Date::11/12/2009
Mshiriki wa Big Brother adai Watanzania wamemwangusha
Anadhidi kutuudhi huyu, anajua amatuingiza hasara kiasi gani lakini?
Na Vicky Kimaro
MSHIRIKI wa Big Brother Revolution, Elizabeth Gupta amewalawahumu Watanzania kwa kushindwa kumpigia kura za kumbakiza ndani ya jumba hilo ambalo mshindi atajinyakulia kitita cha dola 200,000.
Watanzania wengi nikiwemo mimi tunamlaumu Elizabeth kwa kutuzimishia ndoto yetu ya huu mwaka wetu pia wa kulamba bingo na kuibadili kuwa huu mwaka wetu wa kuaibika tena!
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Elizabeth alisema kuwa nchi tano zilimpigia kura, lakini Tanzania ilimuangusha kwa vile mashindano hayo wanaangalia zaidi kura zinazopigwa nchini mwako.
Atasemaje tulimwangusha wakati TZ ni miongoni mwa nchi zilizompigia kura? Hivi hajui watanzania sio wanafiki? Angeona kura alizopata Latoya angajua kuwa watanzania sio wanafiki. Pili alipata kura nyingi sana za wanigeria lakini hazijasaidia. Sikio la Kufa halisikii dawa, au Kunguru hafugiki dada yetu
"
Uganda, Kenya walinipigia, lakini Tanzania kura zilikuwa chache, .
Hata kama kura zingekuwa nyingi bado kama nchi zilizomkataa zinazidi zile zilizo mkubali angetoka tu. Pia lazima ajue kuwa kwa wateja wa DSTV africa, nchi yetu inawateja wachache sana ukilinganisha na nchi kama Bots, SA, Namibia, Zim na Nigeria, watu wanapiga kura kufuatana na kufuatilia mchezo, watu hawauoni mchezo watapigaje kura?
halafu mashindano ya mwaka huu ni magumu tofauti na miaka mitatu iliyopita, safari hii washiriki ni 25 sheria zimebadilika.
Sio kweli mashindano ya mwaka huu yalikuwa ni rahisi kuliko ya miaka mingine, 1. washiriki wa mwaka huu hawakuwa wanatofautiana sana back ground ukiondoa K1 kwa hiyo ilikuwa rahisi kujua mtu anataka kufanya nini na fanye nini 2. Waliruhusiwa kufanya alliance na ku-consipire jambo ambalo unajua kabisa move inandaje.
3. Alichokosea dada yetu kwenye hili ni kutokuwa na kichwa chake mwenyewe, Hata siku moja Liz hajafanya nomination kutokana na utashi wake siku zote alitegemea mawazo ya watu, hata kumswap Erastos lilikuwa kosa la kiufundi (kwanza alishajua kuwa mapacha ni strong condenders wanawashabiki wengi nje) alitakiwa kucheza na wapiga kura sio mahouse mate
Elizabeth aliongeza hakuwa na uhusiano na mshiriki mwenzake Kelvin wa Nigeria na kudai kuwa urafiki wao utabaki kuwa wa kawaida na si vinginevyo..
Ana mpenda sana Kelvin kinachomsumbua ni utoto na ubaguzi wake wa rangi. Shida yake (km kweli) anaamini kuwa watu weusi sio waaminifu na pia ni masikini na hii itampa shida sana, kwa hili amepunguza heshima yake aliyokuwa ajijengee kwenye jamii ya watanzania, alitakiwa kujua idadi ya watanzania weusi ni wangapi na waafrica weusi ni wangapi kabla hajaropoka, uetetezi wake kuwa amekulia kwenye mazingira ya weupe na kusoma nao haujitoshelezi bado. Sisi wengine hatujawahi kuishi na watu weupe, na tumesoma vijijini, hatujawahi kuwaona akina dada wanaoweka Dawa kichwani wala kuweka vipini kwenye ulimi (siipendi tabia hii) lakini siwezi hata siku moja nipo kwenye hadhara (nationa TV) kusema kuwa sitadate mweupe (wakati simjui) au waweka dawa wote na wavaa vipini ni malaya. Hapo unakuwa ni ushamba wangu na sio kulaumu mazingira niliyokulia. Dunia ya leo huwezi ukaa kwa watu wanao elewa ukaanza kucondemn mashoga (kwa mfano) au machangudoa, au watu watakuona huna data, lazima uone dunia inaendaje, sasa hivi kuna movement kubwa ya kudai haki kwa makundi mabli mbali ya kijamii, na yanaungwa mkono sio tu na watu wa jamii hiyo, lakini watu wengine wanaona duniani hapa kila mtu ana haki ya kuheshimiwa na kuthaminiwa utu wake, sio rangi, kabila, wala elimu aua sexuality ya mtu ndiyo inayompa heshima, bali utu wake. Na watanzania tunalijua sana hili, Binadamu wote ni sawa,
Eliza alisema "Kuishi na watu kazi sana kila mtu ana tabia zake, ukizingatia hakuna mawasiliano mimi sikuwa naigiza ndio tabia yangu ilivyo, lakini wapo ambao wanaigiza ingawa wote lengo letu ni kusaka fedha...
