Biharamulo: Kampeni, kura na matokeo!

 

Kama Mkandala aka Prof Mkandala humfahamu basi kumbe wewe ni Chuo Cha Mafisadi - Tumaini mtandao camps.

Hamjui wewe ulimpa nini RA? Suala la kuuliza hili mkuu?

Sisi huku Kahama muda wa kulala? kesho mkuu,
- Hillarious......Bwa! ha! ha! mchanga wa JF bwana Bwa! ha! maneno mazito sana haya mkuu, na ubarikiwe ila acha namecalling, mimi ni FMES sio chuo cha mafisadi wala tumaini camps huo sio ustaarabu, yaani hutaki mawazo yangu wka hiyo ninakuwa chuo cha mafisadi? Haya mkuu.

Respect.

FMEs!
 
Sorry mkuu, ungekuwa CCM ungemfahamu huyu ila wewe either ni mwanachuo, lecturer au supporting staff.

Mkuu wangu tunapojadili suala la mtandao maslahi campus tunakuwa wote ila kwingine unasahau kuwa wewe ni mtanzania. Kwenye sala ya usiku huu nakuombea.

bye
 
FMES anazo data za kwanini walikesha hata hawakulala kwao. Kama kweli FMES una mapenzi na nchi hii sema yote. otherwise unaniyeyusha kinoma.

Mkuu FMEs, naungana na Selous, kama una mapenzi ya kweli na TZ, can you come clean ? Kwa nini tuendelee kukuamini kama hutafanya hivyo ?


Asante sana Selous, umenifungua macho na sasa naweza ku"connect the dots". Nilikuwa najiuliza kwa nini kikao mpaka usiku - well, nilisema tangu mapema kuwa hili jina Mukasa/Rwegasira lina wingu zito. Wazungu husema "covering one's behind" na yanikumbusha watergate - kweli CCM si mchezo. Lakini vipi wataweza kufuta documents zote za nyuma ? mpaka airline tickets ? Kuna mahali watakwama tu ila kwa kuwa ni wahitimu wa kuhalalisha ufisadi, nani wa kuwazuia.
CCM ni Chuo cha Mafisadi kweli kweli !!
Kama Abdulrasul Chakaar sasa ni Mb. Mh. Rostam Aziz
Kimzuie nini Oscar Mukasa kuwa Mb. Mh. Oscar Rwegasira.
Jaji Makame upooooo?
 
 


Mkuu FMES,

Mwendelezo wa hii ahadi vipi? au kama kama?
 
Jamani jibu la kueleweka kuhusu utata wa Mukasa ambaye alibatizwa mara moja jina la Rwegasira?
 
FMES anazo data za kwanini walikesha hata hawakulala kwao. Kama kweli FMES una mapenzi na nchi hii sema yote. otherwise unaniyeyusha kinoma.

Quote; Selous:Mkuu FMES,

Mwendelezo wa hii ahadi vipi? au kama kama?


- Kinachokufurahisha ni ligi tu, na kuvuruga vichwa vya members humu as much as you can it makes you happy, it makes your day and then unageuka na kua kichanga wa JF. Umesema unamjua sana Oscar, alivyozaliwa, familia yake ilivyofika huko Misenyi, sasa wakati ni huu tueleze unachojua hamna lolote ni ile ile tabia ya kuvuruga vuruga watu vichwa hapa,

- Ninasema tena Oscar, anaonekana ni agent of change na JF tuwakumbatie wagombea wana namna hii kwa sababu hata wakikosea ni rahisi kwa sisi wananchi kuwaingia vichwani mwao, wapewe nafasi ya kutuongoza, huyu ni msomi tena kijana JF we should never be a part of kuwakatisha tamaa vijana wasomi, tuwahukumu kutokana na matendo yao kwenye hili la kumshambulia huyu kijana bila facts, we are wrong JF,

- Heshima kwa The rule of law, maana yake sio heshima kwa majungu na politics of desparations, na kila mwananchi hata kama ni mgombea wa siasa au kiongozi wa siasa wana haki sawa na wengine wote ya kuwa afforded nafasi ya kujitetea wanapotuhumiwa na uvunjaji sheria ya jamhuri, Chadema wafukuzeni washauri wenu wote huko wa kampeni na siasa, kwa sababu hawawezi kuwasiaida na mawazo kama haya ya kuwatenga vijana wote wasomi na makini eti kwa sababu tu wanagombea under CCM.

