Biharamulo: Kampeni, kura na matokeo!

Biharamulo: Kampeni, kura na matokeo!

- Look here, Dr. Slaa alipowataja tu kabla hawajawekwa kwenye gazeti lolote la taifa nilikuwa na dataz nikaziweka hapa, sasa ningekua na tatizo nazo kweli ningezileta hapa?

- Kuhusu dataz tunapopewa dataz huwa tunaambiwa, zipi ni off the record na zipi ni on the record, sina dataz yoyote inayoweza kuthibitisha kwamba Oscar sio raia, na sijawahi kusema kua nazo.



- Kwani mkuu naomba kukuuliza eti Mukandala ni nani Tanzania? Maaana simfahamu kiongozi yoyote Tanzania mwenye hilo jina, ni waziri au what na yupo wapi? Halafu hapa sijakupata unasema nini hasa what do I have to do na this stuff?



- Yaani mimi nilimpa RA what? Mkuu mbona sikuelewi unasema nini? what this has to do na uraia wa Oscar?

Respect.

FMEs!


Kama Mkandala aka Prof Mkandala humfahamu basi kumbe wewe ni Chuo Cha Mafisadi - Tumaini mtandao camps.

Hamjui wewe ulimpa nini RA? Suala la kuuliza hili mkuu?

Sisi huku Kahama muda wa kulala? kesho mkuu,
 
Wajameni amani kwenu, JF huwa zinakatwa hoja na facts. Basi hii ligi nyingine tusimamishe tuendeleze hoja kwa hoja. Kwani naona kama sio haya majina ya bandia tungeviziana vibambazani.
Heshima kwenu wakubwa na wadogo tuache yasiyojenga turudi kwenye mada.

Kama Mkandala aka Prof Mkandala humfahamu basi kumbe wewe ni Chuo Cha Mafisadi - Tumaini mtandao camps.

Hamjui wewe ulimpa nini RA? Suala la kuuliza hili mkuu?

Sisi huku Kahama muda wa kulala? kesho mkuu,
- Hillarious......Bwa! ha! ha! mchanga wa JF bwana Bwa! ha! maneno mazito sana haya mkuu, na ubarikiwe ila acha namecalling, mimi ni FMES sio chuo cha mafisadi wala tumaini camps huo sio ustaarabu, yaani hutaki mawazo yangu wka hiyo ninakuwa chuo cha mafisadi? Haya mkuu.

Respect.

FMEs!
 
Sorry mkuu, ungekuwa CCM ungemfahamu huyu ila wewe either ni mwanachuo, lecturer au supporting staff.

Mkuu wangu tunapojadili suala la mtandao maslahi campus tunakuwa wote ila kwingine unasahau kuwa wewe ni mtanzania. Kwenye sala ya usiku huu nakuombea.

bye
 
FMES anazo data za kwanini walikesha hata hawakulala kwao. Kama kweli FMES una mapenzi na nchi hii sema yote. otherwise unaniyeyusha kinoma.

Mkuu FMEs, naungana na Selous, kama una mapenzi ya kweli na TZ, can you come clean ? Kwa nini tuendelee kukuamini kama hutafanya hivyo ?

Kwenye Chuo Cha Mafisadi wewe ni dean wa faculty ipi? propaganda? Unazo data kwa kuwa ulisema hapa kama sikosei. Mzimu wa huyo Dr wa chadema au tlp naona unakunyima usingizi.

Huwezi kuwa na tatizo maana Mkandala mlimuweka pale, RITA mliwatafuta ndo maana mkachelewa kulala. Ilikuwa kama zege kuwa kila mtu anawekwa sawa. ila zile karatasi za miaka ile mmezipata?
Kama RA mlimpa mtashindwa huyu?

