Biharamulo: Kampeni, kura na matokeo!

Biharamulo: Kampeni, kura na matokeo!

- Mkuu hebu fafanua hapo kidogo, eti Lusinde ni watu wa Congo? Kwa vipi yaani?

Respect.

FMEs!

mkuu achana naye huyu ...hajuwi kuwa kati ya makabila ambayo hata ukirudi nyuma miaka 300 iliyopita ...wagogo wamo[watanganyika halisi bila chembe ya shaka]

niwape mfano mmoja ...

wamasai wapo tanzania,kenya na sasa wanatapakaa..wengi wana ndugu pande zote ....na hata sehemu yao ya kuabudu ipo sanya juu kilimanjaro[hadi wa kenya kina saitoti huja pale kutambika]

wachagga wana asili moja na wameru,wasambaa ,wakikuyu etc

wahaya wana asili na waganda [buganda]

wahangaza [burundi,rwanda etc

wangoni...wanatoka south africa..

wamakonde ..msumbiji..

wakwere....ni mchnganyiko wa makabila yaliyotokana na wafanyabiashara walikuwa wakitoka bara kwa miguu kuja pwani wengine wakalowea..ndio wakawa wakwere,zaramo[etc].........

lets share information..

tatizo sielewi kuwa kwa nini mtanzania wa leo ambaye amezaliwa baada ya uhuru bado akose hati ya kuzaliwa.....
 
Mgobea ubunge wa Biharamulo kupitia CCM, Bwana Mukassa, ni kweli si Mtanzania. Sisi tunamfahamu vizuri na kuifahamu familia yake.Pia Ikulu ina ukweli huu kwamba si Mtanzania, ila wanazimisha kwa vile yeye ni wa CCM.

Akipita, tutapigana usiku na mchana kuwatetea wale wote wa Karagwe, Ngara, na Bukoba waliokuwa wakisumbuliwa kwamba waoni wahamiaji haramu. CCM, inatupeleka pabaya. Hata ukiwa mwizi, kwa vile uko CCM, mambo yanayooka?

Mkassa, alizaliwa Uganda na wazazi wake wakaahamia Tanzania kwenye miaka ya sabini. Kusema kweli hadi leo hii hawajaomba uraia! Inashangaza sana kwamba CCM, ina uwezo wa kuvunja sheria za nchi.

Mwenye uwezo wa kusambaza habari hizi afanye hivyo. Wambieni watu wa Biharamulo, kwamba Mukassa, si raia! Na kwamba CCM inavunja sheria na katiba ya nchi yetu. Hivi Katiba, inamruhusu mtu asiyekuwa raia kugombea Ubunge?
 
Hivi hizi habari za huyu Mtanzania na huyu si Mtanzania, huwa haziibuki mpaka pale tunapokuwa kwenye mambo ya Kula kura!?
 
Mie nilifikiri kuwa kuna thread nyingine inayozungumzia uraia wa huyu Bw. Mukassa. Mod unaionaje hii thread unaweza kuiunganisha na ile nyingine..
 
Mgobea ubunge wa Biharamulo kupitia CCM, Bwana Mukassa, ni kweli si Mtanzania. Sisi tunamfahamu vizuri na kuifahamu familia yake.Pia Ikulu ina ukweli huu kwamba si Mtanzania, ila wanazimisha kwa vile yeye ni wa CCM.
QUOTE]

MUTEKANGA,
Akipita hakuna haja ya kupigana.
Kwani OBAMA alizaliwa wapi?
Mahali pa kuzaliwa si tatizo nadhani.
 
duh! nilipoona ni-breaking news, nikadhani tume ya uchaguzi imetoa tamko kumbe yale yale. Sawa Mkuu kwa kutoa ushahidi wako, ila hili suala ni la kisheria zaidi, so, kama unaushahidi wasilisha panapo husika. By the way, tume ya uchaguzi bado haijajibu rufaa ya Chadema?
 