Nakubaliana naye kuishi na watu ni kazi hili sipingi, lakini kuishi na watu kunahitaji akili Je alitumia akili?
SIjamuelewa anaposema kulikuwa hakuna mawasiliano, anamaanisha nini? hakuna mawasiliano na dunia ya nje? lakini aliingia akijua fika kuwa hakutakuwa na mawasiliano na dunia ya nje.
Kwenye huu mchezo lazima kuwe na strategy, kila mtu anapohojiwa husema siigizi lakini ili uweze kuwa mshindi ni lazima uwe na uigizaji fulani ndani yake. Kwa mfano Gaitano (BBA I) alikuwa na nafasi nzuri sana ya kuwini lakini kwasababu ya umri alikuwa mara nyingi anajaribu kuweka busara mbele hivyo akachemsha, Mwisho mwampamba alileta mtafaruku sana alipovuta majani ya chai baada ya kuona sigalla zimeisha ndani (sio kwamba alikaukiwa kiasi hicho, hapo aliigiza) Usiku mwingine waliiba bia na kuzificha, pia waliwahi kuiba sigalla, sio kuwa walikuwa wanatabia hiyo lakini walijua kuwa viewers wanawaona na BB anawaona lakini walaitaka kuleta msisimko kwenye mchezo, Bahati mbaya mawasialiano ya lugha hayakuwa mazuri sana aliishia kushika namba 2. Ukiiangalia Kelvin na Edward kunauigizaji wa hali ya juu sana, sina uhakika Mzamo kama ile kujinafsi ni kawaida yake nahisi ameongeza mno kwa hiyo alitakiwa kubadirika kadiri mchezo unavyoenda na character wanavyotoka
Akizungumzia minong'ono inayodaiwa kuwa yeye ni mjamzito au kabakwa alisema "ni kitu kinachoniuzunisha sana uwa kinaniliza kwa kuwa sikupata muda wa kusikilizwa, ingawa mimi nilisikiliza: ...
mmmh hii sentensi tata. Lakini jinsi alivyoonekana wiki hii anavyofika afya yake inatatanisha sana, amepungua sana (sijui labda macho yangu tu) Lakini mimi sidhani kama ni jambo lilimtokea juzi juzi, mbona alikuwa mwenye amani wiki ya kwanza na ya 2? Mimi nadhani Elizabeth ana shida ya kimalezi kama alivyosema mwenyewe shule alizosoma, watu aliokuwa nao. Alipofika kule ndani alipata mshtuko wa kisaikolojia kwani ahkuzoea kufanya kazi ngumu za mikono kwa muda mrefu, hakuzoea kula na wenzake (mtoto wa kudeka deka) hakuzoea kuunda hoja na kuitetea, inawezekana ana nafasi ya kutoa amri kwenye familia. Sasa baada ya kukumbana na vikwazo kuishi kama alivyozoea kwao ili-react kwa kununa na kuwa makali kama mbogo aliyejeruhiwa. Baadaye aliwapoteza marafiki wote. Lakini ana akili sana, aliigundua hilo na ndio maana hata comrade in arm ilipoisha hakutaka kumpoteza Kelvin maana alijua maisha yatakuwa so boring, alichokosea alitakiwa kuwarudisha wenzie haraka sana. Anahitaji ushauri wa wataalam wa masuala ya kisaikolojia, lakini ni vema akamwambia mtu hilo tatizo lake maana likiwa la kudumu litamuumiza hata kumuua kabisa
"Kubakwa si siri ila ni kitu kibaya kinauzunisha, na mimba pia si siri kwani uwezi kuifika kwa sababu itakuja kuonekana, nilitaka niiseme siri inayoniumiza nikiwa BBA nikijua watazamaji watanisikia, lakini sikuweza kusema, kwa sasa bado iache iwe siri ipo siku nikijisikia kusema nitaisema
. Yeah kubakwa ni jambo zito sana, na mimba sio issue kubwa kama upo tayari, alikuwa SA ambako arbotion ni legal angeweza kuitupa kama hataki mtoto, lakini pia arbotion nayo ingem-haunt maisha yake yote. sasa kama sio kubakwa wala mimba ni nini? nadhani ni vizuri awaambie watanzania nini hicho kimskitishacho kwani tutaendelea kumpakazia kila siku jambo ambalo halifai.
Sidhani kama watanzamaji hatukumpa nafasi ya kusikilizwa, yeye hakutaka kuisema.
Asante sana kwa kutupasha
Watu wengi tunavyosema sana makosa ya Elizabeth wanadhani kuwa tunamchukia, kwa ujumla binafsi nampenda sana huyu mtoto, nimemsuport kupita kiasi huko Obama Forum na forum zingine, na ni matumaini yangu siku moja nikipata nauli nitakuja mjini nipige naye picha. Elizabeth nakukukaribisha Makete, Umetuwakilisha lakini ungeweza kufanya vizuri zaidi, maisha ndivyo yalivyo, mlango mmoja ukifunga mwingine hufunguka. Una nafasi kubwa sasa ya kutengeneza maisha, ni wewe tu kuamua uwe nani na utengeneze maisha hadi wapi. kile ulichouwa kuwa unakikosa sasa hivi utakipa, hujapa hizo dola lakini utapata pesa taratibu, TULIA!