Asante sana Selous, umenifungua macho na sasa naweza ku"connect the dots". Nilikuwa najiuliza kwa nini kikao mpaka usiku - well, nilisema tangu mapema kuwa hili jina Mukasa/Rwegasira lina wingu zito. Wazungu husema "covering one's behind" na yanikumbusha watergate - kweli CCM si mchezo. Lakini vipi wataweza kufuta documents zote za nyuma ? mpaka airline tickets ? Kuna mahali watakwama tu ila kwa kuwa ni wahitimu wa kuhalalisha ufisadi, nani wa kuwazuia.
CCM ni Chuo cha Mafisadi kweli kweli !!
Kama Abdulrasul Chakaar sasa ni Mb. Mh. Rostam Aziz
Kimzuie nini Oscar Mukasa kuwa Mb. Mh. Oscar Rwegasira.
Jaji Makame upooooo?
 
Mkuu FMEs, naungana na Selous, kama una mapenzi ya kweli na TZ, can you come clean ? Kwa nini tuendelee kukuamini kama hutafanya hivyo ?

- Mkuu mbona unabadilika tena, mara ngapi umewahi kusema mimi ni mmoja wa mafisadi, kwa sababu tu nina mawazo tofauti na yako? Na huyu unayem-support ameandika mara nyingi sana hapa kwamba dataz zangu huwa ni za uongo, sasa leo eti zimegeuka kuwa ni za kweli, kisa na mkasa mnataka kumsulubu huyu kijana, Mukasa ndivyo tulivyo hatuwezi kuwa tofauti hata iweje ndivyo tulivyo.

- Mkuu Mag3, sio siri kwamba you are a very smart man jinsi unavyo-move back and forth ndani ya hii forums, lakini sio wote sisi ni wajinga, kuna tunakuona kama ulivyo na siku zote tunajaribu kukupa heshima kwenye ukweli na hoja za kimapinduzi, lakini sometimes na wewe unazidisha mipaka, huwezi kuivalia njuga hii ishu bila ya kuwa na facts, na wakati umefika ni lazima ukubali waliokupa hii ishu na wewe hamna facts, au kama mnazo hamjazitoa wazi tukaziona, kwa hiyo sio haki kumuhukumu Oscar.

- Respect kwa The rule of law, ni pamoja na guarantee ya a due process kwa kila mwanachi anapotuhumiwa kuvunja sheria, ni lazima apewe nafasi ya kujieleza na kujibu ipasavyo na ikibidi jamhuri inatakiwa impe wakili wa kumsaidia, Oscar Mukasa Rwegasira ni raia mwenzetu mpaka sheria itakapotuambia otherwise, hatuko hapa ku-demand creation ya taifa la wenda wazimu, yaani mwananchi mmoja akikurupuka huko kuwa huyu sio raia basi ikishafika tu hapa JF, basi huyoooo sio raia, CCM imeshikwa pabaya!, wamezoea hao hata Rostam sio raia!, hiyo sio the respect kwa the rule of law, huo ni wenda wazimu na chama chochote cha siasa kinachochochea tabia kama hizi ni lazima tukiogope sana kama ukoma!

- Kama kuaminika hapa JF ni lazima kukubaliana na mawazo yako tu, then una haki zote za kuacha kuniamini, yaani unasema mmeanzisha hii ishu kwa kutegemea dataz kutoka kwangu? Eti kwa sababu sujui yote yaliyojaidliwa kwenye kikao cha CC ambacho mimi sio member, sasa ninatakiwa nisiaminiwe hapa JF, na kwamba kuna something ninaficha ambacho wewe uki-connect dots zako unapata jawabu kwamba Oscar sio raia na mimi ninahusika kuficha ukweli, kweli mkuu huoni kwamba haya mawazo ni mufilisi kwa member kichwa kama wewe licha tu ya kuwanayo, lakini hata kusema hadharani hapa ni aibu! Sasa mimi ndiye mchawi wenu, siku zote msopoweza kupata your way na CCM, basi FMEs ndiye mchawi, pole sana mkuu sina cha kukusaidia!


