Biharamulo: Kampeni, kura na matokeo!

Passport yake ina jina la Oscar Rwegasira Mkasa na hata kwenye fomu ya tume amejaza majina yote matatu.

Suala la uraia wa Oscar ni jambo ambalo chadema wamekuta linazungumziwa kila kona ya biharamulo. Katika kura za maoni za ccm, Oscar alisema na ilirekodiwa na kurushwa na Biharamulo Cable TV kwamba yeye amezaliwa wilaya ya Biharamulo. Kijiji alichosema amezaliwa wanakijiji wanakataa na kusema wazazi wake sio watu wa hapo bali ni wahamiaji, tena wa miaka ya karibuni (around late 1980s) wakati Oscar ameshazaliwa. Oscar anaweza kuwa raia wa Tanzania lakini amelikoroga mwenyewe. Utata kwamba amezaliwa wapi ni yeye mwenyewe ameuanzisha kwa kutokuwa makini. Na jinsi alivyojaza fomu (at least iliyokuwa available to the public) kumeibua maswali mengi kuliko majibu.

Barua ya kutupilia mbali pingamizi la chadema ilipitia au ilitengenezwa Chato na siyo Biharamulo mjini kwenye halmashauri na ofisi za mkurugenzi. Kwani watu walioko Chato waliweza kuisoma na kuivujisha kabla haijafika biharamulo. Hapa kuna maswali mengi ya kujiuliza kwanini?

Chadema wameshauriwa na mawakili pamoja na ccm "anti-oscar" wang'ang'anie issue ya kutojaza fomu sawasawa. Kimsingi fomu ni moja na siyo mbili. Mkurugenzi kusema amepokea fomu mblili tofauti anakiri kwamba ama ameshindwa kazi yake kwa kushindwa kuhakiki hizo fomu (kipengele cha tatu hakikujazwa and it was so obvious) au ameshirikiana katika kugushi fomu alizokuwa nazo yeye kwenye ofisi yake.
 

Mkuu wewe ni mtu makini sana katika hoja zako lakini katika hili nadhani inabidi ufanye utafiti zaidi. WABONGO SIKU HIZI WAMEAMKA MKUU: Personally najua vijana kama 3 wamemaliza shule zao pale mlimani kwenye 200/2004 sasa hivi wako ukingoni mwa PhD zao na bado hata miaka 30 hawajafika. Mkuu na hawa siyo watoto wa mafisadi...ila ni wabongo wenzetu wamehaingaika kama sisi. Sema tuu ni kujiwekea priorities na kujua/kupata right channels.Kwa hiyo PhD kabla ya 30 inawezekana kabisa. Ushauri wangu..kama uko nje mwanangu beba box na ule kitabu otherwise ukija bongo na associate degree yako ya community college ni wachache watakaobabaika eti umesoma majuu (no pun intended bro!)
 


mkono wa magufuli upo hapo.......
 

Ndohomayo!!
Nimesikia mkubwa wangu ushauri wako, ngoja nijitahidi tahidi kubeba beba box na kukaangalia ka community college.
 
Naam!


Kwanini kuna suala la Uhamiaji wakati yeye ni Mtanzania?


naam!


Wanavyodai wabishi wa Biharamulo ni kwamba alitaka ku prove hamna records uhamiaji inayosema aliingia tanzania kutoka uganda katika huo mwaka aliotajwa na chadema kwamba ndio aliohamia tanzania.

Mimi kwangu halina mantiki kwakuwa sidhani wahamiaji haramu wanapitiaga ofisi za uhamiaji. Lakini kama nilivyosema hapo awali Oscar anajilipua yeye mwenyewe na issue ya uraia kwa kutokuwa makini. Kwa mfano, kwenye uzinduzi wa kampeni (ingawa alikuwa haruhusiwa kufanya kampeni) mama yake inasemekana alikuwa mgonjwa alishindwa kufika, basi yeye alimyanyua mwanamke mwingine na kudai ndiyo mama yake mzazi wakati watu wanafahamu huyo sio mama yake mzazi. Ilileta miguno no minong'ono kwanini anadanganya wakati si lazima mama yake awepo pale? Watu wanajiuliza anaficha nini?
 
Mtanzania,
Haya ya kubadili majina naona yameshamiri sana CCM. Mimi yule mbunge wa Bukoba aliyepewa uwaziri mdogo wa mambo ya ndani miaka yote nikimjua kama Suedi hata wakati alipokuwa UN Geneva. Mara ghafla vin boom akageuzi jina na kupata ubunge wa CCM na sasa ni waziri mdogo. Labda na mimi nitabadilisha jina nijiunge na CCM:-
 

mmh.. sasa nani anajukumu la kuthibitisha kuwa huyo ni mama yake au si mama yake? Yeye akisema ni mama yake, watu wengine wanaweza vipi kusema siyo? Wao wanaushahidi gani kuwa si mama yake?
 


