Big Brother Africa 2009: The Revolution

Nina swali jamani, hivi kuna replacement yoyote iliyowahi kuwa evicted???
 
Nina swali jamani, hivi kuna replacement yoyote iliyowahi kuwa evicted???

yes, Elizabeth akiwa HoH alimwingiza Erastus badala ya Liz, Erastus aliondoka wiki hiyo hiyo. At least hiyo ndo ninayoikumbuka, na ndicho kinachom-cost Elizabeth mpaka leo. Huyu twin Eddie bado anataka kulipa kisasi na kinaweza kutokea wiki hii.
 
Elizabeth lazima arudi home aliniudhi alivyokuwa anajiadai na kumwambia kevin hajawahi kudate black.
 


Eliza Atapona......................
 
This week's Nominations see "countrymanship" fall by the wayside and Leonel nominate Mzamo.

Kevin Nominates Mzamo and his fellow Nigerian, Nkenna. He tells Big Brother that Nkenna is playing for the other team and is very close to Edward. He says that Edward is his rival in the House and wants him out.

After Kevin's Nomination, Emma and Elizabeth talk to him about Nkenna. He tells them that Geraldine whispered to him that she is planning to put up Edward and Mzamo but Kevin should not tell Nkenna. Kevin says that even Geraldine now has a mind of her own. He also says that he would never Nominate Geraldine because she knows where she stands.

How the rest nominated:

Edward The Head of House, Nominates Elizabeth and Emma. He plans to save his former Comrade in Arms, Emma, and put Kevin in her place.

Nkenna Nominates Emma, because she believes Emma will nominate her too. She also Nominates Edward because he can save himself.

Elizabeth puts up Mzamo because she believes Mzamo does not like her. She also puts up Nkenna because she is not honest.

Mzamo just like Edward, puts up Elizabeth (as Elizabeth had predicted) and Emma!

Itai goes for Mzamo and Emma because they represent the two sides of the House.

Leonel Nominates Nkenna, because "she did something" to him and his lover, Mzamo, because "she is a strong player". Mzamo and Leonel have been romantically involved. Leonel recently told Kevin that he wanted to end his
relationship with Mzamo to pursue Geraldine.
Leonel once expressed his love for Geraldine but she turned him down.

Geraldine goes against Nkenna and puts up Mzamo and Edward.

Emma puts up Nkenna for putting her up for Nomination last week and also Nominates Mzamo because she is close to Edward who will be able to save her.

Nkenna and Mzamo seem to be leading with the most Nominations.

source: http://www.mnetafrica.com/bigbrother/Article/
 
Kwahivo mana yake ni
Mzamo - 6
Emma - 4
Nkenna -4

Nafkili hao watatu watakua up for nominations this week kabla Ed haja swap! Nyepesi zinadai kua ed atamswap Emma na kumuweka Kevin
 
Wadau Wa JF kwanini nikipost naiona inaingia kisha niki Log out nikirudi Post Siioni au inakuwa mawazo yangu hayana maana???? please kama kuna kitu nakosea nijue.
 
Kwahivo mana yake ni
Mzamo - 6
Emma - 4
Nkenna -4

Nafkili hao watatu watakua up for nominations this week kabla Ed haja swap! Nyepesi zinadai kua ed atamswap Emma na kumuweka Kevin


Kura ziko hivi:
Mzamo=6
Nkenna=5
Emma=4
Edward=2
Eliza=2

Kwa hiyo Mzamo, Nkenna na Emma wako juu, na hatujui Edward atamwokoa nani na kumuweka nani. Tusubiri tu.
 
Walio up for eviction ni hawa wafuatao:

Nkenna

Elizabeth

Emma


Eviction ya wiki hii ni mbaya sana, Nkenna anaweza kuchomokea dirishani iwapo viewers hawatakuwa makini.

Ugomvi wa Nkenna na Kelvin unamuweka Nkenna kwenye nafasi ya kutetewa, na hivyo swala la Nigeria factor linaweza kuuawa kwa kuwa Kelvin amem-nominate Nkenna leo. So Nkenna is officially going solo.

Kitendo cha Emma na Eliza kupanga nominations za Nkenna na Mzamo, inampa advantage Nkenna so kura ya Malawi iko. Pia Nkenna ndiye rafiki wa kike wa Mzamo ambaye huwa wanapiga nae sana stori.