Asante sana Selous, umenifungua macho na sasa naweza ku"connect the dots". Nilikuwa najiuliza kwa nini kikao mpaka usiku - well, nilisema tangu mapema kuwa hili jina Mukasa/Rwegasira lina wingu zito. Wazungu husema "covering one's behind" na yanikumbusha watergate - kweli CCM si mchezo. Lakini vipi wataweza kufuta documents zote za nyuma ? mpaka airline tickets ? Kuna mahali watakwama tu ila kwa kuwa ni wahitimu wa kuhalalisha ufisadi, nani wa kuwazuia.
CCM ni Chuo cha Mafisadi kweli kweli !!
Kama Abdulrasul Chakaar sasa ni Mb. Mh. Rostam Aziz
Kimzuie nini Oscar Mukasa kuwa Mb. Mh. Oscar Rwegasira.
Jaji Makame upooooo?
- Haya ndio maneno ya kawaida sana hapa ukitaka fame ya temporary hapa JF, lakini inapokuja kwenye ukweli wake siku zote ni tatizo, na matokeo huwa wananchi kukatishwa tamaa, kwa sababu look sasa hivi mnajaribu kutuaminisha kwamba mna ishu nzito na huu uchaguzi wa Biharamulo kuhusu uraia wa Oscar, matokeo wananchi wengi wata-invest in this kusadikika theory kama unavyoona kwenye hii thread, tayari wengi wameshanasa bila facts, maana ukisema wewe Mag3 kwa wengi wetu humu JF huwa ni kweli tu, halafu tutakuja kuambiwa jinsi CCM ilivyozoea kuwakumbatia wageni, tizama Ulimwengu ni mgeni, Rostam ni mgeni, Idd Simba ni mgeni, halafu wameiba shahada hawa mbona walioandikisha ni laki moja waliopiga kura 50,000 tu CCM wameiba, siku imekwisha wananchi wajinga ndio waliwao, hakuna responsibility wala uwajibikaji wa hela zetu nyingi za ruzuku wanazopewa Upinzani, ila ni CCM tu ndio waizi na wakumbatiaji wageni.

- Mmerukia habari ya uraia wa Oscar, sasa bado ni burden yenu kuleta ukweli wote kwa nini mnamtuhumu huyu kijana kuwa sio raia, tunajua alizaliwa Uganda alikuja Tanzania mwaka 1977, okay wapi ushahidi wa kisheria maana kuzaliwa kwa mwananchi lazima kuthibitishwe na sheria, ooooh FMEs anajua huyu anaficha maana kikao kimefanyika mpaka usiku wa manane, huyu FMEs haaminiki kabisa ni fisadi!, really? vipi wewe unayeaminika ushahidi uko wapi? abanwe FMEs tu ndio anajua, Bwa! ha! ha! ha!!....Hillarious...!

- Nimewahi kusema mara nyingi sana hapa JF, kwamba siasa ni kipaji huwezi kubabaisha tu ukafanikiwa, mtu unaweza kujua kuandika hoja, kupanga maelezo, ukawa mwanafalsafa na the rest of the story, lakini haina maana unaweza kukurupuka tu ukawa mwanasiasa na ku-get the job done, Chadema angalieni tena washauri wenu wa siasa mlionao ikibidi fukuzeni wote hawawafai, unless mmeridhika na kukusanya ruzuku tu, lakini kama ni kuweza kutu-convince wananchi tuliochoshwa na political nonsense za bongo, basi anzeni upya ondoeni wote huko maana sio siri kuwa mko kwenye the wrong track!

-Smart politics ni kwamba, unless mna concrete hard facts ku-prove beyond any reasonable doubt kwamba Oscar sio raia, kama hamna kama mnavyoonyesha so far, basi hii ilikuwa ni ishu ya door to door huko Biharamulo, hii ishu imewahi kukumkuta Masha uchaguzi uliopita, mpinzani wake did this hakua na ushahidi kwamba Lau sio raia lakini akaenda door to door kwamba huyu kijana sio raia, na he almost convinced wananchi wote huko na hii theory.

