika mbali ili mradi wacheze game vizuri. Unajua wale ambao ni wasemaji sana ni rahisi kukwaruzana na washiriki wengine.

Ukimya wa Geraldine unaweza kumfikisha mbali, maana ikifika wakati wa nominations, housemates wala hawakumbuki kama kuna mshiriki mwenye jina hilo. Nkenna amejisogeza sana kwa Paloma na Liz na hilo linaweza kumletea kasheshe kwa kuwa Paloma ana maadui wengi. Jeremy tayari ameishasema hao watu wanamkera sana hapendi attitude zao.

Hannington leo anaonekana yuko super baada ya kuwa na uhakika wa mapozeo kutoka kwa Mzamo. Hata kama hawafanyi chochote, lakini uwepo wa mtu mwingine ambae anaweza kukufariji na kukuambia pole na kuku-encourage, inatosha sana. Wasiwasi wangu ni mmoja kwamba JEMMA imekufa rasmi na wame-settle for a friendship, na mtoto amekuwa disappointed. Je, anaweza kumsogelea Hannington? Maana kijana naona amepunguza ndevu zake na pia amesuka nywele, vitu ambavyo Emma alisema vinam-irritate. Na si ajabu ameishakata kucha za miguuni pia. Yetu macho kuangalia mambo yanavyokwenda ndani ya jumba.
 
Nadhani Eliza ameliona hili maana jana niliona anajichanganya na Kaone kijana wa Botswana. Nadhani ni strategy nzuri sana, maana kumsamehe Hannington ambaye atatolewa tu inampa kura ya Uganda, na kumleta Kaone ambaye bado haileweki kama ana nafasi kama akitoka mapema basi yeye atakuwa na kura ya Botswana atakuwa amewagawa jamaa wa kusini, watswana hawaaminiki laikni wana weza kuamua kumpigia kura Msouth afrika mzungu kuliko Mwafrika mwenzao. Lakini mpaka sasa naona move yake na strategy yake, which is a good move.

shida ni Mkimya mno, engeongeza kidogo tu, Hata hivyo nina matumaini makubwa sana naye.

Baada ya News kwamba washiriki 3 watafungasha virago weekend hii, nimeona kwamba move ya Elizabeth haiwezi kuwa madhara makubwa. Kama itatokea m-Namibia mmoja kabaki basi ndani atabaki na adui mmoja, wakiondoka wote ndani atakuwa hana adui. Atabaki na adui mmoja wa nje ambaye ni sawa na adui mwingine yeyote. Kum-swap Liz inaweza kuwa advantage kwake kwamba may be siku moja South Africans wanaweza kumpa kura, japo ni kura ambayo haina uhakika sana.

Ukimya wake sioni kama ni mbaya sana, angalau yupo yupo siyo kama Geraldine. Tatizo ni pale atakaposhindwa ku-handle maswala humo ndani maana naona K1 yuko bennet fulani hivi na pia Elizabeth mwenyewe alikuwa anamwambia BB kwamba ameanza maongezi na K1 na sijui direction ya hayo maongezi, let us hope yataishia pazuri bila ya kujenga uadui ama uhasama.
 
Updates za Leo asubuhi

Niliyoyasema jana naona yameanza kutimia. Leo asubuhi Paloma alikuwa anawashawishi Emma na Eliza kwamba next ni kumtoa Kevin. Kevin alikuwa ni kama kiongozi wa Non smokers alliance ambayo ilikuwa imeungana informally na Girl Power.

Nkenna (Nigeria) ni member wa Girl Power, je, atakubali kumsaliti Kevin ambaye wanatoka nchi moja? Jana asubuhi Nkenna alikwaruzana na Emma na Emma alionekana mwenye hasira siku nzima, je, hakutakuwa na kisasi kutokana na mikwaruzano hiyo?

Wakati Paloma anaanza kuongelea mambo ya nominations na hatimaye jinsi Kevin alivyomtazama wakati wanafanya mazoezi, Liz na Kristal waliamua kuondoka, hiyo nayo haikuwa sign nzuri.

Wakati wa diary session a typical African Woman amemwaga mchozi, mtu ambaye alikuwa anajiona yuko strong kuliko wasichana wote. Tayari ameishaona kwamba amebaki kisiwani. Alipata matumaini alipochaguliwa kuwa HoH wa akina dada wakati wakiwa wako peke yao na hivyo kujiona ana aminika sana among wasichana, lakini naona amehisi upepo umegeuka.

Jana, wa-Nigeria walikuwa wanampigia debe/kampeni Paloma kwamba apigiwe kura ili abaki kwenye jumba kwa kuwa yuko close na Kevin, na Paloma akibaki kwenye jumba itakuwa ni advantage kwa Kevin. Kauli ya Paloma aliyoitoa leo kwa akina dada, imem-cost kupoteza kura moja (Nigeria) ambayo ni muhimu sana kwake.

Kura nyingine ambazo atapoteza ni pamoja na ya Namibia, Malawi (kwa kuwa ana kasheshe na Mzamo na alitaka kum-nominate), ya Zimbabwe (kwa kuwa alitaka pia kum-nominate Itai), ya Ethiopia (kwa kuwa yuko against Yacob mwakilishi wa Ethiopia), Uganda (kwa kuwa ana kasheshe na Hannington). Pia naona kuna dalili za kupoteza kura ya Botswana kwa kuwa K1 yuko bennet sana na Kevin na kum-target Kevin ni sawa na kuwa-target K1 na Quinn. Kwa kifupi nchi ambazo zina wawakilishi wanaume lazima zitajiuliza mara 2 kabla ya kumpigia kura ya kubaki kwenye jumba, maaana akibaki bado ataendeleza kampeni za kuwatoa wanaume wote kwanza. Pia closeness na Liz nayo imeanza kupungua kitu ambacho kinamuweka pabaya. The only advantage she has, ni kwamba anapambana na 3 Namibians kwa hiyo wapiga kura hawajui wampe nani kura kati ya hao 3, na pia uwepo wa mapacha una-complicate zoezi lote na watu wanachanganyikiwa wampe pacha yupi kura zao.

Hapo ndipo ninaposema kwamba hakuna anayeishi maisha halisi, maisha halisi ni pamoja na kuwa mkweli. Huyu ndiye Paloma aliyesemwa kwamba siyo mnafiki, kama kweli Kevin ni mtu aliyekuwa anamwamini na wako kwenye alliance moja, kwanini hakwenda kum-face amuulize na badala yake anaanza kuwashawishi akina dada wam-nominate siku ya Jumatatu? Mbona alienda kum-confront Itai siku alipoambiwa kwamba Itai ameuza strategy ya alliance?
 
Back
Top Bottom