Big Brother Africa 2009: The Revolution

Big Brother Africa 2009: The Revolution

Ninahisi huyu mtoto ana matatizo ya maruhani ya hisia za mapenzi (huwa anasisimka kirahisi sana), kwanini huwa anaogopa kuguswa? Ukichunguza sehemu nyingi wanazogombana, chanzo kinaweza kuwa Kelvin kutaka kuongea na mtoto huku akiwa ana mshika mshika ama akiwa anamsogelea, kitu ambacho kwa marafiki wa opposite sex na kwenye jumba kama hilo ni cha kawaida sana, hata kama hakuna mahusiano ya kimapenzi. Kweli ukiwa kwenye hayo mazingira unaweza ku-avoid kuguswa completely na rafiki yako?

JEMMA wanasema ana "sexual tension" (whatever that phrase means), nahisi mtoto mambo yake huwa yako jirani sana na ndio maana anaogopa sana kuguswa guswa kwa kuwa anaweza kuanguka kirahisi sana.

Mkuu Keil nimekubali wewe ni mchambuzi wa hii reality show itabidi utafute kazi kwenye TV! hahaha yani yawezekana ni kweli tupu! Hii nafkiri ni defensive mechanism ya dada yetu maana anajijua ni dhaifu kwenye hiyo idara!
 
Jioni hii mida ya saa moja hivi, ameongea kwa hisia na kulia sana. Anadai anayosiri kubwa. Kuna kitu kimemtokea siku chache kabla hajaingia big brother. Anadai kitu hicho anajua kilivyofanyika (how) na muda (when) lakini hajui ni nani waliofanya (who), wapi (where) na kwa nini hajui.

Nimeanza kuhisi huenda alitekwa na kubakwa siku chache kabla ya kuiingia big brother. Ndiyo maana siku za mwanzoni Biggie alimpatia daktari. Hivyo, ameathirika kisaikolojia, plan zake na strategy za game zimevurugika na ndo maana anahasira siku zote.

Amemwambia Kevin kwamba akimwambia hiyo siri, Kevin atashindwa hata kumwangalia usoni. Kuna kubwa hapa, pole sana Elizabeth.

kwa kweli alivyokuwa anaelezea hata mimi machozi yamenitoka...poor kid!

labda ndio sababu hapendi kabisa kuguswa...
 
Keil nimekubaliana na wewe mkuu wangu. Nadhani niendelee kutoa support.

Jioni hii mida ya saa moja hivi, ameongea kwa hisia na kulia sana. Anadai anayosiri kubwa. Kuna kitu kimemtokea siku chache kabla hajaingia big brother. Anadai kitu hicho anajua kilivyofanyika (how) na muda (when) lakini hajui ni nani waliofanya (who), wapi (where) na kwa nini hajui.

Nimeanza kuhisi huenda alitekwa na kubakwa siku chache kabla ya kuiingia big brother. Ndiyo maana siku za mwanzoni Biggie alimpatia daktari. Hivyo, ameathirika kisaikolojia, plan zake na strategy za game zimevurugika na ndo maana anahasira siku zote.

Amemwambia Kevin kwamba akimwambia hiyo siri, Kevin atashindwa hata kumwangalia usoni. Kuna kubwa hapa, pole sana Elizabeth.

Duuuu basi kuna issue hata kama sio Kubwakwa lakini inawezekana ni jambo ambalo limemuathiri kabisa kipsycholojia. Unaweza ukaona ni issue zake na huyo mpz wake lakini pia. Nadhani tunaweza kujifunza kitu kikubwa sana kwa huyu mtoto. Nimeshakata tamaa kuwa huu ni mwaka wetu tena nadhani tusubiri mwakani, Keil tuanze kujipanga kuandaa mtu wa mwakani mkuu wangu, hauna madogo wanaojiweza lugha wapigwe msasa kama m-net watakuwa fair basi tupeleke mtu anayeelewa anaenda kufanya nini? Mbona tumesoma na wadada sekondari mpaka vyuo vikuu hawajamegwa hata siku moja lakini hawajawahi kuwa na bifu na mtu? na walikuwa very popular na kupendeka na kila mtu???
 
Nimekupata vizuri sana mkuu Keil, kwa kusema ukweli Elizabeth si entertainer kabisa. Housemates wote wameshamchoka vibaya. Jana akina Leonel, Itai, Nkenna na Geraldine walikuwa wanajadili kwamba Elizabeth ame-survive nominations zilizopita kwasababu ya Kevin. Sababu yao ni kwamba Eliza si intertainer hivyo wapiga kura wasingempa kura. Baada ya kuendelea kugombana na Kevin, Jeremy na Emma pia wakawa wanajadiliana juu yake na wakasema anachukizwa na Kevin. Elizabeth mwenyewe akamwambia Kevin kwamba watu wanamuona psycho.

