JAMANI nadhani swala la uraia watu tumeshaliongelea hapa mpaka sheria na misahafu ikatundikwa humu. Kikubwa hapa naomba tujue kwamba..kila mtu anayo haki ya kubadilisha jina lake na kuitwa anavyotaka. Hata kama angeamua kuitwa Chungwa au embe...its him! Unless proved otherwise.
Nategemea watu humu JF tulijadili swala hili objectively. Kwanza, lazima tujue kabisa watu wengi wa Tanzania especially wa mikoa iliyo pembezoni mwa nchi kama Kagera, Kigoma, Mara nk..wengi wa wananchi wana connection na nchi jirani either kwa lugha au undugu. NA HILI ni purely geographical accident halikwepeki. Mtu wa Kigoma au Ngara definitely yuko closer na mtu wa Burundi kuliko mtu wa Rukwa kwa sababu ambazo ziko wazi kabisa. Wanaongea lugha moja! So is mtu wa Mara na mtu wa Kenya. But kasumba ambayo tunaiendekeza especially wabongo wengi..ni kuwaona raia wa hizi sehemu kama warwanda au warundi..simply because they speak similar language..same ukija Msoma..Mkurya ataambiwa..wewe kwanza ni mkenya..and on and on.. Hili lazima tulikubali kama legacy ya mipaka iliyowekwa blindly na mkoloni na kuhalalishwa na nchi zetu baada ya uhuru. Na hawa watu wameingiliana maana ndo wanasaidiana katika shida na raha..Its purely geographical accident.
Pili, lazima tujue kwamba Tanzania yetu sheria nyingi ziko kwenye mashelf wananchi waliowengi hawazijui na viongozi ambao wanapaswa kuzitekeleza wanafumba macho..zinaibuliwa pale kunapokuwa na maslahi ya watu fulani. Kwa hiyo usishangae kuona kuna warwanda, wakenya, waganda..name them..wameishi tanzania wakaoa watanzania..watoto wao wamezaliwa Tanzania..wamekulia tanzania kifupi they have known no other homeland than Tanzania. Na wamefanya yote haya bila kuulizwa na mtu. Sasa inapofika watoto kama hawa waliohangaika kama watanzania, ingawa wazazi wao either hawakuwa raia au hawakuhalalisha uraia wao.. wengine wanataka ku-participate kwenye shughuli pevu kama hizi za kisiasa..ndo sheria zinaibuliwa. Sasa huyu mtu aende wapi? mtu kazaliwa kijijini hata hiyo birth certificate hana! Yes, ni rahisi kusema kwamba watu wahalalishe uraia wao..lakini do you think..hii fursa ni wangapi wanaijua? Na swali langu kubwa..why should we punish a child kwa sababu ya makosa ya wazazi wake? Huyu hata ungemrudisha Uganda kwanza atajulikana kama Mtanzania..na at the end of the day..atakuwa Stateless. Maana hata huko hatakubalika!
Kama alivyouliza FMES..iweje kama baba siyo raia afikie level kubwa ya utumishi katika jamhuri yetu? Jibu wote tunalijua..swala la uraia ni kadi ya maslahi especially siasa. na si Tanzania tuu..its all over Africa.
Mi nadhani issue kama hizi za uraia..ni vema ku-raise legitimate questions, lakini tusiwahukumu watoto ambao wamepigana kama sisi..simply because their parents did this or that. Ni kuwanyima fursa...simply because baba au mama hakufanya kitu fulani..ni kama kumuita mtoto wa nje ya ndoa..illegitimate..its damn unfair..maana mtoto hakuhusika na maelewano ya wazazi wake..sasa kwa nini leo anyimwe haki sawa..simply because alizaliwa kwa baba aliyekimbia mimba? Think about it. NA KUNA SHERIA KAMA HIZI ARCHAIC NYINGI..BADO ZIMO KWENYE VITABU VYETU!
Ndo maana governance inatushinda, maana jiulize..ni lini hawa wanaomuwekea pingamizi walijua kwamba jamaa siyo raia? mbona hawakusema hilo mapema? Ofcourse Chadema wana haki ya kuuliza maswali kama haya..lakini..sisi kama wasomi humu JF..we should go beyond these cheap talk..tupeane ideas namna ya kuli-address hili tatizo maana kuna silent majorities wengi sana kwenye hii dilemma. Yaani baba ni wa kuja lakini mtu kazaliwa Tanzania na ameishi TZ miaka yote..leo amemaliza Chuo kikuu..amepata scholarship ya kwenda PHD nje..ananyimwa passport kwamba siyo raia..it doesnt add up..mtu kama huyo..anakuwa frustrated sana...yuko radhi kutoa rushwa yoyote apate hiyo passport.
My suggestion: Tufanye kama USA with some modifications kiasi..kila mtu ahukumiwe kama yeye! Kama umezaliwa ndani ya mipaka yetu basi wewe ni raia (with few exceptions kama wakimbizi walio chini ya uangalizi wa sheria za kimataifa..etc).... Hii itawasaidia watoto wengi..especially wanaozaliwa vijijini. Otherwise hii ni political witch hunt..ambayo inamuumiza kijana wa watu kwa kosa ambalo hakulifanya. Angalia hata CV yake..kijana ni mpiganaji..leo anaambiwa eti siyo raia..duh!
Masanja,