Nkenna alimtoa Itai kwenye kitanzi last week so kura ya Zimbabwe anaweza kuipata na alikuwa anasema anaitaka kura ya Zimbabwe kwa nguvu zote. Tatizo ni kwamba Itai ameishaanza ku-defect kuelekea kwa Kelvin na kama nchi yake inaona hiyo move wanaweza kuhamishia support kwa Eliza, lakini siyo kwa Emma. Emma alikuwa haivi na Kristal na pia kuna mmoja wao kwenye hilo kundi alimwita Kristal albino. Ni mambo madogo lakini ya effect kubwa kwenye kujenga chuki na visasi.

Emma na Eliza wana beef na Namibia kwa sababu ya kutolewa Erastus na Rene kwa hiyo kura ya Namibia iko mgongoni mwa Nkenna.

Uganda wana beef na Eliza na pia Eddie ameendelea kulia kwamba vijana wake walitolewa na hiyo alliance ya Emma na Eliza plus Kelvin, hapo kuna split kali ya kura, Nkenna anaweza kuchukua Uganda.

Nigeria iko more complex kwa kuwa Kelvin mwenyewe kajichanganya kwa kum-nominate dada yake while Nkenna hakumgusa Eliza wala Kelvin, so ana stand a good chance ya support. Pia Nigerians kama watakuwa wanafikiria nje ya box, kumtoa Eliza itamsaidia sana Kelvin wao ili aweze ku-focus kwenye game. Analysis ya hapa ina utata, najua wapo watakao mpa kura Eliza sababu ya Kelvin na wako watakaomnyima kura Eliza sababu ya Kelvin na wako ambao watampa kura Nkenna sababu ya uzawa.

Ethiopia bado wana lia Eliza na Emma kwa kuwa walishiriki kuiondoa pair ya Hannington/Yacob. Kwa hiyo hilo linampa leeway Nkenna.

Wote walio up for eviction walikuwa kwenye alliance moja, japo Nkenna ali-defect mapema na kuwaacha Eliza na Emma. Hiyo inaweza kumpa advantage Nkenna.

Kosa kubwa ambalo linaweza kumwokoa Nkenna ni kitendo cha kuwa nominated na Kevin na pia yeye kutomgusa Kelvin wala Eliza. Aliowa-nominate mmoja yuko up so hakuna hasara, mwingine ni HoH, na alisema atajiokoa mwenyewe. So hana hasara kwa hao aliowa-nominate.

Pamoja na analysis hiyo hapo juu, bado ni mapema sana kusema lolote. Itai ameishaanza kuvuraga mambo huko ndani na anaweza kuifanya nyumba iwe ya moto sana na pattern ya kura inaweza kubadilika wakati wowote. Kwa hiyo kwa sasa lolote linaweza kutokea. Kwa ujumla tutarajie mchuano mkali sana kwa kuwa kuna washiriki 3 ambao wote na kasoro zao, japo Eliza anaweza kuwa na advantage zaidi.
 

Uchambuzi mzuri.

Wiki hii tunaweza kumpokea Elizabeth nyumbani, hii inatokana na ugumu wa mfumo wa kuhesabu kura wa sasa hivi. Hata hivyo, anaweza kupona na badala yake Emma ndo akaondoka kutokana na ugumu wa mgawanyo wa kura.

Biggie kwasasa anaangalia the least popular housemate katika wale walio-nominated. Zamani alikuwa anaangalia the most popular. Labda nieleze kwa kirefu. Biggie alikuwa anampa kura ya nchi housemate aliyepata kura nyingi zaidi. Kwa mfano housemate akiongoza ktk nchi 3 basi anapewa kura 3. Mwisho anamuondoa aliyepata kura chache za mfumo huu.

Kwasasa, biggie anampa kura ya nchi housemate aliyepata kura chache kuliko wengine. Let say Tanzania - Elizabeth (1st), Emma (2nd) na Nkenna (3rd) basi Nkenna anapewa kura 1 (yaani ni kura ya kupingwa). Mwishowe atakayekuwa amepata kura nyingi za namna hii (kupingwa) ndo anaondolewa mjengoni. Biggie ameweka assumption kwamba every nominated housemate will get votes from all countries isipokuwa idadi ndo itatofautiana.