- Investing in uraia wa Oscar, kwenye kampeni za Biharamulo ni a wrong political strategy, eti kugomea uchaguzi nayo pia ni childish strategy Wa-Tanzania ifike wakati tuachane na hizi politics za kuwekeza kwenye majina kwa sababu ndizo zimetufikisha hapa tulipo yaani backwards, tiujifunze kuwekeza kwenye sound policies!

Respect.

FMEs!
 
Mzee Mwanakijiji unasema eti CCM ni chama makini; kwa hiyo hakiwezi kumteua Mgombea ambaye si raia! Inaonekana wewe si Mzee sana, au umesahau kwamba CCM mwaka wa 1993 ilimteua Azim Premji wa Kigoma-Ujiji kugombea mara tu Tz ilipoingia ktk Mfumo wa Vyama vingi vya Siasa. CHADEMA kilimsimamisha Walid Kabourou. Awali Premji alishinda kwa margin kidogo na Chadema kilikwenda Mahakamani kueleza dosari zilizojitokeza katika kampeni, zikiwa ni pamoja na kwamba Premji alikuwa sio Raia halali wa Tz.

Uchaguzi ulitangazwa na Mahakama Kuu kwamba ni batili kutokana na Premji kutokuwa Raia, pamoja na irregularities nyingine. Licha ya kwamba Azim Premji alizaliwa Tanzania, wazazi wake walikuwa wahamiaji. Sheria inatamka kwamba ni lazima mtoto kama huyo, anapofikia umri wa miaka 18 ajiandikishe rasmi kama raia wa Tz na aukane uraia wa awali wa wazazi wake.

Maelezo yaMag3 kwamba baba yake huyu Mgomgea wa CCM, yaani Oscar Rwegasira/? Mukasa alikuwa mfanyakazi ktk wilaya za Biharamulo na Ngara siyo jibu. Inawezekana ni Mganda na si Mtanzania. Kama mtoto wake hajajiandikisha rasmi na kuomba uraia wa Tanzania, na kuukana wa Uganda wa kuzaliwa, basi siyo Raia wa Tz na hawezi kugombea Ubunge.

CCM imekosea kumteua na imwondoe, badala ya kujiaibisha kwa kukiuka Sheria iliyoitunga yenyewe wakati wa Mfumo wa Chama Kimoja. Na wewe Judge Makame, Mwenyekiti wa NEC usiendelee kujiaibisha kwa kutotoa uamuzi. Thibitisha kuwa wewe ni mtu usiyependelea CCM au chama chochote cha siasa kwa kutamka huyo Rwegasira ni mgombea batili endapo sio Raia wa Tz. Shame on you if you don't.
 
Ni kweli Mgombea wa Biharamulo si Mtanzania, lakini kwa vile ni mgombea wa CCM, sheria zitabadilishwa! CCM Daima!
 
Now Look at this theory hapa chini ili uone hili starved information nation linavyohangaika na habari:-
- Sasa JF ni taasisi ya great thinkers, tizama charges hapo juu dhidi ya Mukasa na verdict humo humo, pamoja jury kwanza anasema inawezekana, meaning kwamba hajui anachosema, halafu anasema kama hajajiandikisha, and then anakuja na strong verdict pamoja sentense against CCM na Oscar, na this ni kutoka JF great thinkers!

Mungu Aibariki Tanzania.

FMEs!
 


