Mkuu FMEs, naungana na Selous, kama una mapenzi ya kweli na TZ, can you come clean ? Kwa nini tuendelee kukuamini kama hutafanya hivyo ?
- Mkuu mbona unabadilika tena, mara ngapi umewahi kusema mimi ni mmoja wa mafisadi, kwa sababu tu nina mawazo tofauti na yako? Na huyu unayem-support ameandika mara nyingi sana hapa kwamba dataz zangu huwa ni za uongo, sasa leo eti zimegeuka kuwa ni za kweli, kisa na mkasa mnataka kumsulubu huyu kijana, Mukasa ndivyo tulivyo hatuwezi kuwa tofauti hata iweje ndivyo tulivyo.
- Mkuu Mag3, sio siri kwamba you are a very smart man jinsi unavyo-move back and forth ndani ya hii forums, lakini sio wote sisi ni wajinga, kuna tunakuona kama ulivyo na siku zote tunajaribu kukupa heshima kwenye ukweli na hoja za kimapinduzi, lakini sometimes na wewe unazidisha mipaka, huwezi kuivalia njuga hii ishu bila ya kuwa na facts, na wakati umefika ni lazima ukubali waliokupa hii ishu na wewe hamna facts, au kama mnazo hamjazitoa wazi tukaziona, kwa hiyo sio haki kumuhukumu Oscar.
- Respect kwa The rule of law, ni pamoja na guarantee ya a due process kwa kila mwanachi anapotuhumiwa kuvunja sheria, ni lazima apewe nafasi ya kujieleza na kujibu ipasavyo na ikibidi jamhuri inatakiwa impe wakili wa kumsaidia, Oscar Mukasa Rwegasira ni raia mwenzetu mpaka sheria itakapotuambia otherwise, hatuko hapa ku-demand creation ya taifa la wenda wazimu, yaani mwananchi mmoja akikurupuka huko kuwa huyu sio raia basi ikishafika tu hapa JF, basi huyoooo sio raia, CCM imeshikwa pabaya!, wamezoea hao hata Rostam sio raia!, hiyo sio the respect kwa the rule of law, huo ni wenda wazimu na chama chochote cha siasa kinachochochea tabia kama hizi ni lazima tukiogope sana kama ukoma!
- Kama kuaminika hapa JF ni lazima kukubaliana na mawazo yako tu, then una haki zote za kuacha kuniamini, yaani unasema mmeanzisha hii ishu kwa kutegemea dataz kutoka kwangu? Eti kwa sababu sujui yote yaliyojaidliwa kwenye kikao cha CC ambacho mimi sio member, sasa ninatakiwa nisiaminiwe hapa JF, na kwamba kuna something ninaficha ambacho wewe uki-connect dots zako unapata jawabu kwamba Oscar sio raia na mimi ninahusika kuficha ukweli, kweli mkuu huoni kwamba haya mawazo ni mufilisi kwa member kichwa kama wewe licha tu ya kuwanayo, lakini hata kusema hadharani hapa ni aibu! Sasa mimi ndiye mchawi wenu, siku zote msopoweza kupata your way na CCM, basi FMEs ndiye mchawi, pole sana mkuu sina cha kukusaidia!
Asante sana Selous, umenifungua macho na sasa naweza ku"connect the dots". Nilikuwa najiuliza kwa nini kikao mpaka usiku - well, nilisema tangu mapema kuwa hili jina Mukasa/Rwegasira lina wingu zito. Wazungu husema "covering one's behind" na yanikumbusha watergate - kweli CCM si mchezo. Lakini vipi wataweza kufuta documents zote za nyuma ? mpaka airline tickets ? Kuna mahali watakwama tu ila kwa kuwa ni wahitimu wa kuhalalisha ufisadi, nani wa kuwazuia.
CCM ni Chuo cha Mafisadi kweli kweli !!
Kama Abdulrasul Chakaar sasa ni Mb. Mh. Rostam Aziz
Kimzuie nini Oscar Mukasa kuwa Mb. Mh. Oscar Rwegasira.
Jaji Makame upooooo?