Mgobea ubunge wa Biharamulo kupitia CCM, Bwana Mukassa, ni kweli si Mtanzania. Sisi tunamfahamu vizuri na kuifahamu familia yake.Pia Ikulu ina ukweli huu kwamba si Mtanzania, ila wanazimisha kwa vile yeye ni wa CCM.

Akipita, tutapigana usiku na mchana kuwatetea wale wote wa Karagwe, Ngara, na Bukoba waliokuwa wakisumbuliwa kwamba waoni wahamiaji haramu. CCM, inatupeleka pabaya. Hata ukiwa mwizi, kwa vile uko CCM, mambo yanayooka?

Mkassa, alizaliwa Uganda na wazazi wake wakaahamia Tanzania kwenye miaka ya sabini. Kusema kweli hadi leo hii hawajaomba uraia! Inashangaza sana kwamba CCM, ina uwezo wa kuvunja sheria za nchi.

Mwenye uwezo wa kusambaza habari hizi afanye hivyo. Wambieni watu wa Biharamulo, kwamba Mukassa, si raia! Na kwamba CCM inavunja sheria na katiba ya nchi yetu. Hivi Katiba, inamruhusu mtu asiyekuwa raia kugombea Ubunge?

Breaking news wapi mkuu wakati hili lilisha jadiliwa kwa urefu na upana na bado hakuna ushahidi uliotolewa? Kama una ushahidi weka hapa au kama kuna jipya weka hapa. Mimi sioni hapa breaking news iko wapi. Aaaaarrrgh watu mnaboa sasa. USHAHIDI PLEASE!!!
 
MUTEKANGA,
Akipita hakuna haja ya kupigana.
Kwani OBAMA alizaliwa wapi?
Mahali pa kuzaliwa si tatizo nadhani.

Mkuu Exaud yapasa ujue kuwa kila nchi inakatiba yake na sheria yake. Huenda US hata ukizaliwa angani (kwenye ndege) ndani ya anga la US unakuwa raia. Lakini Sheria yetu ya Tz si hivyo. Kwamujibu wa sheria zetu unakuwa raia moja kwa moja pale tu wazazi wako wote wanapokuwa ni raia wa Tanzania. Endapo mzazi mmoja ni Mtz basi unapaswa kutoa kiapo cha kukana uraia wa mzazi mmoja ukishafikia miaka 18. Kama wazazi wote si raia basi unapaswa kuomba uraia kwa mujibu wa sheria. so, usilinganishe US na Tz, pia suala linalolalamikiwa hapa si mahali alipozaliwa bali wazazi kutokuwa raia wa Tz.
 
Mgobea ubunge wa Biharamulo kupitia CCM, Bwana Mukassa, ni kweli si Mtanzania. Sisi tunamfahamu vizuri na kuifahamu familia yake.Pia Ikulu ina ukweli huu kwamba si Mtanzania, ila wanazimisha kwa vile yeye ni wa CCM.
QUOTE]

MUTEKANGA,
Akipita hakuna haja ya kupigana.
Kwani OBAMA alizaliwa wapi?
Mahali pa kuzaliwa si tatizo nadhani.

Mkuu kwani sheria za uraia wa Marekani na Tanzania ni sawa? Kwanza hapa umechemsha katika tafsiri kwa sababu Obama kazaliwa Marekani na mmoja wa wazazi wake alikuwa Mmarekani sasa una linganisha nini haswa?
 
jamani kwa aliyeko B'mlo atuhabarishe yanayojiri ktk kampeni
 
CHADEMA MATATANI BIHARAMULO
Imeandikwa na Neophitius Kyaruzi, Biharamulo
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeingia matatani katika kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Biharamulo Magharibi baada ya kukiuka taratibu za kampeni, kwa kupotosha habari kwa kutumia kibonzo kinachoonesha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewakashifu wananchi wa jimbo hilo. Kutokana na hali hiyo, Mkurugenzi wa Vijana wa Chadema, Mwita Waitara anashikiliwa na polisi kwa mahojiano kuhusu tukio hilo ambalo linadaiwa kuwa na nia ya kuvuruga taratibu za kampeni kwa kutoa ujumbe ambao si wa kweli.