Sasa tafuteni facts mtuletee hapa na taifa zima tuwaunge mkono mshinde Biharamulo, lakini msije JF kutafuta wachawi, mimi simjui Oscar na wala mimi sio member wa CC, dataz nilizonazo nimezisema mapema sana kwamba kulikuwa na mvutano sana huko CC, na pia nikasema hata kikao kilichopita kulikuwa na mvutano sana huko ndani kuhusu Mengi, zaidi ya hayo sijui lolote, lakini kama kwa kuwa na mawazo ya kutaka facts on the ishu kunanifanya nisiaminiwe tena JF, sawa sawa hilo sina tatizo kulikubali. Ila ninaomba kuwakumbusha Chadema na wapenzi wake wote hapa Jf, siku mtakapokuwa serious na sisi wananchi tutawachukulia serious vile vile, lakini hatuwezi kugeuza majungu kuwa facts za kisheria na kuharibu career za wananchi wanaotaka kujitolea kuendeleza taifa letu, niansema hivi ninaridhishwa sana na CV ya Oscar, kijana tena msomi huyu anaweza kuwa ni agent of change, JF tuwafagilie wagombea kama huyu bila kujali anatoka chama gani,

- Halafu it about time sasa mkatuambia mgombea wa Chadema ni nani na Cv yake ili tuichambue pia, si hii ni JF kumkoma nyani, au?

Respect.

FMEs!
 
- Kujitoa? Too early for that, sasa labda tusubiri majbu yake maana that is what demokrasia requires, yaani dual process Chadema wamelalamika Oscar na CCM watajibu, ndipo tutaweza kuona ukeli ulipo maana hii ni JF ukiweza kutudanganya hapa basi wewe huba mfano.

- Binafsi nimeamua kusubiri majibu ya Oscar na CCM, ndio nitaendelea na huu mjadala. CCM najua kwamba walijadili sana hii ishu mpaka suiku wa manane na kuishia kumpitisha, sasa kweli huko kwenye kura za maoni hakuna aliyeshituka? Chadema wamedanganywa na mtu mbaya sana maana kama jamaa ni raia, basi atakuwa mshindi tu bila ubishi, halafu sijui tutaambiwa nini this time!

Later!

Respect.

FMEs!


Mkuu FMES,

Mwendelezo wa hii ahadi vipi? au kama kama?
 
Jamani jibu la kueleweka kuhusu utata wa Mukasa ambaye alibatizwa mara moja jina la Rwegasira?
 
FMES anazo data za kwanini walikesha hata hawakulala kwao. Kama kweli FMES una mapenzi na nchi hii sema yote. otherwise unaniyeyusha kinoma.

Quote; Selous:Mkuu FMES,

Mwendelezo wa hii ahadi vipi? au kama kama?


- Kinachokufurahisha ni ligi tu, na kuvuruga vichwa vya members humu as much as you can it makes you happy, it makes your day and then unageuka na kua kichanga wa JF. Umesema unamjua sana Oscar, alivyozaliwa, familia yake ilivyofika huko Misenyi, sasa wakati ni huu tueleze unachojua hamna lolote ni ile ile tabia ya kuvuruga vuruga watu vichwa hapa,

- Ninasema tena Oscar, anaonekana ni agent of change na JF tuwakumbatie wagombea wana namna hii kwa sababu hata wakikosea ni rahisi kwa sisi wananchi kuwaingia vichwani mwao, wapewe nafasi ya kutuongoza, huyu ni msomi tena kijana JF we should never be a part of kuwakatisha tamaa vijana wasomi, tuwahukumu kutokana na matendo yao kwenye hili la kumshambulia huyu kijana bila facts, we are wrong JF,

- Heshima kwa The rule of law, maana yake sio heshima kwa majungu na politics of desparations, na kila mwananchi hata kama ni mgombea wa siasa au kiongozi wa siasa wana haki sawa na wengine wote ya kuwa afforded nafasi ya kujitetea wanapotuhumiwa na uvunjaji sheria ya jamhuri, Chadema wafukuzeni washauri wenu wote huko wa kampeni na siasa, kwa sababu hawawezi kuwasiaida na mawazo kama haya ya kuwatenga vijana wote wasomi na makini eti kwa sababu tu wanagombea under CCM.

- Investing in uraia wa Oscar, kwenye kampeni za Biharamulo ni a wrong political strategy, eti kugomea uchaguzi nayo pia ni childish strategy Wa-Tanzania ifike wakati tuachane na hizi politics za kuwekeza kwenye majina kwa sababu ndizo zimetufikisha hapa tulipo yaani backwards, tiujifunze kuwekeza kwenye sound policies!