Hali ilivyo hakuna housemate aliyetayari kuwa karibu na Elizabeth kutokana na tabia yake ya ugomvi na chuki. Kevin akiamua kumtosa basi atabaki hana mtu wa karibu. Kwa hali ilivyo ni dhahiri gemu limemshinda na limekuwa mzigo kwake na wiki ijayo anarudi Dar.

Elizabeth ameshajanga uadui mkubwa na Mzamo, Leonel, Itai, Eddie na Nkenna. Endapo Emma na Jeremy wataondoka jpili itakuwa mbaya zaidi kwake. Binafsi nime-give up na sitampigia kura tena, msaada ninaoweza kuutoa ni kusaidia arudi nyumbani haraka.
...........giving up now is good!!!!it's a pity kwamba Tanzania tulivyo na watu wakarimu na wasio na chuki tumepata bad luck ya kuwa represented na Elizabeth mwaka huu. So far the women who have gone in the house have dissapointed us...if it was up to me i would in future send a male rep....Another thing with Elizabeth nadhani hayuko ambitious sana....she did not go into that house with the urge to really WIN!!!!iko siku i was listening to her talking to Kevin and saying how the money pot is gonna help her sijui buy a car etc......si mawazo mabaya but what happened to fighting for more? yaani mi nilipomsikia anaongea you could see hana fighting spirit...for her just being able to participate in the house, sharing the stage with Keri Hislon and now being among the remaining ten is an achievment enough(can you imagine??)....Tz lets help her come home to her family...kama alivyosema Mbogela or Nemesis im not sure tujipange mwakani we send in a good candidate!! If anyone knows someone who fits the criteria plz let them audition nxt year......Swali la kizushi.....hivi hapa bongo esp Dar kuna BB Fan club? if it's there plz let me know coz i'd like to hook up
 
Mkuu Kelelee,

Ninakubaliana na hoja zako, lakini naomba usije ukawahukumu sana akina dada kwamba wanashindwa kutuwakilisha. Nina amini yaliyojitokeza kwa LaToya na Eliza ni weaknesses za mtu binafsi.

So far the women who have gone in the house have dissapointed us...if it was up to me i would in future send a male rep....

LaToya alikosea step japo alijitetea kinyume. Kilichowakera viewers ni pale alipomtosa Morris na kwenda kwa Ricco, hilo ndio lilikuwa kosa lake kubwa sana. Viewers wengi wanapenda mwanamke aliye-consistent, kwamba stick to your man. LaToya aliingia kwa Morris haraka kabla hajagundua kwamba hakuwa anamfaa, kama angetumia two weeks akichunguza awe na yupi kati ya wanaume wote wale, angeweza kukaa humo ndani kwa muda mrefu sana na esp kama angeweza kubaki na Ricco.

Yeye alijitetea kwamba alitaka kuona drama jinsi wanaume wanavyogombana kwa ajili yake. Lakini that drama ilim-cost kwa kuwa evicted.

Another thing with Elizabeth nadhani hayuko ambitious sana....she did not go into that house with the urge to really WIN!!!! iko siku i was listening to her talking to Kevin and saying how the money pot is gonna help her sijui buy a car etc......si mawazo mabaya but what happened to fighting for more? yaani mi nilipomsikia anaongea you could see hana fighting spirit...for her just being able to participate in the house, sharing the stage with Keri Hislon and now being among the remaining ten is an achievment enough(can you imagine??)....

This has a lot to do with her background, ndio maana hata thinking yake imekuwa affected kwa kiasi kikubwa. Hela anazoongelea zinaongezeka on weekly basis, yeye anatakiwa ku-aim higher (prize) na siyo kwenye hizo hela ambazo kwa jinsi anavyoongelea habari ya ada yake ya shule na wadogo zake bado haziwezi kununua gari na kulipia msululu wa vitu anavyotaka kufanyia hizo hela. Akipata Bingo ya $ 200,000 inaweza kumsaidia sana na anaweza ku-kiss goodbye umasikini as long as atazitumia wisely.
 
Mkuu Keil nimekubali wewe ni mchambuzi wa hii reality show itabidi utafute kazi kwenye TV! hahaha yani yawezekana ni kweli tupu! Hii nafkiri ni defensive mechanism ya dada yetu maana anajijua ni dhaifu kwenye hiyo idara!

