Paloma sio mnafiki anaishi maisha halisi sio muigizaji. Baadhi yetu tunapenda sana kuishi artficial life has tunapofukuzia demu au dili fulani, kwa mfano mabrother watajifanya hata kupika ukitembelewa na kidosho but baada ya kuona au kumlamba, unang'aka jikono siingii.
Paloma anaishi kama alivyo. She is a real African woman wdo do what her heart and mind tell her. Wengine kuanzia kiingereza mpaka kujipodoa, kula na mengineyo ni artificial life. Sana na jamaa wa Botswana anaishi maisha yake halisi kama alivyo.
Wote hapa duniani at one point huwa tunaishi artificial life ikitegemeana na uko na watu wa aina gani na una malengo gani. Kinachotakiwa ni mtu kutokwenda kwenye extremes (ku-overdo) na hicho ndio huwa kina wa-expose wengi na hatimaye kuumbuka.
Kwanza labda nikuulize, nini maana ya mtu mnafiki? Nini maana ya maisha halisi? Kusema kiingereza ni kuishi artificial life? Kula vyakula wanavyopewa na BB ni artificial life? Hata kama kwao alikuwa anakula pumba, kama haziko kwenye shopping list unataka aagize wapi? Kutumia vipodozi nayo ni nongwa?
Kwamba Paloma anafanya kile ambacho moyo na akili yake vinamtuma afanye, very true. Alienda kusaka dollar laki 2, kwa hiyo moyo na akili yake vinamtuma kwamba lazima apate hilo donge kwa njia yoyote ile na alisema tangu siku ya kwanza anaingia hapo ndani. Kama umesahau naomba pitia tena clips zao usikie maneno yake, alisema yuko tayari ku-back stab kama itamsaidia kushinda. She is the biggest pretender hapo ndani na nina hakika kuna wanaume wanamvutia, ila kwa kuwa anataka donge nono hana jinsi inabidi aishi artificial life.
A typical African Woman hawezi kuambiwa geuka tuone wowowo lako na akatimiza, hilo ni tusi kwa maadili ya kiafrika. Siku alipokuwa anaingia mashabiki walimuomba ageuke na aligeuka mpaka IK akamuuliza vipi? Akasema mashabiki wameomba nigeuke, huyo ndiyo unasema mwanamke wa kiafrika halisi ambaye yuko tayari ktingisha wowowo lake ili apate kura? Tuache game liendelee na tusije kuleta hoja ambazo hazina mashiko.
Kwa kifupi ni kwamba Paloma ame-copy na ku-paste strategy za Cherise (the winner of BBAI) ambaye alikuwa kama mlokole tangu day 1 mpaka siku anatoka and she kissed Mwisho only, tena siku ya mwisho kabisa. Advantage ya Cherise ilikuwa ni kwamba alikuwa mkimya hakuwa mpiga domo kama Paloma ambaye saa zote ni ku-discuss nominations na alliances, hana kitu kingine cha kufanya zaidi ya hivyo. Ofuneka (Nigeria BBA II) nae alijaribu ku-copy na ilim-save mara moja akaondolewa kwenye nominations kwa kigezo kwamba jiko lingechafuka maana ndio demu pekee aliyekuwa anajishughulisha na mambo ya usafi na kupika jikoni. Hazel (Malawi BBA 3) nae alikuwa hivyo mpaka akawa analalamika kwamba anafanya kazi nyingi na watu hawa-appreciate.
Wote hao niliowataja walikuwa wanapenda shughuli za jikoni na kujifanya wako poa kiaina, lakini hayo siyo maisha yao halisi. Wape ulabu kidogo uone kama hawajachanganyikiwa. Ofuneka alifanya maajabu wiki ya mwisho kabisa sababu ya pombe. Kuna siku Hazel alilewa akawa anajichekea ovyo ovyo na kuwakalia wanaume mapajani, lakini ukimkuta hajanywa pombe unaweza kusema umekutana na mwanamke wa kiafrika mwenye nidhamu ya kutosha na kumbe ni usanii mtupu.
BBA is just a game hakuna maisha halisi hapo ndani, lazima kuna sehemu watu wanaigiza. Maisha halisi tunayoyaona ni kasehemu kadogo sana ka maisha yao ya huko mtaani. Wengi wao wanaishia kuigiza tu na kujifanya wako hivi ama vile, lakini ukweli ni kwamba hawako hivyo ila wanafanya hivyo ili washinde na ndiyo maana kuna alliances na kuchunguzana na ku-pretend.