Big results now

Big results now

Kwa nilivyoielewa mimi big results si kwa elimu tu ni mpango wa dhaifu kwa wizara 5 elimu, afya, kilimo, miundo mbimu na ya 5 nimeghafilika kuikumbuka. Kwamba kila wizara tajwa inatakiwa kupandisha malengo yake ya utendaji na kufikia ufanisi wa hali ya juu wa 60 percent kwa mwaka huu na kuendelea. Haiusiani na kuongezwa mshahara. Sbb mshahara kuongezeka ni kwa watumishi wote si walimu tu.

Sasa basi ufanisi katika elimu unaonekana katika ufaulu wa wanafunzi that is obvious, na kwa wizara nyinngine pia inategemea nini kinapima ufanisi huo kuonekana umekuwa kwa percent hiyo.

Turudi kwenye elimu...wameweka mikakati mingi sana sna kwenye hiyo kauli mbiu yao..walichokosea hawakuwashirikisha wadau wa 3 muhimu sana katika malengo yao hayo mzazi, mwalimu na mwanafunzi kwa mapana yake na marefu yake.

Pili mazingira ya kuifanya hiyo big results ni yale yale. Mishahara duni kwa walimu, mazingira magumu ya kufundishia na yakusomea, vikwazo vya kisiasa katika taaluma hasa kwa hawa madiwani na watendaji kata, gap kubwa ya kielimu kati ya watoto wa viongozi, walionacho na wasio nacho. kutokuwa na usawa katika kutahini watoto...i mean wale waliofundishwa katika mazingira mazuri sna na kuwa na walimu wa masomo yoote na facilities zote wanatahiniwa sawa na wale walio katika mazingira dunii ya kusomea bila walimu wala vitendea kazi.

Na madhaifu mengine meengi one can help kuyaorodhesha

Walikuw na malengo mazuri but wamechelewa sana and they DID NOT THINK BIG at ALL.

hii serikali wanatufanya walimu kama punda kututwisha mzigo mzito husio bebeka sijui walimu wanatuonaje.
 
Dharau wanayoionesha serikali ya ccm sasa imetosha. They are now stepping on a dog, just wait for the outcome. Wapo walioongezwa 6% ya basic salary. Hiyo wanayosema big results now labda iwe kinyume chake. Huwezi kuwa na matokeo makubwa kwa aina ya wanafunzi walewale wenye below average, the same few resources, mazingira magumu ya kazi na sasa wameongeza hasira kwa walimu kwa kuwaongeza this god damed increment. Give us a break! We are not working on filthy slogans. Kwa kuwa serikali haisikii action speaks louder than words. Wananchi wenye watoto wao watawasamehe walimu kwa kitakachotokea.

kwanza ukiangalia mazingira mabovu ya kufundia vifaa duni,maabara azijitoshelezi sijui serikali inafikiriaje hapo.
 
mbona umeongezewa % kubwa mkuu!!mm nimeongezewa 10% lkn me sio mwalim,so walim mmependelewa!!

Tofauti na kupandishiwa mshahara serikali inabidi watoe motivation lakini sio kwa hili, walitangaza walimu mishahara juu na mategemeo yake yanakuwa tofauti.
 
Mkuu umeongea point, ni kweli waalimu wanahitaji kulipwa vizuri lakini matokeo hayawezi kubadilika kwa haraka hivyo.

Ninafanya Teaching Practice mahali fulani, kwa kweli ni majanga. Watoto wana msingi mbaya sana, watoto wamejengeka katika misingi ya kuchukia baadhi ya masomo (mf. Maths) na hawajitumi kabisa.

Mishahara ya waalimu haiwezi kujenga maabara na maktaba, sasa hawa wanafunzi watafaulu vipi? Serikali itafakari vizuri.

kweli mkuu.
 
Hivi wakuu kuna kauli moja imetolewa kwa walimu kuhusu big results walimu wanatakiwa kufahulisha wanafunzi katika kiwango cha asilimia 60 % kwa fomu 2 na four 4 kutokana na kupandishiwa mshahara mnaonaje suala hili walimu uwanja wenu tililikeni .
BIG RESULTS NOW with such SMALL SALARY INCREMENT NOW is equal to BIG FAILURE NOW!!!! The CCM Government has failed completely!!!
 
BIG RESULTS NOW with such SMALL SALARY INCREMENT NOW is equal to BIG FAILURE NOW!!!! The CCM Government has failed completely!!!

serikali wanatakiwa waunde kamati kwa kuwachunguza hawa wanaounda sera kama hizi .
 
Back
Top Bottom