Kamanda wa Operesheni ya Upelelezi ambaye pia ni Mkuu wa Polisi wa Kuzuia Ghasia Tanzania (FFU), Tresphory Anaclet alithibitisha kukamatwa kwa Waitara na kuhojiwa. Viongozi wa Chadema wilayani hapa, wanatuhumiwa kushirikiana na kuondoa maelezo halisi ya kibonzo kilichotolewa katika gazeti la Sauti Huru toleo namba 34, na kuweka maelezo yao yanayoidhalilisha CCM, kukashifu wapiga kura kisha kudurufu maelezo hayo waliyopotosha na kuyasambaza katika mji wa Biharamulo na maeneo mengine.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa chama hicho, John Mnyika alikiri kupata taarifa hizo na kukamatwa kwa Waitara na kisha kuhojiwa na polisi, lakini alikana Chadema kuhusiana na tuhuma hizo huku akidai kuwa hizo ni fitina zilizotengenezwa na CCM ili kukidhalilisha chama hicho.

"Sisi ni chama makini na tunajua taratibu za uchaguzi na sheria zinazotuongoza hatuwezi kufanya upuuzi kama huo, jambo hilo litakuwa limepandikizwa na CCM ili kutudhalilisha," alisema Mnyika. Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kupitia mahojiano na wananchi mbalimbali, unaonesha kwamba magari ya kampeni ya Chadema yamekuwa yakipita mitaani na kusambaza nakala zilizodurufiwa zinazoonyesha ujumbe uliopotoshwa katika gazeti hilo.

Kwa mujibu wa mfanyabiashara maarufu mjini hapo, John Rwegasira ambaye pia ni mhamasishaji wa Kampeni wa CCM, takribani siku ya tatu sasa Chadema kimekuwa kikikodi waendesha pikipiki na kupeleka nakala za maelezo ya upotoshaji katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo. Alisema kwamba baada ya CCM kupata taarifa na kushuhudia nakala hizo, ilipeleka taarifa katika vyombo vya usalama ili suala hilo lishughulikiwe.

Naye Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema alidai kuwa fitina hiyo ya Chadema ni dalili za kutojiamini kwao katika uchaguzi huo baada ya kushindwa katika uchaguzi wa Busanda uliofanyika hivi karibuni na CCM kupata ushindi. Alisema Chadema sasa kimejaa ubinafsi na ubabaishaji ndio maana ilifikia hatua ya kutangaza chama chake cha TLP kutosimamisha mgombea wakati si kweli.

"Nataka niwaambie wananchi wa Biharamulo na Watanzania wote kwamba Chadema ni chama kilichojaa ubinafsi na ubabaishaji wa hali ya juu kwani kinataka kujifanya kiranja wa vyama vingine vya upinzani wakati kinajua wazi kimepoteza mwelekeo," alisema Mrema. Alisema kwa mwenendo unaoonekana sasa, Chadema haina uwezo wa kushindana na CCM na kunyakua majimbo, lakini imeendelea kuvishawishi vyama vingine vijitoe wakati havina uwezo na baada ya kushindwa ni ushahidi tosha. (tamati).
 
CHADEMA MATATANI BIHARAMULO

Naye Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema alidai kuwa fitina hiyo ya Chadema ni dalili za kutojiamini kwao katika uchaguzi huo baada ya kushindwa katika uchaguzi wa Busanda uliofanyika hivi karibuni na CCM kupata ushindi. Alisema Chadema sasa kimejaa ubinafsi na ubabaishaji ndio maana ilifikia hatua ya kutangaza chama chake cha TLP kutosimamisha mgombea wakati si kweli.

“Nataka niwaambie wananchi wa Biharamulo na Watanzania wote kwamba Chadema ni chama kilichojaa ubinafsi na ubabaishaji wa hali ya juu kwani kinataka kujifanya kiranja wa vyama vingine vya upinzani wakati kinajua wazi kimepoteza mwelekeo,” alisema Mrema. Alisema kwa mwenendo unaoonekana sasa, Chadema haina uwezo wa kushindana na CCM na kunyakua majimbo, lakini imeendelea kuvishawishi vyama vingine vijitoe wakati havina uwezo na baada ya kushindwa ni ushahidi tosha. (tamati).

