Naona huu mchuano ni kali sana wana jamii.tunachotakiwa kufanya ni kupiga kura kwa wingi kama tz na rest of africa.nimeangalia poll muda mfupi anayeongoza kwa asilimia nyingi ni Nkenna AKIWA NA 36.2% ELIZA 33.1% NA EMMA 30.7%total votes ni 8107
Ni kweli mchuano ni mkali sana na kwa sasa ni kama vile kuna tie kati ya Nkenna na Eliza, Eliza anaongoza kwa kura chache sana, less than 10. Emma ameachwa kwa gap la kura 1000 hivi.
Jana, Eliza alikuwa nyuma ya Nkenna kwa kura 300, Emma alikuwa nyuma ya Nkenna kwa kura 500. It seems that some voters are pulling out their support from Nkenna and Emma, or may be Eliza is getting more new supporters.
Lakini ikumbukwe kwamba kura hizi ni za mtandaoni tu, hazichangii kwenye kura zile zinazohesabiwa kwa ajili ya eviction.
Kwa muda mrefu kura hizi zimekuwa ziki-predict matokeo, kasoro eviction ya Paloma, ambapo aliongoza mpaka dakika ya mwisho na alifuatiwa na Eddie. Lakini Eddie akaja ku-save na Paloma alitoka kwa kuwa kuna nchi 2 ambazo hazikumpenda.
Hapa naomba nikumbushe kwamba Nigeria walikuwa wanamuunga mkono Paloma kwa kuwa alikuwa anampenda Kelvin, so kuendelea kuwepo ndani ya Jumba kungempa support zaidi Kelvin. Na pia kulikuwa na Namibians 3 ambao walikuwa up. Scenario hii inafanana sana na ya sasa hivi.
Kwa trend ya polls zinavyokwendaa hapo, wiki hii
tunaweza kupata matokeo ambayo yanaweza kuwa kinyume na polls zinavyoonyesha. Hii inatokana na ku-split kura za nchi kama Nigeria na South Africa. Nina hakika kuna nchi nyingine nyingi tu ambazo zinawapenda Emma na Eliza na wao watajikuta wanagawa kura zao mara 2 na hiyo inampa advantage Nkenna.
Baadhi ya Nigerians wanataka Nkenna atoke kwa kuwa wanahisi ana chuki na Kelvin. Wanaotaka atoke, wanataka Eliza na Emma wabaki kwa kuwa wako kambi moja na Kelvin, so linapokuja swala la nominations wanaweza kuwa numbers na ku-control game.
South Africans wanamtetea Nkenna kwa kuwa wana uadui na Nigeria, sijui ulianzia wapi. South Africans wengine wanataka Nkenna atoke kwa kuwa ndani ya Jumba kuna Nigerians wengi, same feeling iko kwa nchi nyingine. But again Nkenna amegombana na Kelvin, so nchi nyingine wanaona kuendelea kumuweka Nkenna ni fair tu na kitendo cha Kelvin kum-nominate Nkenna wanakiona kwamba sasa Nigerians wanaweza kugeukana.
Kwa hiyo hizi kura zinaweza kutu-mislead na kuhisi kwamba labda Eliza yuko salama na kumbe anapata kura nyingi toka Nigeria, while nchi nyingine wanapiga zile zinazohesabiwa na wala hawapigi kura zao huko Oboma. Silent voters wako wengi tu na hasa wanaotumia simu zao za kiganjani.
Mfano last week, Mzamo alikuwa na 41.92%, Emma alikuwa na 38.38% na Jeremmy alikuwa na 19.70%. Pamoja na hilo gap dogo kati ya Mzamo na Emma, lakini wote walikuwa hawapendwi na nchi 3.
Kwa hiyo tusipoteze muda kuangalia sana hizo kura za huko Oboma, tu-focus kwenye kupiga kura ambazo zinahesabiwa. Ngoma ya wiki hii ni ngumu sana, tusipoikomalia tutampokea Eliza pale JKN International Airport katikati ya wiki ijayo! But wale wenye access ya kupiga kura Oboma, waendelee kupiga ili kuwa-scare supporters wa washiriki wengine na hivyo inaweza kuwavunja moyo kama wanaangalia hizo kura.