Respect.

FMEs!
 
Mzee Mwanakijiji unasema eti CCM ni chama makini; kwa hiyo hakiwezi kumteua Mgombea ambaye si raia! Inaonekana wewe si Mzee sana, au umesahau kwamba CCM mwaka wa 1993 ilimteua Azim Premji wa Kigoma-Ujiji kugombea mara tu Tz ilipoingia ktk Mfumo wa Vyama vingi vya Siasa. CHADEMA kilimsimamisha Walid Kabourou. Awali Premji alishinda kwa margin kidogo na Chadema kilikwenda Mahakamani kueleza dosari zilizojitokeza katika kampeni, zikiwa ni pamoja na kwamba Premji alikuwa sio Raia halali wa Tz.

Uchaguzi ulitangazwa na Mahakama Kuu kwamba ni batili kutokana na Premji kutokuwa Raia, pamoja na irregularities nyingine. Licha ya kwamba Azim Premji alizaliwa Tanzania, wazazi wake walikuwa wahamiaji. Sheria inatamka kwamba ni lazima mtoto kama huyo, anapofikia umri wa miaka 18 ajiandikishe rasmi kama raia wa Tz na aukane uraia wa awali wa wazazi wake.

Maelezo yaMag3 kwamba baba yake huyu Mgomgea wa CCM, yaani Oscar Rwegasira/? Mukasa alikuwa mfanyakazi ktk wilaya za Biharamulo na Ngara siyo jibu. Inawezekana ni Mganda na si Mtanzania. Kama mtoto wake hajajiandikisha rasmi na kuomba uraia wa Tanzania, na kuukana wa Uganda wa kuzaliwa, basi siyo Raia wa Tz na hawezi kugombea Ubunge.

CCM imekosea kumteua na imwondoe, badala ya kujiaibisha kwa kukiuka Sheria iliyoitunga yenyewe wakati wa Mfumo wa Chama Kimoja. Na wewe Judge Makame, Mwenyekiti wa NEC usiendelee kujiaibisha kwa kutotoa uamuzi. Thibitisha kuwa wewe ni mtu usiyependelea CCM au chama chochote cha siasa kwa kutamka huyo Rwegasira ni mgombea batili endapo sio Raia wa Tz. Shame on you if you don't.
 
Ni kweli Mgombea wa Biharamulo si Mtanzania, lakini kwa vile ni mgombea wa CCM, sheria zitabadilishwa! CCM Daima!
 
Now Look at this theory hapa chini ili uone hili starved information nation linavyohangaika na habari:-
1. Maelezo yaMag3 kwamba baba yake huyu Mgomgea wa CCM, yaani Oscar Rwegasira/? Mukasa alikuwa mfanyakazi ktk wilaya za Biharamulo na Ngara siyo jibu.

2. Inawezekana ni Mganda na si Mtanzania. Kama mtoto wake hajajiandikisha rasmi na kuomba uraia wa Tanzania, na kuukana wa Uganda wa kuzaliwa, basi siyo Raia wa Tz na hawezi kugombea Ubunge.

3. CCM imekosea kumteua na imwondoe, badala ya kujiaibisha kwa kukiuka Sheria iliyoitunga yenyewe wakati wa Mfumo wa Chama Kimoja. Na wewe Judge Makame, Mwenyekiti wa NEC usiendelee kujiaibisha kwa kutotoa uamuzi. Thibitisha kuwa wewe ni mtu usiyependelea CCM au chama chochote cha siasa kwa kutamka huyo Rwegasira ni mgombea batili endapo sio Raia wa Tz. Shame on you if you don't.

- Sasa JF ni taasisi ya great thinkers, tizama charges hapo juu dhidi ya Mukasa na verdict humo humo, pamoja jury kwanza anasema inawezekana, meaning kwamba hajui anachosema, halafu anasema kama hajajiandikisha, and then anakuja na strong verdict pamoja sentense against CCM na Oscar, na this ni kutoka JF great thinkers!

Mungu Aibariki Tanzania.

FMEs!
 