- Haya ndio maneno ya kawaida sana hapa ukitaka fame ya temporary hapa JF, lakini inapokuja kwenye ukweli wake siku zote ni tatizo, na matokeo huwa wananchi kukatishwa tamaa, kwa sababu look sasa hivi mnajaribu kutuaminisha kwamba mna ishu nzito na huu uchaguzi wa Biharamulo kuhusu uraia wa Oscar, matokeo wananchi wengi wata-invest in this kusadikika theory kama unavyoona kwenye hii thread, tayari wengi wameshanasa bila facts, maana ukisema wewe Mag3 kwa wengi wetu humu JF huwa ni kweli tu, halafu tutakuja kuambiwa jinsi CCM ilivyozoea kuwakumbatia wageni, tizama Ulimwengu ni mgeni, Rostam ni mgeni, Idd Simba ni mgeni, halafu wameiba shahada hawa mbona walioandikisha ni laki moja waliopiga kura 50,000 tu CCM wameiba, siku imekwisha wananchi wajinga ndio waliwao, hakuna responsibility wala uwajibikaji wa hela zetu nyingi za ruzuku wanazopewa Upinzani, ila ni CCM tu ndio waizi na wakumbatiaji wageni.
- Mmerukia habari ya uraia wa Oscar, sasa bado ni burden yenu kuleta ukweli wote kwa nini mnamtuhumu huyu kijana kuwa sio raia, tunajua alizaliwa Uganda alikuja Tanzania mwaka 1977, okay wapi ushahidi wa kisheria maana kuzaliwa kwa mwananchi lazima kuthibitishwe na sheria, ooooh FMEs anajua huyu anaficha maana kikao kimefanyika mpaka usiku wa manane, huyu FMEs haaminiki kabisa ni fisadi!, really? vipi wewe unayeaminika ushahidi uko wapi? abanwe FMEs tu ndio anajua, Bwa! ha! ha! ha!!....Hillarious...!
- Nimewahi kusema mara nyingi sana hapa JF, kwamba siasa ni kipaji huwezi kubabaisha tu ukafanikiwa, mtu unaweza kujua kuandika hoja, kupanga maelezo, ukawa mwanafalsafa na the rest of the story, lakini haina maana unaweza kukurupuka tu ukawa mwanasiasa na ku-get the job done, Chadema angalieni tena washauri wenu wa siasa mlionao ikibidi fukuzeni wote hawawafai, unless mmeridhika na kukusanya ruzuku tu, lakini kama ni kuweza kutu-convince wananchi tuliochoshwa na political nonsense za bongo, basi anzeni upya ondoeni wote huko maana sio siri kuwa mko kwenye the wrong track!
-Smart politics ni kwamba, unless mna concrete hard facts ku-prove beyond any reasonable doubt kwamba Oscar sio raia, kama hamna kama mnavyoonyesha so far, basi hii ilikuwa ni ishu ya door to door huko Biharamulo, hii ishu imewahi kukumkuta Masha uchaguzi uliopita, mpinzani wake did this hakua na ushahidi kwamba Lau sio raia lakini akaenda door to door kwamba huyu kijana sio raia, na he almost convinced wananchi wote huko na hii theory.
Sasa tafuteni facts mtuletee hapa na taifa zima tuwaunge mkono mshinde Biharamulo, lakini msije JF kutafuta wachawi, mimi simjui Oscar na wala mimi sio member wa CC, dataz nilizonazo nimezisema mapema sana kwamba kulikuwa na mvutano sana huko CC, na pia nikasema hata kikao kilichopita kulikuwa na mvutano sana huko ndani kuhusu Mengi, zaidi ya hayo sijui lolote, lakini kama kwa kuwa na mawazo ya kutaka facts on the ishu kunanifanya nisiaminiwe tena JF, sawa sawa hilo sina tatizo kulikubali. Ila ninaomba kuwakumbusha Chadema na wapenzi wake wote hapa Jf, siku mtakapokuwa serious na sisi wananchi tutawachukulia serious vile vile, lakini hatuwezi kugeuza majungu kuwa facts za kisheria na kuharibu career za wananchi wanaotaka kujitolea kuendeleza taifa letu, niansema hivi ninaridhishwa sana na CV ya Oscar, kijana tena msomi huyu anaweza kuwa ni agent of change, JF tuwafagilie wagombea kama huyu bila kujali anatoka chama gani,
- Halafu it about time sasa mkatuambia mgombea wa Chadema ni nani na Cv yake ili tuichambue pia, si hii ni JF kumkoma nyani, au?
Respect.
FMEs!