Sasa huyu mzee jamani? kwahiyo yeye anafanya nini huko kama anajua kabisa nani mshindi? mbona asiseme chama chake ndo kitashinda? kwahiyo yeye furaha yake ni Chadema kushindwa? yaani rupia mbaya sana.
 
Huyo Mzee (Mrema) ameshachoka, hata hana la kuongea. Arudi zake kijijini kwao akapumzike.
 
Sasa Mrema nae amepoteza sifa za uanamageuzi.Astaafu tu maanake hata mimi naelekea kumchoka sasa,naeza mweka kundi moja na Mtikila na si vizuri tufikie hatua ya kufanya hivyo.
 
Taarifa tulizo nazo ni kwamba
Mhe. Yusuphuh Makamba na Pius Msekwa wameondoka Biharamulo kimya kimya. Vyanzo vyetu havijapata sababu haswa za kuondoka kwa wakuu hao wa CCM katika kipindi hiki kigumu cha kampeni.

Tulipokea pia taarifa za uhakika kuwa yule gwiji wa siasa za vichekesho Mhe Agustino Lyatonga Mrema ameanguka bafuni kutokana na msongo mkubwa na uchovu siku ya Jumamosi. Kwa sasa anaendelea vizuri kiafya. Kampeni za Mrema hapa Bihyaramulo ni kwamba "Ichagueni TLP: kama hamtaki basi chagueni CCM".
Anasisitiza kuwa CHADEMA ni adui wa demokrasia.

Haya ndiyo machache niliyo nayo mapya kutoka hapa Biharamulo.
 
itikafu za kwa mtoro zinafanya kazi hizo maana swahiba wake yule mtu wa shirkinaye alishindwa kutabiri kama ataugua

kaaazi kweli kweli
 
Taarifa tulizo nazo ni kwamba
Mhe. Yusuphuh Makamba na Pius Msekwa wameondoka Biharamulo kimya kimya. Vyanzo vyetu havijapata sababu haswa za kuondoka kwa wakuu hao wa CCM katika kipindi hiki kigumu cha kampeni.

Tulipokea pia taarifa za uhakika kuwa yule gwiji wa siasa za vichekesho Mhe Agustino Lyatonga Mrema ameanguka bafuni kutokana na msongo mkubwa na uchovu siku ya Jumamosi. Kwa sasa anaendelea vizuri kiafya. Kampeni za Mrema hapa Bihyaramulo ni kwamba "Ichagueni TLP: kama hamtaki basi chagueni CCM".
Anasisitiza kuwa CHADEMA ni adui wa demokrasia.

Haya ndiyo machache niliyo nayo mapya kutoka hapa Biharamulo.

Masikini Mrema, kweli kaishiwa du?

Chadema kazeni buti.. kwani hii ni dalili njema kwamba kwamba washindani wote wanawagwaya!
 
Kaanguka -- Duh! Vipi aliweza kusimama tena? Si arudi tu CCM? watamfadhili tu maana hawa jamaa hawawatupi kondoo wanaorudi kundini. Nasikia wana-TLP kule wamejikita Chadema kwa sababu mgombea wa TLP aliteuliwa na Mrema, na siyo wanachama!
Amwombe RA asaidie kampeni yake -- si alimtolea statement nzuri dhidi ya Mengi?
 
Mrema: (Akizinduka baada ya kuanguka bafuni) Ichagueni TLP: kama hamtaki basi chagueni CCM
Mficha ficha maradhi, kilio humfichua.
Sasa ni wakati muafaka kuvizika vyama feki
na kubaki na vyama viwili tu -
Chadema na CCM
vyenye tofauti kama mchana na usiku au mwanga na giza.
Kimoja kinawatetea wananchi
kingine kinawakumbatia mafisadi.

Back
Top Bottom