1. Kuna watu walinotisi mara moja mabadiliko ya kutoka kutumia jina la "Mukasa" kwenda kwa "Rwegasira"... well

2. "Baada ya kubaini hilo na kufuatilia uhamiaji na kwingineko, wamebaini kwamba wazazi wake mgombea huyo walingia nchini mwaka 1971 wakitokea Bunyoro nchini Uganda na kuishi eneo la Misenyi," alidai Mrema.

3. Alidai kuwa mgombea huyo wa CCM, alizaliwa Uganda mwaka 1970 na si katika kijiji cha Rukalagata Biharamulo kama anavyodai.


- Wazazi wa Oscar walihamia Tanzania mwaka 1971, na in Six years tayari Baba wa Oscar alishaji-establish mpaka kufikia kuwa ofisa mkubwa sana serikalini yaani local govmnt, I mean sijui the facts lakini logically does this make any sense?

Respect.

FMEs!
 
Mzee Mwanakijiji unasema eti CCM ni chama makini; kwa hiyo hakiwezi kumteua Mgombea ambaye si raia! Inaonekana wewe si Mzee sana, au umesahau kwamba CCM mwaka wa 1993 ilimteua Azim Premji wa Kigoma-Ujiji kugombea mara tu Tz ilipoingia ktk Mfumo wa Vyama vingi vya Siasa. CHADEMA kilimsimamisha Walid Kabourou. Awali Premji alishinda kwa margin kidogo na Chadema kilikwenda Mahakamani kueleza dosari zilizojitokeza katika kampeni, zikiwa ni pamoja na kwamba Premji alikuwa sio Raia halali wa Tz.

Uchaguzi ulitangazwa na Mahakama Kuu kwamba ni batili kutokana na Premji kutokuwa Raia, pamoja na irregularities nyingine. Licha ya kwamba Azim Premji alizaliwa Tanzania, wazazi wake walikuwa wahamiaji. Sheria inatamka kwamba ni lazima mtoto kama huyo, anapofikia umri wa miaka 18 ajiandikishe rasmi kama raia wa Tz na aukane uraia wa awali wa wazazi wake.

Maelezo yaMag3 kwamba baba yake huyu Mgomgea wa CCM, yaani Oscar Rwegasira/? Mukasa alikuwa mfanyakazi ktk wilaya za Biharamulo na Ngara siyo jibu. Inawezekana ni Mganda na si Mtanzania. Kama mtoto wake hajajiandikisha rasmi na kuomba uraia wa Tanzania, na kuukana wa Uganda wa kuzaliwa, basi siyo Raia wa Tz na hawezi kugombea Ubunge.

CCM imekosea kumteua na imwondoe, badala ya kujiaibisha kwa kukiuka Sheria iliyoitunga yenyewe wakati wa Mfumo wa Chama Kimoja. Na wewe Judge Makame, Mwenyekiti wa NEC usiendelee kujiaibisha kwa kutotoa uamuzi. Thibitisha kuwa wewe ni mtu usiyependelea CCM au chama chochote cha siasa kwa kutamka huyo Rwegasira ni mgombea batili endapo sio Raia wa Tz. Shame on you if you don't.
Je kuna uwezekano wa kutumia hiyo kwa Rostam?
 
FMES mbona hii umeivali njuga hii kitu kuna siri unaijua ambayo sasa unaogopa itatoka nje ? Si kawaida yako mkuu kukaza buti namna hebu butafute sirini kwanza tuseme maana niko Bukoba nikupe yaliyopo hapa.
 
FMES mbona hii umeivali njuga hii kitu kuna siri unaijua ambayo sasa unaogopa itatoka nje ? Si kawaida yako mkuu kukaza buti namna hebu butafute sirini kwanza tuseme maana niko Bukoba nikupe yaliyopo hapa.


Mkuu tupe yanayo jili huko, hata hivo hiki kigugumizi chanini? mbona hatuambiwi ni ama si raia wa bongo kwa mjibu wa sheria?

