Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi
Hii ni makala yangu kwenye gazeti la NIPASHE la leo 1/09/2024
Kama kawa kila nipatapo fursa huja na makala zangu elimishi za Kwa Maslahi ya Taifa ambazo huwa na swali, hoja kisha jibu utatoa wewe mwenyewe.
Mada ya leo ni pongezi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kuwatumia wahariri wa habari wa TEF na vyombo
vya habari, the media kuelimisha umma eimu ya kodi na umuhimu wa kodi kila mtu alipe kodi. Swali ni je wajua kuna baadhi ya viongozi wetu wakuu hawalipi kodi?. Viongozi hao hawalipi kodi kwasababu wamekuwa exempted kulipa kodi kwa mujibu wa sheria. Tunaposema kila mtu alipe kodi, kwanini wengine wawe exempted kulipa kodi?!.
Hili jambo la baadhi ya viongozi kutolipa kodi kwanza liliibuliwa na binti mdogo huyu Je, Rais wetu, Magufuli anasoma JF? Rais, Please msikilize Binti huyu, ana hoja ya Msingi! hivyo tukashauri Kuepuka Double Standards ya Kodi, Nashauri Rais Uongezwe Mshahara, Ili Alipe Kodi, Wote Tulipe Kodi!
Tanzania tumetawaliwa na Waingereza, hivyo tulipota uhuru tuliiga mambo mengi ya Uingereza, kule mkuu wa nchi ni mfalme, halipi kodi. Hivyo na sisi tukaiga mkuu wa nchi asilipe kodi, s/he is exempted, hivyo analipwa mshahara tax free.
Kuna aina mbili za utendaji wa viongozi, kuna viongozi wanatenda kwasababu wanaamini wanachotenda ni kitu sahihi, lakini kuna viongozi wanatenda ili tuu kuonyeshea watu waone. Hawa watendaji wanaotenda kwa ukweli wanaitwa genuine leaders they practice what they preach, na hawa watendaji wa maonyesho hawa ni pretenders, wanafanya show off na kwa kuongea wanafanya kitu kinachoitwa paying lip services they don't practice what they preach, kitendo cha kiongozi kuhimiza watu wote walipe kodi huku yeye halipi kodi ni hoodwinking.
Ili kila mtu alipe kodi, Tanzania tubadili sheria zetu za kodi tufuate the American system hadi rais analipa kodi!.
Wiki hii, kumefanyika kikao kazi kati ya Jukwaa la Wahariri TEF na Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA, kuhusu kuwatumia wahariri na vyombo rasmi vya habari, kueneza elimu ya kodi ili walipa kodi waelimishwe kuhusu kodi mbalimbali na umuhimu wa kulipa kodi, ili wajisikie fahari kulipa kodi.
Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile, aliipongeza TRA kwa kuwashirikisha wahariri na vyombo vya habari, katika suala zima la utoaji wa elimu kwa walipa kodi, badala ya jukumu hilo kubebwa na TRA wenyewe.
Balile amesema kama TRA itawatumia kikamilifu wahariri na vyombo vya habari kuelimisha umma kuhusiana na mambo ya kodi, vyombo vya habari vinawafikia wananchi wote na wananchi wakielimishwa kuhusu kodi na matokeo ya kodi zao, watakuwa wanalipa kodi na kujisikia fahari kulipa kodi.
Balile ametolea mfano mkoa wa Iringa, hakuna purukushani za kulipa kodi wala kukimbizana na wafanyabishara kuhusu kulipa kodi, kwasababu kitengo cha elimu kwa mlipa kodi cha Iringa, kimekuwa kikitoa elimu ya kodi kwa wananchi kupitia vyombo vya habari vya Iringa, zikiwemo redio za jamii, hivyo walipakodi wa Iringa, wameelewa umuhimu wa kodi, wanalipa kodi bila shuruti na hakuna kukimbizana wala kamata kamata au fungia fungia biashara kati ya wafanyabiashara wa Iringa na TRA.
Balile alimpongeza mkuu wa kitengo cha Elimu kwa Walipakodi wa Iringa, Paul John Walalaze, kwa ushirikiano wake na media za Iringa, ambapo sasa Walalaze amehamishiwa TRA Makao makuu kuwa meneja wa elimu kwa walipa kodi, Balile amemtaka Walalaze, kukifanya kile alichokifanya Iringa, akifanye Tanzania nzima, walipa kodi waelimishwe kuhusu kodi, TRA wadai kodi halali, na walipa kodi walipe kodi bila shuruti.
