Sidhani kama Eddie amechemsha, move yake ya sasa wanataka Leonel aondoke ili kupunguza makali ya kambi ya upande wa pili (Emma/Kelvin/Leonel). Wakishamtoa Leonel, then the other side watabaki Kelvin na Emma tu. Itai hayuko mahali popote, ana hang. So in terms of numbers it will be 4 vs 2 kwenye nominations.
Eddie anaweza kutoka iwapo atasimama na Kelvin au Mzamo. Lakini housemates wengine wote sioni hata mmoja anayeweza kumtikisa. Chances za Eddie kusimama na hao watu sizioni kwa kuwa kambi ya Kelvin hawana numbers, wangekuwa na numbers wangeweza kum-nominate Eddie na mtu mwingine yoyote, then HoH akaenda ku-swap kwa kumuokoa huyo mwingine na kumpachika Mzamo.
Scenario pekee ya Eddie kusimama na Kelvin ni hii hapa. Kelvin awe HoH, then kambi ya Eddie wawa-nominate Kelvin na Emma, halafu Kelvin aamue kumuokoa Emma halafu ampandishe Eddie. HAWEZI kufanya hiyo swap, ina risk kubwa sana. Sana sana atajichomoa mwenyewe na kumpachika Eddie au Mzamo.
Kelvin akishinda HoH on Friday, basi Jumatatu nominations zitakuwa ni Kelvin na Emma. Emma akishinda HoH, basi nominations za Jumatatu zitakuwa ni Emma na Itai. Kambi ya Eddie hawawezi kum-nominate Kelvin wiki ijayo kwa sababu ya dada zake. Lakini dada zake watakubali kum-nominate iwapo atakuwa ame-win HoH na hivyo atajiokoa mwenyewe.