Kwanza kwa mtu wa kawaida utaanza kustukia hata wasifu wa mgombea, kujua kwamba ulikuwa una kitu unakifukia, ulijikita zaidi kueleza wasifu wa baba yake alivokuwa ofisa wa serikali as if yeye ndo mgombea! why all those?

We need our law to stand firm!
 
FMES,

..kwa kweli nimechanganyikiwa sasa.

..huyu jamaa kwenye kura ya maoni si alikuwa Oscar Mukasa? sasa kwanini usiku wa manane CCM-Central Committee wambatize kuwa Oscar Rwegasira?

..hivi taratibu za kubadilisha jina toka Oscar Mukasa mpaka Oscar Rwegasira zimefuatwa?

..nadhani kabla hata ya kwenda kwenye uraia wa huyu bwana hilo la kubadilisha majina lazima lishughulikiwe kwanza.
 
FMES,
..huyu jamaa kwenye kura ya maoni si alikuwa Oscar Mukasa? sasa kwanini usiku wa manane CCM-Central Committee wambatize kuwa Oscar Rwegasira?

JK unataka kununua vita na mzee wa sauti? FMES anadai CCM ni makini sana wanajua wanachokifanya ..... wakati mwingine huwa anapenda kukimbia ukweli!
 
Rwagubiri issue iko hivi , hakuna anayempinga msomi wa Kitanzania kama angalikuwa Mtanzania msomi na kijana kama Oscar.Issue si kwamba anagombea CCM ila nataka kusema kwamba Oscar ni opportunitst ambaye hatakuwa namsaada kwa Taifa .Ana tabia za kiganda kwisha ama kinyarwanda kwamba nia yake sasa inaelekea kutimia .Huyu kijana ni mwajiriwa pale Morogoro na shule yake inakubalika lakini Oscar kama kuna mtu anabisha aje asema kadi ya Chadema aliirudisha lini na kwa nini .Tunajua walitumwa watu akiwemo Kamara walimpa live kwamba arudishe kadi na kuingia CCM na wao watachuua jukumu la kumsaidia . Naombeni wana JF wote mjue kwamba Oscar aliitwa Ikulu na aliongea na JK kwa saa moja nzima na ndipo akaenda straight Jimboni.Leo tunalia kwamba si raia lakini nataka mjue kwamba pamoja na kwamba tunataka haki itendeke JK anajua na anatarajia Oscar Mukasa kushinda kwa kuwa ana baraka zake na mambo ya Uraia ni kupoteza muda atakuwa cleared na mtegemeeni baadaye kushika uwaziri .Yangu ni hayo endeleeni kubisha lakini mtaona baadaye .Niko kwenye meli naelekea Bukoba
 
Degauche 2008 hapo juu umeuliza kama interpretation yangu kuhusu uraia ingeweza kutumika kuhusu Rostam Aziz, Mbunge wa Igunga!

Nielewavyo, huyu gabachori alizaliwa huko Tabora. Wazazi wake pia walizaliwa Tanganyika. It is unfortunate for us. Labda tutafute evidence kwamba ana uraia mwingine kama Uajemi n.k. Angekuwa amekiuka sheria ya uraia ya sasa inayokataza dual citizenship.
 