Hivyo ni ngumu sana kutabiri nini kitatokea. Ila Nkenna atakuwa ktk nafasi nzuri ku-save. Shughuli ni kati ya Emma na Elizabeth. Kumbuka nchi zinazompenda Elizabeth, zinampenda Emma pia.

Nawashauri Watanzania wapige kura nyingi kwa kujiweka ktk kundi la Rest of Africa, hii itasaidia kumwondoa Elizabeth ktk kura ya kukataliwa na RoA. Kuna uwezekano mkubwa akapona kupata kura hii ktk nchi hizi: Tanzania, Nigeria, Angola, Kenya, South Africa (kama wanakumbuka alivyom-save Liz) sasa tutafute na RoA.
 
......i agree with you. Bottom line its gonna be a tough one. Between Nkenna na Elizabeth mchuano ni mkali co they are both hated WITH PASSION hehehe!!! Its unfortunate but thats the game!!!!Watu wanadhani Eddy ni harmless na ni mjinga but i think ndio strategy yake....anajifanya kuwa full of pranks na nini ili housemates wasimchukulie serious especially wakati wa nominations but sadly next to Itai he is a cunning snake...switch yake ya jana inadhihirisha hivyo!!!!!He did not hesitate in putting up Eliza cos he has been planning/strategising ila ni mjanja..he does it on his own.....I wish Elizabeth good luck...iam voting for her (guess im being patriotic 🙂)
 

Mkuu ninakubaliana na wewe kwamba mfumo wa kuhesabu kura utampa advantage Nkenna. Mfano, Nkenna na Eliza wanaweza kupata kura ya Nigeria lakini Emma atakosa, na hivyo Nigeria itaonekana haimpendi Emma.

Same applies kwa Angola, Kenya na Tanzania, wote hao wanaweza ama kumpigia kura Eliza au Emma, na hivyo hizo nchi zote 3 zikawa hazimpendi Nkenna.

Kuna kosa limefanywa na wa-Nigeria ambao wameamua kumuunga mkono Kelvin kwa kuwa wanahisi kwamba Nkenna akipona, Kelvin atakuwa na wakati mgumu sana na hasa kwa kuwa anazidi kulishwa sumu mbaya na Itai. So Nigeria wameamua kumpa kura Eliza, lakini wako ambao watampa kura Nkenna kwa sababu ya uzawa.

South Africa wameamua kwenda kinyume wanatafuta support ili kumuokoa Nkenna and I can see South Africans supporting Nkenna.

Pamoja na hayo tuendelee ku-cross fingers labda dada yetu anaweza kupona, lakini kama nilivyosema ugomvi wa Kelvin na Nkenna unamuweka Nkenna kwenye advantage kwa kuwa viewers sasa hawamuoni kama m-Nigeria.

Kwenye mitandao, Nigerians wameishasema sana kwamba hawamtaki Nkenna, non-Nigerians wanamwita mtoto yatima ambaye amekuwa disowned na ndugu zake, so anaweza kupata kura za sympathy.

Zoezi zima linakuwa more complicated kwa kuwa kuna watu 3 na miongoni mwao wawili wanatoka kambi moja, hapo ndipo kasheshe ilipo. Dhambi ya kula mtu itawamaliza. Maana ni wao wenyewe walianzisha huo mfumo wa kupandisha Namibians/twins wote. Sasa ni zamu yao kupandishwa. Last week ilikuwa JEMMA vs Mzamo. Wiki hii Emma/Eliza vs Nkenna.
 
Nina swali jamani, hivi kuna replacement yoyote iliyowahi kuwa evicted???

Apart from Erastus, third week, Kelvin akiwa HoH alim-swap Phil wa Uganda na aliondoka. Ni ile week ambayo wasichana wengi walitaka Eddie na Erastus waondoke kwa kuwa wanaonekana wanachoongelea ni sex tu masaa yote. Kelvin alim-save Eddie, akampandisha Phil. Phil aliondoka na Erastus akapona.
 