Akina Dr. Liki (yule mchambuzi mahiri wa mpira wa miguu) tuko wengi, lakini ukituuweka humo ndani ya jumba tunaweza kutolewa wiki ya kwanza tu. Tunachangia kulingana na jinsi tunavyoona mwelekeo wa game linavyokwenda.
 
mwakani M-net waweke jin wazi la mtu anayeenda na waombe msaada wa coaching, nadhani Mkuu tukimpa msasa wa wiki 2 na kumuweka ndani na notice na malelekozo akaangalia clips zote wapi watu walipga bao wapi watu walimess up anaweza akafika mbali kimtindo. Kwa Mfano Paloma naamini kabisa alikuwa amekula desa la Cherrishe maana alitaka ku-copy and paste style ya cherrishe lakini alichemsha kuwa cherrish pamoja na kuwa alijituma sana jikoni na kushika dini pia alikuwa hana bifu na mtu na hakuwa mtu wa mastrategies, alikuwa ameacha game lichukue mkondo wake. Shida ni kuwa kumwambia mtu tu kama alikuwa hafuatilii hili game angalau masaa 2 kwa siku hapo itakuwa sawa na kutwanga maji kwenye kinu. Elizabeth alichokuwa anajua ni kuogopa kuwa LaToya akasahau kuwa sio Latoya tu amecheza hili game, angeona wengine alichezaje, kama Tapiwa (Zim, BBA I) au yule dada wa Malawi (BBA III). Lakini amejitahidi huyu mnaijeria asingekuwa king'ang'anizi angefika mbali sana.
 
Je, Elizabeth anapo-claim kwamba wao ni masikini, kuna ukweli wowote?

KILIMANJARO-SERENGETI TOURS & TRAVELS LTD, is a limited Company with share holders.
The Company has been dealing with Tourism Industry since 1993 when she was registered officially.
The main office is located in Tanzania, Kilimanjaro Region, Moshi town, in the Old CCM Building, just a few steps from the main Bus station.
A person can reach easily from Tanzania Tellecoms Office, next to Kilimanjaro Cooperative Bank.

Directors:

Ms Hellen Gupta

Mr Tumaini David

Ms Elizabeth Gupta (Queen)

Mr Kristolumba Gupta

Mr David Gupta

Mr Zakaria Gupta.

Staff:

* Managing Director - Ms Hellen Gupta.

* Lawyer of the Company - Advocate Njau.

* Head of Finance Department – (Holder of CPA), Mr Stanley Nsebo.

* Chief Mountain Guide - Mr Mark Urio

* Chief Driver/Guide - Mr Clemence Mollel

* Sales & Marketing Officer - Mr Tumaini David

* IT expert - Mr Tumaini David

Bankers : -CRDB

Membership:

• Tanzania Chamber of Commerce, Industry & Agriculture.
• Kilimanjaro Association of Tour Operators.
Home Contact us Copyright © 2006 KILIMANJARO-SERENGETI TOURS & TRAVELS LTD
Best viewed in IE6,Firefox 1.0.6, Opera 8.5.
Last modified 17 may 2006

Source: http://www.kilimanjaroserengeti.com/about.htm

Hizo bold zinaonyesha hii ni kampuni ya familia na Elizabeth mwenyewe ni mmoja wa Directors. The rest of Directors wanaonekana ni family members (nucleus family) with exception of one Tumain David.

Je, kweli anatokea kwenye familia masikini?

Je, Kampuni hiyo bado ipo na inafanya kazi? Info za kwenye mtandao zilikuwa updated mara ya mwisho May 2006.

Anyway, labda walikuwa nazo then wakafilisika baada ya baba kufa, maana Eliza mwenyewe amekuwa akisema maisha ya familia yalikuwa magumu baada ya baba yake kufariki.

Ama kulia lia ni strategy ya kupata kura za huruma kutoka kwa watazamaji?
 
Jeremy ndo katolewa

Hahaaaa, sasa ndio picha linaanza!!! Alliances zinajiform upya, na Eliza sasa ataanza kupata challenge kwenye partners!!! Lazma atavua very soon kwasababu ya competition
 
Hahaaaa, sasa ndio picha linaanza!!! Alliances zinajiform upya, na Eliza sasa ataanza kupata challenge kwenye partners!!! Lazma atavua very soon kwasababu ya competition

sijajua kura ya Tanzania ilienda wapi? kama tulimnyima Jeremy hiyo ni disaster, Kenya hawatatu-support. Bila shaka ktk nomination za kesho, Elizabeth atakuwemo kwenye list. Kama atapona basi Eddie atamswap.