Kwenye siasa, chama au mgombea hujitahidi kuonyesha tabia njema zaidi wakati wa uchaguzi. Kwa hiyo kama tukichora grafu ya tabia njema za wanasiasa au vyama vya siasa basi kilele cha grafu hiyo kitakuwa siku ambazo kulikuwa na uchaguzi.
Aina ya mijadala inayochukua kipaumbele katika chaguzi zetu inanifanya nijiulize, je, ni kweli wanasiasa wetu wanatambua mahitaji ya jamii?
Chaguzi zimejaa malumbano ya kuzomeana, kurushiana mawe, kuchimbachimba mgombea gani hajakamilisha nakala gani ili awekewe pingamizi, kulumbana juu ya nani amuachie nani kugombea n.k
Nilitegemea kipindi hiki kiwe fursa kwa wananchi wote wa Tanzania kuielewa kwa ukaribu jiografia ya Biharamulo, matatizo yanayowakabili watu wake na jinsi kila chama/mgombea kilivyojidhatiti kuyatatua matatizo hayo. Badala yake, kwa mara nyingine tena, wananchi wanaanza kusikia malumbano kama ya Mbeya,Tarime,Busanda n.k
Je, katika siasa za Tanzania kuvutanavutana bila kuzungumzia sera ndio inaonekana tabia njema zaidi? Na kama hivyo ndivyo ilivyo, je, tunategemea maendeleo yaje kama mikate inayoanguka toka mbinguni?
Ni vyema mijadala mingi ikazunguka kwenye sera na mikakati endelevu.
ZeMarcopolo,
Nadhani huifanyii Taifa lako haki kwa comment hii.
i) Malumbano ya kisiasa wakati wa uchaguzi ni sehemu, process ya kumtambua mgombea mzuri. Hii haifanyiki tu Tanzania, hata nchi zote kubwa kuchimbiana, na ni sehemu muhimu ya kupata credibility na trustworthiness ya Wagombea. Hivyo si suala la maendeleo tu. Wakati wa Utawala wa Chama kimoja tulioshiriki tulielezwa tusilumbane, bali tuzungumzie shida. Kwa miaka zaidi ya 45 hiyo hali haijatokea. Hivyo si Comment ya namna hii haina basis ya kisayansi kuhukumu kuwa maendeleo hayako kwa sababu ya aina ya malumbano yaliyoko wakati wa Kampeni.
2) Katika Kampeni kama unafuatia vizuri, mfumo wa constructive kampeni ni kukosoa sera ya Chama Tawala au vyama vilivyoko kwenye kinyang'anyiro ikiwa ni pamoja na kuchambua utekelezaji wa Sera hizo kwa upande wa Chama Tawala ambao ndio wenye jukumu la kutumia kodi ya Wananchi kwa maendeleo yao. Uchambuzi huo sio malumbano, bali ni analysis muhimu kuona kuwa chama kitakachochaguliwa kinaweza kuwa na sera nzuri kwenye makaratasi, lakini sera na Ilani hizo zimetumika kwa kiasi gani katika kuwaletea maendeleo wananchi. Hoja za aina hii, zinawafumbua wananchi macho, wafanye tathmini ya kweli kwa kuwapatia silaha yaani data muhimu ambao kwa hali yao ya vijijini hawawezi kuipata kama si kwa njia ya mikutano hiyo ya hadhara. Mwanasiasa wa kweli anafahamu umuhimu wa hoja ya aina hiyo na hawezi kuipuuza hata kidogo.
3)Mwanasiasa yeyote makini, hataishia katika kutoa critique ya utekelezaji wa sera za Chama Tawala, ataenda mbele kuchambua mahitaji muhimu ya wananchi, na tofauti na chama kingine chama chake kitafanya nini kuondoa au kupunguza matatizo hayo. Hivyo kwa mtu yeyote asiyefuatilia kwa undani hotuba za jukwaani na kusoma tu sehemu ya mambo yanayorekodiwa akapata tu taarifa ya kurushiana mawe, au sura ya kuwasema watu na au hata kutukanana kunakoripotiwa ni sehemu ndogo sana ya matukio yaliyoko kwenye Kampeni. Haiwezekani Mwanasiasa mahiri asimame jukwaani kwa zaidi ya dakika 40 au saa moja, aishie kutukana tu au kulumbana tu. Nadhani ZeMarcopolo kuna haja ya utafiti wa kina wa siasa za Tanzania kuliko kui paint negatively kama ulivyofanya. Ninayasema haya from field experience, sasa kama kuna experience tofauti ni vema ukatueleza concrete cases ili tuzichambue lakini generalization za aina ya hoja yako ni hatari hata kwa wanaofuatilia hoja katika JF ambako kwa wengi ni sehemu muhimu ya kujifunzia pia. Let us do justice to ourselves and to our nation.
4) Wana JF naomba radhi kwa muda nilipotea kwenye mtandao kwa vile nilikuwa niko nje ya Nchi kuhudhuria SADC-Parliamentary Forum ( Bunge la Mpito la SADC). Sasa niko hewani tena. Nawashukuru sana kwa michango yenu.
 
Back
Top Bottom