Hiyo ndiyo siri ya mafanikio. Tatizo ni kwamba ukiwa kwenye frontline ku-strategize na ku-mobilize watu kum-nominate mshiriki fulani unajenga uadui ndani na nje ya jumba. Lakini kama unafanya maamuzi yako peke yako, inakusaidia sana kwa kuwa wenzako hawawezi kujua unafikiria nini.

Sometimes swala la ku-swap linahitaji sana kutafakari kwa kina ili uweze kujua faida na hasara za mabadiliko unayoyafanya na namna ya ku-deal nayo. Eliza kipindi kile ali-swap kwa maelekezo ya alliance ambazo haziangalii interest zako, bali za kwao. So wewe unae swap ndo unakuwa adui while waliokushawishi ufanye hivyo wanabaki salama.

Eddie alichofanya ilikuwa ni kulipa kisasi kwa niaba ya pacha wake.
 
Naona huu mchuano ni kali sana wana jamii.tunachotakiwa kufanya ni kupiga kura kwa wingi kama tz na rest of africa.nimeangalia poll muda mfupi anayeongoza kwa asilimia nyingi ni Nkenna AKIWA NA 36.2% ELIZA 33.1% NA EMMA 30.7%total votes ni 8107
 
....though i hate Eddy with a passion naona mambo yanamnyookea and he will still be around coz im imagining next head of house atakuwa mzamo hehehe.......and what u said is very true...ujanja ni kukaa kimya na kufanya vitu vyako diary room....personally i think this BB revolution is a flop especially walipoamua kuwaachia housemates uhuru wa kuform alliances etc....mi naona the whole game has now been overcome by politics n stuff mara unasikia nchi za SADC mara East Africa..frankly i think i enjoyed BB 1 and 2 (didnt watch 3 at all)..yaani kuna vitu negative ndani ya nyumba this time especially the kind of pranks that these guys are playing on each other...chukulia prank ya Eddy after Lionel pranked him....grrrrrrrrrrrrrrrr..i was so annoyed!!!What Eddy did was not even a prank it was malicious and he gets away with it.....
 
Naona huu mchuano ni kali sana wana jamii.tunachotakiwa kufanya ni kupiga kura kwa wingi kama tz na rest of africa.nimeangalia poll muda mfupi anayeongoza kwa asilimia nyingi ni Nkenna AKIWA NA 36.2% ELIZA 33.1% NA EMMA 30.7%total votes ni 8107

Ni kweli mchuano ni mkali sana na kwa sasa ni kama vile kuna tie kati ya Nkenna na Eliza, Eliza anaongoza kwa kura chache sana, less than 10. Emma ameachwa kwa gap la kura 1000 hivi.

Jana, Eliza alikuwa nyuma ya Nkenna kwa kura 300, Emma alikuwa nyuma ya Nkenna kwa kura 500. It seems that some voters are pulling out their support from Nkenna and Emma, or may be Eliza is getting more new supporters.

Lakini ikumbukwe kwamba kura hizi ni za mtandaoni tu, hazichangii kwenye kura zile zinazohesabiwa kwa ajili ya eviction.

Kwa muda mrefu kura hizi zimekuwa ziki-predict matokeo, kasoro eviction ya Paloma, ambapo aliongoza mpaka dakika ya mwisho na alifuatiwa na Eddie. Lakini Eddie akaja ku-save na Paloma alitoka kwa kuwa kuna nchi 2 ambazo hazikumpenda.

Hapa naomba nikumbushe kwamba Nigeria walikuwa wanamuunga mkono Paloma kwa kuwa alikuwa anampenda Kelvin, so kuendelea kuwepo ndani ya Jumba kungempa support zaidi Kelvin. Na pia kulikuwa na Namibians 3 ambao walikuwa up. Scenario hii inafanana sana na ya sasa hivi.

Kwa trend ya polls zinavyokwendaa hapo, wiki hii tunaweza kupata matokeo ambayo yanaweza kuwa kinyume na polls zinavyoonyesha. Hii inatokana na ku-split kura za nchi kama Nigeria na South Africa. Nina hakika kuna nchi nyingine nyingi tu ambazo zinawapenda Emma na Eliza na wao watajikuta wanagawa kura zao mara 2 na hiyo inampa advantage Nkenna.

