Mkuu Mbogela,
Hilo sio game ila ni ujinga, ninasikitika kutumia hilo neno kwa kuwa hiyo pair imepoteza umaarufu wao wote. Sasa hivi wako kwenye crisis, kila mmoja anajuta kwanini alipata balaa ya kuwa kwenye pair hiyo.
Wamepoteza focus ya game, Eliza kawa mkali bila sababu ya kueleweka, Kelvin anaona aibu na amebaki kuwa mtu wa kujibembeleza kwa Eliza masaa yote na mtoto hataki kuwa close na kajamaa basi ni kero tupu.
Dada yetu yuko too moody, huwezi kutabiri ata-respond vipi akiambiwa kitu chochote na housemate yeyote na ninahisi most of housemates wanam-avoid kwa sasa na ndio maana most of the time yuko mwenyewe peke yake ama wanagombana na Kelvin.
Oboma forum wamembatiza kwamba ni mshiriki ambaye ni mgonjwa kila kukicha na saa zote wanaulizia yuko wapi, maana haonekani/hasikiki.
Hii pair ilikuwa very strong lakini tangu wameanza huo ujinga wao, wamepoteza mashabiki kibao. Hata Nigerians ambao walikuwa wapiga debe wakuu wa Kevin nao wameanza kukata tamaa na wameanza kuhamishia nguvu kwa Geraldine, hivi kweli Geraldine nae ni mshiriki wa kulinganisha na washiriki wengine?
Kelvin alihisi kwamba Eliza anampenda, na alihisi angekubaliwa na hatimaye akatangaza kwenye diary session kwamba karibu ata-win. Baada ya Eliza kubadilisha kibao, naona Kelvin amepoteza game, kashikwa na aibu sasa saa zote anambembeleza Eliza.
Dada yetu nae hataki mchezo ni mkali kama pilipili, hataki hata kuguswa wala hataki mambo ya kufunikwa kana kwamba yeye mgonjwa.
Matokeo yake ndio hayo. Nimesikitika sana, maana wote wawili wameonyesha hawajakomaa. Kelvin hataki kukubali kushindwa, dada yangu nae hataki kuonyesha ukomavu wa majibu ya kistaarab ikitokea ametongozwa. Mbona karibu wasichana wote humo ndani wametongozwa na wamekataa na walitoa majibu kwa ustaarab bila hata kuonyesha kwamba wamechukia ama hawataki kuwa close na walio watongoza, na pia watongozaji nao walijikata kimya kimya wakakubali kushindwa. Sasa hao wote wamekutana hawajakomaa.