Kwa upande wake, Meneja huyu wa Elimu kwa walipa kodi, Paul John Walalaze, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa kodi, Richard Kayombo, Walalaze amesema kwa kutambua umuhuhimu wa vyombo vya habari katika kuyafikia makundi yote ya jamii, TRA imeamua kushirikiana na Jukwaa la Wahariri, kama wadau muhimu wa kufikisha elimu ya kodi kwa wananchi.
Walalaze amesema kuanzia mwaka huu wa fedha, TRA katika mikoa yote itazitumia redio za jamii kueneza elimu ya kodi, na wahariri wakashauri, sio tuu watumie redio za jamii pekee, bali pia watumie TV, magazeti na mitandao ya kijamii kila mkoa.
Kwa kuanzia TRA inaanzisha kampeni ya “Hakiki Stempu”, kutumia vyombo vya habari kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuhakiki Stempu za Ki Electroniki – ETF, (Electronic Tax Stamp) kwenye bidhaa mbalimbali za vinjwaji, zikiwemo maji, bia, soda, wines na vinywaji vikali vyote vinavyozalishwa nchini na vinavyoingizwa nchini kutoka nje ya nchi.
Wananchi wakielimishwa kuhakiki stempu za kielectroniki, sio tuu watabaini kama bidhaa hiyo ni bidhaa halali, uhakiki huo pia unawasaidia kubaini bidhaa bandia, hivyo uhakiki kusaidia kulinda afya za mlaji, ukigundua ni bidhaa bandia, usinywe kinywaji hicho kwa usalama wa afya yako.
Mtaalamu wa ETS wa TRA, Bwana Tweve alitoa mafunzo kwa wahariri ya jinsi ya kuhariri stempu za ki electroniki.
Mjumbe wa kamati ya uongozi ya TEF, Salim Said Salim kutoka Zanzibar, ambaye ni mmoja wa waandishi wa habari wakongwe nchini anayeandika mpaka sasa huku akielekea umri wa miaka 80!, aliwashauri TRA, kuwa wananchi hawapendi kuona wao wananchi wa kawaida ni masikini wa kutupa, wanaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, lakini bado wanakamuliwa kodi, halafu TRA wanatoa misamaha ya kodi kwa matajiri!, ameshauri misamaha ya kodi isiwepo, kila mtu alipe kodi.
Pia Salim Said Salim amezungumzia adhabu kali kwa wakepaji wa kodi, halafu adhabu kiduchu kwa wezi wa mali ya umma, wahujumu na wala rushwa, akataka wapewe adhabu kali kabisa kama wahalifu hatari!.
Mafundisho ya dini zote yanafundisha kuwa "Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu", kwa lengo la kuwathibitishia waumini wote wa dini zote kuwa tawala zozote zilizo madarakani kwa mujibu wa sheria, zinapaswa kuheshimiwa, kuungwa mkono na kupewa utii wa sheria bila shuruti, taratibu na kanuni, na miongoni mwa hayo ya Kaisari, ni pamoja na suala la kulipa kodi ambapo watu wote lazima walipe kodi ili kuiwezesha serikali kuendesha nchi!. Hivyo vitendo vyovyote vya ukwepaji kodi wa aina yoyote sio tuu ni ukiukwaji wa sheria, bali pia ni dhambi mbele ya Mwenyeezi Mungu!.
Katika sheria zetu za kodi, tuna sheria mbili, moja ni sheria ya watu wengine wote kulazimika kulipa kodi, na sheria nyingine imewatenga baadhi ya viongozi fulani fulani kwa kuwapa msamaha wa kutokulipa kodi yoyote kwa mujibu wa sheria.
Wahariri wamependekeza kuondoa hii double standards ya kodi, kwa wananchi kutozwa kodi, huku baadhi ya viongozi kuwa exempted kulipa kodi hivyo hawalipi kodi, lengo la hatua hii, ni kuwawezesha viongozi wetu kuyaishi kwa vitendo maisha wanayoyahubiri, yaani to practice what you preach, haiwezekani kiongozi ahamashishe kila mtu alipe kodi, huku kumbe yeye mwenyewe halipi kodi!, hili likifanyika litaondoa double standards ya kodi, kila mtu kulipa kodi, tena baadhi ya wahariri wameshauri, Tax Clearance certificate ya TRA iwe miongoni mwa sifa za kugombea uongozi ili tupate viongozi waadilifu.
Je tuendelee na mfumo wetu wa kuhubiri kila mtu alipe kodi huku kuna baadhi yetu wana misamaha ya kodi, au tubadili sheria, tuwaongeze mishahara hao viongozi wasiolipa kodi ili kila mtu alipe kodi?
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali