Biharamulo: Kampeni, kura na matokeo!

Masanilo
FMES huwa ananifurahisha sana CCM ikiwekwa angle mbaya.This time wanalo,Mukasa hebu tueleze,kulikoni gafla bin vuu ukawa Rwegasira?

Ni kweli naona ni vizuri mamba tukimuita mamba. Tusimuite Kenge. Lakini tukumbuke kuwa inapofika swala la CCM, maslahi yake yanakuwa mbele zaidi kuliko maslahi ya Taifa. Kuna mifano mingi tu ya watu wenye utanzania wenye utata, lakini kwa kuwa wanaCCM au kwa kuimba nyimbo za CCM wanakuwa WATANZANIA, wakibadilika kidogo tu basi wanakuwa siwatanzania. Hii tutake tusitake ni mbegu iliyopandwa na CCM kwa watanzania, si ajabu kama ikiota kama ilivyopandwa.
 
Kwani Katiba inasemaje? Kama katiba imeonyesha dhahili nani anae qualify kuwa Mtanzania kwa nini tuipinge?

Kwani ni mbunge tu ndiye anayestahili kuwa mtanzania? Mbona huu uzalendo hatunao kwenye nafasi nyingine? Mbona hatusikii tarishi kwenye ofisi ya serikali akisakamwa kuhusu uraia? Ni unafik kumuachia mtu asome, atumikie taifa hili kwa nguvu zake zote halafu vup bin vuu mara tunataka kujua uraia wake!

Amandla..........
 
- Sasa baba yake alifikiaje kufanya kazi kwenye serikali yetu mpaka kuwa ofisa wa juu huko wilayani na mkoani bila kua raia wetu? It does not add up!

Respect.

FMEs!

wakati wa nyerere nadhani hakuwa akifuata sana hayo mambo ya uraia, akiona wewe ni potential na uko tayari kulitumikia taifa basi unaishi na kuwa kama raia wako wengi tu hasa Wamalawi, Zambia, Warundi na Waganda
 

Mwanawane,

Mneno mingi but Sheria ni msumemo.
 
CCM waliwahi kumchagua Premji kule Kigoma akasimama akashinda uchaguzi mahakama ikatangua kwa kuwa hakuwa raia kwa mujibu wa sheria za nchi kwa hiyo hata huko Biharamulo wanaweza kumsimamisha mtu asiye raia
 
Kulingana na mfano wako, Ndumilakuili Kipepe ni mtu tofauti na Ndumilakuili Pimbi Betiba. Hivyo utatiwa hatiani kwa kutoa taarifa za uwongo. lakini si kosa watu kukuhoji kwa nini umedanganya majina. In fact wasipokuhoji ndio watakuwa wanafanya kosa
 
Kulingana na mfano wako, Ndumilakuili Kipepe ni mtu tofauti na Ndumilakuili Pimbi Betiba. Hivyo utatiwa hatiani kwa kutoa taarifa za uwongo. lakini si kosa watu kukuhoji kwa nini umedanganya majina. In fact wasipokuhoji ndio watakuwa wanafanya kosa

Sasa cha msingi ni kuangalia document zote kama bwana Mukasa alidanganya majina basi sheria ichukue mkondo wake, anyway sheria huwa inakuwa mbaya inapowahusu baadhi ya watu.
This is animal farm principalkwambat all animals are equal but others are more equal than other
 
Ile kutoka Mukasa kuja Rwegasira ilikuwa ni ishara tosha, lakini mbona Matayo david Msuya alivyobadili kuwa Matayo David Matayo hakukuwa na angalizi ama kwa kuwa yote ni majina ya kitanzania? Mukasa aje na vielelezo vya uraia wake!


Huyu matayo haileti maswali sababu kaondoa tu ubini wa kipare kwa sababu anazojua mwenyewe. Historia yake inafahamika na waliompakata akiwa mdogo wanashuhudia
 
Kulingana na mfano wako, Ndumilakuili Kipepe ni mtu tofauti na Ndumilakuili Pimbi Betiba. Hivyo utatiwa hatiani kwa kutoa taarifa za uwongo. lakini si kosa watu kukuhoji kwa nini umedanganya majina. In fact wasipokuhoji ndio watakuwa wanafanya kosa


Mpitanjia, Mfano wa ndege ya uchumi inatupeleka kule kule kwa ROSTUM, RUSTUM, ROSTAM, Sakary n.k. Hivyo sasa hivi mtu akileta majina tofauti tu tunashtuka!
 
tunasubiri kwa hamu!

POLENI Kwa kusubiria ni kweli pingamizi limetupiliwa mbali sababu msimamzi ameeleza lakini chadema wameamua kukata rufaa tume ya taifa ya uchaguzi na wamedai kuwa wanao ushahidi, mmoja wapo ya ushahidi huo ni mkanda wa video wa maelezo ya mgombea huyo ambayo yanatofautiana na yake aliyojaza katika fomu na yake aliyosema katika kikao cha CCM
 
CCM ni noma. Hilo pingamizi lazima walikatae (kwa kutumia wasimamizi wa uchaguzi). Halafu CHADEMA wakikata rufaa tume ya uchaguzi, nayo itakataa. Wakienda mahakamani hakuna uchaguzi hadi mwakani, wanapitisha mgombea mwingine!

Kule mbeya mtu alitolewa kwa kusign kwa wakili badala ya hakimu. Ni wagombea wangapi wa CCM wengine wako madarakani waliokwisha sainisha fomu zao kwa mawakili? Wapo wengi. Ila uamuzi ilikuwa wa mara moja usio na mjadala. Sasa hili wako tayari kusiwe na uchaguzi B'muro. They will do it!
 

Kwa nini hawaendi mahakamani moja kwa moja?
Kabla msimamizi wa uchaguzi hajatupilia mbali malalamiko yao ni lazima amewasiliana na tume, kwa hiyo CHADEMA wasitegemee muujiza toka tume. Kama wako serious waende mahakamani moja kwa moja.
 
Msemo wa "Sheria ni msumeno" nadhani kwa sasa ufutwe na uwe "sheria ni kisu" kinachokata upande mmoja aupendao mkataji.
 
Dah dogo wajanja ndo washakuharibi, kwa kifupi kitumbia kishaingia mchanga, no deal tena, rudi Ifakara health uendeleze fani yako ya IT
 
Nikisema Uwiano ni Mkenya, huna jukumu kuthibisha we si Mkenya. Mzigo wa kuthibisha tuhuma ni wa mtuhumu.
Lakini kwa Immigration mambo huwa tofauti. Ukiambiwa wewe si raia basi unatakiwa uondoke, otherwise uthibitishe kwamba wewe ni raia wa Tz. Na ndio maana Immigration wakikuambia uondoke Tz, huwa hawasemi ni nchi gani uende, kwa maana wanachukulia kwamba hilo si jukumu lao, ila sasa ni jukumu lako wewe mtuhumiwa kuthibitisha kwamba wewe ni Mtanzania so unatakiwa kuwapo Tanzania kama raia. Umeshawahi kusikia Immigration wanamtajia mtu nchi yake? No, ila wanakupa tu masaa machache unayoweza kuwepo Tz.
 
Binafsi nilijua Chadema hawafiki mbali - kwani Jaji Lewis Makame akale wapi ? mzee wa watu na umri ndio huo tena. Kisheria Oscar Mukasa hawezi kuwa Oscar Rwegasira - labda akale kiapo mahakamani. Kuna ushahidi wa tangu awali kuwa Oscar Mukasa ndiye alijitokeza kuwania ubunge kwa tiketi ya CCM. Hili jina ndilo lililowasilishwa CC na ndio maana wadakuzi wakatutangazia kuwa aliyeteuliwa ni Oscar Mukasa

Hata hivyo baada ya vuta nikuvute ndani ya kikao cha CC kuhusiana na jina Mukasa, kikao kinachojulikana zaidi kwa kuhalalisha ufisadi, jina Rwegasira likawa "invented". Shughuli kubwa iliyofanyika baada ya hapo ni kulihalalisha hili jina na kikao kilimalizika tu baada ya kuhakikisha kuwa mamlaka zote husika zimehamasishwa. Ndio maana tunasikia habari za CCM chama makini, hakiwezi kufanya kosa kama hilo.


Oscar Mukasa - Rwegasira katoka wapi ?

CCM wameweza kumhalalisha Abdulrasul Chakaar
watashindwaje Oscar Rwegasira ?
 
..nimezungumza na jamaa wanaomfahamu mgombea wa CCM. wanadai siku zote amekuwa akijulikana kama Oscar Mukasa.

..labda ana matatizo ya uraia kama wengi wanavyohisi hapa.

..uwezekano mwingine alirudia shule[darasa la saba] na kulazimika kubadilisha jina.
 
Bofya HAPA kunogesha mjadala. Jamaa wanaua noma kwa kutoweka jina la baba ya mgombea, vinginevyo yangekuwa manne na kuongeza maswali. Nadhani la Mukasa wameliweka katikati ili lionekane ni la baba yake, na si la ukoo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…