- Wazazi wa Oscar walihamia Tanzania mwaka 1971, na in Six years tayari Baba wa Oscar alishaji-establish mpaka kufikia kuwa ofisa mkubwa sana serikalini yaani local govmnt, I mean sijui the facts lakini logically does this make any sense?

Respect.

FMEs!
 
Je kuna uwezekano wa kutumia hiyo kwa Rostam?
 
FMES mbona hii umeivali njuga hii kitu kuna siri unaijua ambayo sasa unaogopa itatoka nje ? Si kawaida yako mkuu kukaza buti namna hebu butafute sirini kwanza tuseme maana niko Bukoba nikupe yaliyopo hapa.
 
FMES mbona hii umeivali njuga hii kitu kuna siri unaijua ambayo sasa unaogopa itatoka nje ? Si kawaida yako mkuu kukaza buti namna hebu butafute sirini kwanza tuseme maana niko Bukoba nikupe yaliyopo hapa.


Mkuu tupe yanayo jili huko, hata hivo hiki kigugumizi chanini? mbona hatuambiwi ni ama si raia wa bongo kwa mjibu wa sheria?

Kwanza kwa mtu wa kawaida utaanza kustukia hata wasifu wa mgombea, kujua kwamba ulikuwa una kitu unakifukia, ulijikita zaidi kueleza wasifu wa baba yake alivokuwa ofisa wa serikali as if yeye ndo mgombea! why all those?

We need our law to stand firm!
 
FMES,

..kwa kweli nimechanganyikiwa sasa.

..huyu jamaa kwenye kura ya maoni si alikuwa Oscar Mukasa? sasa kwanini usiku wa manane CCM-Central Committee wambatize kuwa Oscar Rwegasira?

..hivi taratibu za kubadilisha jina toka Oscar Mukasa mpaka Oscar Rwegasira zimefuatwa?

..nadhani kabla hata ya kwenda kwenye uraia wa huyu bwana hilo la kubadilisha majina lazima lishughulikiwe kwanza.
 
FMES,
..huyu jamaa kwenye kura ya maoni si alikuwa Oscar Mukasa? sasa kwanini usiku wa manane CCM-Central Committee wambatize kuwa Oscar Rwegasira?

JK unataka kununua vita na mzee wa sauti? FMES anadai CCM ni makini sana wanajua wanachokifanya ..... wakati mwingine huwa anapenda kukimbia ukweli!
 
Rwagubiri issue iko hivi , hakuna anayempinga msomi wa Kitanzania kama angalikuwa Mtanzania msomi na kijana kama Oscar.Issue si kwamba anagombea CCM ila nataka kusema kwamba Oscar ni opportunitst ambaye hatakuwa namsaada kwa Taifa .Ana tabia za kiganda kwisha ama kinyarwanda kwamba nia yake sasa inaelekea kutimia .Huyu kijana ni mwajiriwa pale Morogoro na shule yake inakubalika lakini Oscar kama kuna mtu anabisha aje asema kadi ya Chadema aliirudisha lini na kwa nini .Tunajua walitumwa watu akiwemo Kamara walimpa live kwamba arudishe kadi na kuingia CCM na wao watachuua jukumu la kumsaidia . Naombeni wana JF wote mjue kwamba Oscar aliitwa Ikulu na aliongea na JK kwa saa moja nzima na ndipo akaenda straight Jimboni.Leo tunalia kwamba si raia lakini nataka mjue kwamba pamoja na kwamba tunataka haki itendeke JK anajua na anatarajia Oscar Mukasa kushinda kwa kuwa ana baraka zake na mambo ya Uraia ni kupoteza muda atakuwa cleared na mtegemeeni baadaye kushika uwaziri .Yangu ni hayo endeleeni kubisha lakini mtaona baadaye .Niko kwenye meli naelekea Bukoba
 
Degauche 2008 hapo juu umeuliza kama interpretation yangu kuhusu uraia ingeweza kutumika kuhusu Rostam Aziz, Mbunge wa Igunga!