Baadhi ya Nigerians wanataka Nkenna atoke kwa kuwa wanahisi ana chuki na Kelvin. Wanaotaka atoke, wanataka Eliza na Emma wabaki kwa kuwa wako kambi moja na Kelvin, so linapokuja swala la nominations wanaweza kuwa numbers na ku-control game.

South Africans wanamtetea Nkenna kwa kuwa wana uadui na Nigeria, sijui ulianzia wapi. South Africans wengine wanataka Nkenna atoke kwa kuwa ndani ya Jumba kuna Nigerians wengi, same feeling iko kwa nchi nyingine. But again Nkenna amegombana na Kelvin, so nchi nyingine wanaona kuendelea kumuweka Nkenna ni fair tu na kitendo cha Kelvin kum-nominate Nkenna wanakiona kwamba sasa Nigerians wanaweza kugeukana.

Kwa hiyo hizi kura zinaweza kutu-mislead na kuhisi kwamba labda Eliza yuko salama na kumbe anapata kura nyingi toka Nigeria, while nchi nyingine wanapiga zile zinazohesabiwa na wala hawapigi kura zao huko Oboma. Silent voters wako wengi tu na hasa wanaotumia simu zao za kiganjani.

Mfano last week, Mzamo alikuwa na 41.92%, Emma alikuwa na 38.38% na Jeremmy alikuwa na 19.70%. Pamoja na hilo gap dogo kati ya Mzamo na Emma, lakini wote walikuwa hawapendwi na nchi 3.

Kwa hiyo tusipoteze muda kuangalia sana hizo kura za huko Oboma, tu-focus kwenye kupiga kura ambazo zinahesabiwa. Ngoma ya wiki hii ni ngumu sana, tusipoikomalia tutampokea Eliza pale JKN International Airport katikati ya wiki ijayo! But wale wenye access ya kupiga kura Oboma, waendelee kupiga ili kuwa-scare supporters wa washiriki wengine na hivyo inaweza kuwavunja moyo kama wanaangalia hizo kura.
 
mimi leo nimeanza kukata tamaa kikwelikweli, Eddy kashinda HOH tena, dada yetu akipona wiki hii Eddy anaweza kumswap tena next week ili ahakikishe aliyemtoa twin wake ana pay the price....
 
mimi leo nimeanza kukata tamaa kikwelikweli, Eddy kashinda HOH tena, dada yetu akipona wiki hii Eddy anaweza kumswap tena next week ili ahakikishe aliyemtoa twin wake ana pay the price....

That was the biggest mistake ambayo ilifanywa na Eliza. Iwapo tu kum-swap rafiki/countryman wa housemate ni issue, je kum-swap twin wa mtu si ndio uhaini?

May be alitegemea wote wangetoka, lakini mmoja ali-save wiki ya 3, so ilikuwa ni dalili tosha kwamba hao jamaa wanapendwa na viewers, ingawaje housemates wa kike walikuwa wanawaona wana tabia za ajabu ajabu. May be hizo tabia za ajabu ajabu ndio ambazo ziliwafanya wapendwe zaidi na watazamaji, you never know.

Eddy sidhani kama target yake ni Elizabeth, target yake ni mpinzani wake mkuu ambaye ni Kelvin. Of course Eddy akifanikiwa kumtoa Eliza, atakuwa ameua ndege 3 kwa jiwe moja. Atakuwa amelipa kisasi cha twin wake; atakuwa amepunguza nguvu ya Kelvin kwenye alliance yake na inaweza kumsumbua kwa muda kabla hajaanza ku-cope na situation humo ndani na mwisho anapunguza nguvu ya alliance iliyokuwa inaonekana kuwa na nguvu sana.
 

Kama mambo yatanyoka yaani sunday aondoke Nkenna, basi alliance ya akina Eliza (yaani Elizabeth, Emma, Kevin, Leonel (wameshamdaka) wa-nominate Edward na Mzamo. Hii itampa taabu kidogo ku-swap zaidi atajiokoa yeye na kumwacha Mzamo. Nadhani nchi zisizo za sadc hazimpendi Mzamo pia Mozambique ataingia ili kumpatia nafasi Leo ya kumpata Geraldine. By the way game ni gumu sana na huenda jpili hii wakaondoka wawili. Kumbuka yamebaki majuma 3 ya kutoa watu kabla ya final.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…