Itakuwa vema kama lobbying ya Emma itazaa matunda yaani Leonel na Itai watawaunga mkono kwa kumnominate Mnaigeria mmoja wapo hasa Nnkena au Geradine. Mpaka hapa wa9ja wenyewe including Kevin wanaona aibu na vibaya kuwa na wawakilishi watatu. Kwakuwa wana9ja wanampenda Kevin, watapiga kura kumwondoa mdada mmoja.

Elizabeth na Emma, wanapaswa kufanya kazi kubwa kuwashawishi Itai na Leonel wajiunge na alliance yao ili wawe 5 including Kevin. Otherwise wamekwisha.
 
Yaani jinsi mda unavyoenda ndio eviction inazidi kumsogelea Eliza, i think she needs to start a "player" game now!!!
 
Jeremy is out, Mzamo and Emma have survived eviction.

Mzamo hakupendwa na nchi hizi: Kenya, Angola na Tanzania.

Emma hakupendwa na nchi hizi: Uganda, Ethiopia na South Africa.

Jeremy hakupendwa na nchi hizi: Zimbabwe, Ghana, Malawi, Mozambique, Zambia, Nigeria, Rest of Africa, Namibia na Botswana!

Ukiangalia kura za Mzamo na Emma zimekaa very strategically. Kenya, Angola na Tanzania walitaka Mzamo atoke kwa kuwa sababu ya JEMMA. Elizabeth ni memba wa alliance ya akina Emma. So Mkuu Nemesis kazi yako tumeiona na watu walimnyima kura Mzamo kama ulivyopendekeza.

Emma alinyimwa kura na Uganda, Ethiopia na South Africa, sababu ziko wazi. Emma alishiriki kuwa-nominate Hannington na Yacob. Pia Emma alishiriki kulipiza kisasi kwa Quinn pale alipoomba alliance yao wam-nominate.

Kilichomponza Jeremy hayuko active na alikuwa kwenye alliance iliyo kwenye target na imesababisha majeruhi wengi sana kwenye evictions zilizopita, na hivyo ni kama vile watu wanalipa kisasi.

Sasa tusubiri nominations za kesho ambazo zitategemea sana strategies za usiku huu, japo ninapata mashaka kwamba kura za kesho kila mtu anaweza kuingia kivyake.
 
sijajua kura ya Tanzania ilienda wapi? kama tulimnyima Jeremy hiyo ni disaster, Kenya hawatatu-support. Bila shaka ktk nomination za kesho, Elizabeth atakuwemo kwenye list. Kama atapona basi Eddie atamswap.

Itakuwa vema kama lobbying ya Emma itazaa matunda yaani Leonel na Itai watawaunga mkono kwa kumnominate Mnaigeria mmoja wapo hasa Nnkena au Geradine. Mpaka hapa wa9ja wenyewe including Kevin wanaona aibu na vibaya kuwa na wawakilishi watatu. Kwakuwa wana9ja wanampenda Kevin, watapiga kura kumwondoa mdada mmoja.

Elizabeth na Emma, wanapaswa kufanya kazi kubwa kuwashawishi Itai na Leonel wajiunge na alliance yao ili wawe 5 including Kevin. Otherwise wamekwisha.

Wakenya wasipotuunga mkono basi watakuwa na lao jambo. Uganda tusitegemee kura yao hata siku moja. Pattern ya kura imenishitua sana na ninapata mashaka makubwa sana.

Mkuu kuhusu prediction ya nominations, uko sahihi kwa kiasi kikubwa na mimi ninakuunga mkono kwamba leo Eliza anaweza kuwa nominated na asipokuwa nominated basi kuna uwezekano Eddie akamuweka kwa kuwa Eddie ana wabaya 2 humo ndani, Itai na Eliza.

Eliza, anaweza kuwa nominated na wafuatao: Nkenna, Mzamo, Geraldine na Eddie. Pia Itai anaweza kum-nominate japo haeleweki sana na ni nyoka flani ndani ya Jumba. Kwenye kundi hili pia second nominee wao anaweza kuwa Emma, japo timing inaweza kuwa mbaya kwa kuwa anaweza kuokolewa na Eddie.