Sasa jamani huyu kaanza kuchezea akili za watu hata kabla ya kutinga ndani ya jumba, sasa akisha fika huko na akapewa meza kuu kama alivo ahidiwa? si ndo atasaini mikataba ya kuuza nchi uvunguni? make yeye inaonekana ni voda fasta kwa kwenda mbele! Loooo.. utasemaje huyu ndo mama yangu mzazi ili hali mama yako yu hai tena mgonjwa?


 
mmh.. sasa nani anajukumu la kuthibitisha kuwa huyo ni mama yake au si mama yake? Yeye akisema ni mama yake, watu wengine wanaweza vipi kusema siyo? Wao wanaushahidi gani kuwa si mama yake?
Mzee mwana kijiji kuhusu suala la kumjua mama ushahidi unaweza kupatikana tatizo angekuwa ni baba hilo ndiyo lingekuwa tatizo kuthibitisha kama kweli ni baba yake.
 

Jasusi,

Sidhani kama ni CCM tu, nafikiri ni kwenye siasa ambako unategemea kura za wananchi.

Wale ambao hawatumii majina ya ukoo makazini ndio wanajikuta wanahitaji kuyaingiza dakika za mwisho. Kule Kyela Kasyupa aliwahi kushinda mara mbili bila kuhitaji kutumia jina lake la Mwa.. Huenda ni woga tu.
 

- Mkulu Nyumbu, ahsante sana kwa huu ujumbe, at least sasa tuna muongozo, kama ninakuelewa vizuri ni kwamba kuna uzembe umefanywa na CCM katika kujaza fomu za mgombea wao, huu uzembe ni not punishable by our laws of the land niko sawa au ninakosea wakuu?

- Na je tunakubaliana kwamba la uraia sio ishu tena hapa au Chadema wamekata rufaa on uraia grounds?

FMEs!
 


M'Kijiji,

Kuna tetesi kwamba aliyekuwa Mbunge wa Busanda (marehemu) hakuwa raia wa Tanzania. Mtu mmoja ninayemfahamu aliniambia kwamba, alipokwenda kwenye msiba wa marehemu huyo, ndugu zake wengi waliokuwa hapo walithibitika kuwa raia wa Burundi, hata lugha waliyokuwa wakiongea ilikuwa Kirundi. Haya yalitokea Dar.

Kwa hiyo, upo uwezekano mkubwa kwamba "Rwegasira" huyu akawa kweli ni "Mukasa".

Lisemwalo lipo, kama halipo ......

./Mwana wa Haki
 

- Again ahsante sana na hizi info mkuu, ninarudia tena reading between the lines, ni kwamba kisheria Oscar ni raia wa Tanzania hilo halina ubishi na ndio maana Chadema sasa wanashauriwa kunga'ng'ania makosa ya CCM kutojaza fomu sawa sawa, je tuko pamoja wakuu au?

FMEs!
 

Watanzania walio wengi huwa hawawezi kuishi bila ujanja ujanja usio na maana. Imefika mahali watu wanafikiri unaweza kutumia shortcuts kwenye kila kitu.

Hii ni tabia mbaya ambayo lazima ilaaniwe sana. Kama ni kweli alimsimamisha mama mwingine na kusema ni mamake; huyo mimi nitamwona kama tunaandaa fisadi mwingine ambaye huko mbele anaweza kutuliza.

Ufisadi hauanzi na kuiba mabilioni, unaanza na mambo haya madogo madogo na kisha hupanda mpaka kufikia level ya akina Chenge.

Mambo kama haya sio madogo na yakiachiwa yana madhara kwa nchi.
 
Hivi kweli kinachotutatiza ni Oscar kubadili jina la uzawa? Hivi haiwezekani ikawa ni mkakati wa kumfanya mgombea wake akubalike zaidi katika jimbo atakalogombea? Inasemekana Hillary Rodham Clinton, kama feminist mkereketwa, alipoolewa hakutaka kuchukua jina la mume wake. Lakini mumewe alipotaka kugombea ugavana Arkansas aliambiwa kuwa watu wa jimbo hilo hawatamuelewa kama yeye akiwa mtu aliyeolewa, asipochukua jina la mume wake. Hillary kwa vile alitaka mumewe ashinde akabadili jina la ubini na kuchukua jina la mumewe and the rest kama wanavyosema wengine, is history. Mimi naamini kwa strategist yeyote anayetaka mgombea wake akagombee huko vijijini atajitahidi kwa kila namna kumuunganisha huyo mgombea na sehemu hiyo. Kama itabidi kubadili jina liwe la kihaya zaidi, atafanya hivyo. Kama itabidi mgombea anywe lubisi, atafanya hivyo. Kama itabidi mgombea aanze kuongea kwa lahfudh ya kihaya atafanya hivyo. Yote hayo ni katika kutafuta ushindi. Au mnataka kutuambia kuwa angebakia na jina lake la awali basi watu wasingemwekea pingamizi? Yote haya ni politics. Kwenye jina, naona kama inavyoanza kuwa kawaida yetu, tunageuza kichuguu kuwa mlima!

Amandla.......
 
Last edited:

Hillary Bowmann Clinton ndio nani huyo?
 
Touche, McCain. Kabla hajaitwa Rodham! Nitarekebisha. Nilisahau kwamba wamarekani mko wengi humu! Hasa Clintonites.

Amandla......

Rodham ndio maiden jina lake so what do you mean kabla hajaitwa Rodham? Her full name before marrying Bubba was Hillary Diane Rodham. Hilo la Bowmann limetoka wapi bana...au ushalewa mataputapu yako? Acha kumharibia Mama....Mama wa shoka huyo na unajua jinsi ninavyomzimia...oohoooo....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…