Nielewavyo, huyu gabachori alizaliwa huko Tabora. Wazazi wake pia walizaliwa Tanganyika. It is unfortunate for us. Labda tutafute evidence kwamba ana uraia mwingine kama Uajemi n.k. Angekuwa amekiuka sheria ya uraia ya sasa inayokataza dual citizenship.
 
ZeMarcopolo,
Nadhani huifanyii Taifa lako haki kwa comment hii.
i) Malumbano ya kisiasa wakati wa uchaguzi ni sehemu, process ya kumtambua mgombea mzuri. Hii haifanyiki tu Tanzania, hata nchi zote kubwa kuchimbiana, na ni sehemu muhimu ya kupata credibility na trustworthiness ya Wagombea. Hivyo si suala la maendeleo tu. Wakati wa Utawala wa Chama kimoja tulioshiriki tulielezwa tusilumbane, bali tuzungumzie shida. Kwa miaka zaidi ya 45 hiyo hali haijatokea. Hivyo si Comment ya namna hii haina basis ya kisayansi kuhukumu kuwa maendeleo hayako kwa sababu ya aina ya malumbano yaliyoko wakati wa Kampeni.
2) Katika Kampeni kama unafuatia vizuri, mfumo wa constructive kampeni ni kukosoa sera ya Chama Tawala au vyama vilivyoko kwenye kinyang'anyiro ikiwa ni pamoja na kuchambua utekelezaji wa Sera hizo kwa upande wa Chama Tawala ambao ndio wenye jukumu la kutumia kodi ya Wananchi kwa maendeleo yao. Uchambuzi huo sio malumbano, bali ni analysis muhimu kuona kuwa chama kitakachochaguliwa kinaweza kuwa na sera nzuri kwenye makaratasi, lakini sera na Ilani hizo zimetumika kwa kiasi gani katika kuwaletea maendeleo wananchi. Hoja za aina hii, zinawafumbua wananchi macho, wafanye tathmini ya kweli kwa kuwapatia silaha yaani data muhimu ambao kwa hali yao ya vijijini hawawezi kuipata kama si kwa njia ya mikutano hiyo ya hadhara. Mwanasiasa wa kweli anafahamu umuhimu wa hoja ya aina hiyo na hawezi kuipuuza hata kidogo.
3)Mwanasiasa yeyote makini, hataishia katika kutoa critique ya utekelezaji wa sera za Chama Tawala, ataenda mbele kuchambua mahitaji muhimu ya wananchi, na tofauti na chama kingine chama chake kitafanya nini kuondoa au kupunguza matatizo hayo. Hivyo kwa mtu yeyote asiyefuatilia kwa undani hotuba za jukwaani na kusoma tu sehemu ya mambo yanayorekodiwa akapata tu taarifa ya kurushiana mawe, au sura ya kuwasema watu na au hata kutukanana kunakoripotiwa ni sehemu ndogo sana ya matukio yaliyoko kwenye Kampeni. Haiwezekani Mwanasiasa mahiri asimame jukwaani kwa zaidi ya dakika 40 au saa moja, aishie kutukana tu au kulumbana tu. Nadhani ZeMarcopolo kuna haja ya utafiti wa kina wa siasa za Tanzania kuliko kui paint negatively kama ulivyofanya. Ninayasema haya from field experience, sasa kama kuna experience tofauti ni vema ukatueleza concrete cases ili tuzichambue lakini generalization za aina ya hoja yako ni hatari hata kwa wanaofuatilia hoja katika JF ambako kwa wengi ni sehemu muhimu ya kujifunzia pia. Let us do justice to ourselves and to our nation.
4) Wana JF naomba radhi kwa muda nilipotea kwenye mtandao kwa vile nilikuwa niko nje ya Nchi kuhudhuria SADC-Parliamentary Forum ( Bunge la Mpito la SADC). Sasa niko hewani tena. Nawashukuru sana kwa michango yenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…