Mtu mwingine ambaye ninaona yuko kwenye target ni Nkenna, atakuwa nominated na Emma, Leonel na Eliza. Kelvin na Itai waliombwa kura lakini sioni dalili za wao kum-nominate Nkenna kwa kuwa ni kosa linaloweza kuwapunguzia kura za nje, na hakuna ambaye yuko tayari kwa hilo. Nina mashaka sana Nigerians wanaweza kupona tena leo. Nkenna ambaye ni target namuona yuko makini kujenga majeshi ya kuwamaliza Emma na Eliza. Akifanikiwa hilo basi atakuwa kapona na sioni kama Eddie anaweza kumpandisha while Itai yupo.

Kwa hiyo matarajio ni nominees 3, Eliza, Nkenna na Emma. Ngoja tusubiri nominations asubuhi hii. Hizi ni dakika za majeruhi, watu wanaweza kukuunga mkono ukiwa nje na akiingia diary room anabadilisha mawazo, na inabaki kuwa siri yake.
 
Today's Nominations:

Eddie: Eliza + Emma
Nkenna: Eddie + Emma
Eliza: Mzamo + Nkenna
Leonel: Mzamo + Nkenna
Mzamo: Eliza + Emma
Itai: Emma + Mzamo
Geraldine: Eddie + Mzamo
Emma: Mzamo + Nkenna
Kelvin: Mzamo + Nkenna

Preliminary Results:

Mzamo - 6
Nkenna - 4
Emma - 4

Imekula kwetu ... sina imani sana na Eddie. Nominations zake za asubuhi hazitoi ishara nzuri hata kidogo, japo ana wabaya wawili, Itai na Eliza. Kuna dalili kubwa anaweza kumpandisha Eliza ili kuisambaratisha kabisa Girl Power.

Leonel kajipalia makaa, amejijengea image mbaya sana kwa kum-nominate mwanamke ambaye amefanya nae mambo makubwa wakati ndani ya Jumba kuna washiriki 9.

Kelvin kajichongea kwa wa-Nigeria wenzake, na inaweza kum-cost siku akija kusimama na strong contender kama Eddie.
 
Keil hii inatia mashaka hehehe......the game is getting tough!!!!! my bet is that Eddie will replace Emma with either Elizabeth or Kevin.....naegemea sana kwa Kevin nadhani Eddie feels Kevin is strong anaweza akataka kumtoa. Kevin kumchagua Nkenna was kind of inevitable nadhani ali sense and correctly so kwamba Nkenna does not want him in the house either.....she cannot be trusted. Ofcourse it will cost him na sasa tunataka kuona Nigeria itasema nini i remember sometime back when Keliz was up for eviction alot of the Nigerians were begging for people to save Kevin and they promised that should Keliz survive they will return the favour by sacrificing Nkenna sijui kama watalikumbuka hili since inavyoonyesha wameanza kugawanyika with Nkenna getting more support than before....Mh..hili game tough. If Elizabeth is put up......sidhani kama atapona...i gat the feeling people would rather have Nkenna and Mzamo than the "unpredictable and always throwing tantrums Elizabeth"
 
Hivi how come nchi nyingine zina ma-presenter wengi? an zingine zina mmoja tuu?...just curious...me i thought kila nchi inakuwa na presenter mmoja tuu?...
 
Duh! nimekubali Emma ni strategist, yaani ameweza kumshawishi Leonel ampandishe Nnkena kizimbani? tena ameweza kumshawishi Kevin kumnominate dadayake? Emma ni kichwa. Nadhani kutokuwemo kwa Elizabeth ktk nomination za leo ni kazi kubwa ya Emma hasa kumshawishi Leo.

Ninamheshimu sana Itai. Tangu sasa ninavutwa kumpenda huyu jamaa. Aliniudhi sana alipomswap Eliza kipindi kile, lakini nadhani alikuwa anamtaka Kevin. Kwa namna ambavyo Eliza alimwakia last week, ilitegemewa kabisa, atamnominate lakini wala.

Kimsingi ninaungana na Kevin, jamaa ni mwananume kweli. Eliza alimwambia Kevin kuwa Nnkena hampendi. Sasa kama dada hampendi wifi si inabidi aondoke nyumbani? Pia Kevin amerealize kwamba siku atakapowekwa Mnaigeria itakuwa rahisi sana kuondoka hivyo ni suala la ujanja kuwahi.

Eddie asipomuweka Eliza itakuwa safi sana. Lakini ndo aliyemnominate leo, hivyo anaweza kumwokoa Mzamo na kumwingiza either Elizabeth au Itai au Kevin. Itakuwa vema Africa ikimwondoa Nnkena.
 
Back
Top Bottom