Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lakini pamoja na kwamba CCM itashinda kule kutokana na incumbency
- Heshima mbele mkuu, hivi huko Biharamulo si hakuna mbunge toka Mh. Kabuye alifariki, na besides si alikuwa mbunge wa TLP, sasa incumbency ya CCM huko inatokea wapi mkuu?
- After all this, hawa wananchi wakaichagua CCM anyways, something is not right hapo au?Tuliona jinsi Mama Kilango alivyokuwa akipata taabu jukwaani huko Busanda alipokuwa anajaribu kukiosoa chama chake kuhusu ufisadi -- hadi masikini wakamzomea -- kwani wananchi waliona vita dhidi ya ufisadi haiwezi ikawa agernda ya CCM -- agenda ya chama hichio ni kinyume chake.
Respect.
FMEs!
1.- Heshima mbele mkuu, hivi huko Biharamulo si hakuna mbunge toka Mh. Kabuye alifariki, na besides si alikuwa mbunge wa TLP, sasa incumbency ya CCM huko inatokea wapi mkuu?
***********
2.- After all this, hawa wananchi wakaichagua CCM anyways, something is not right hapo au?
_____________________________________
FM ES:
1. Incumbency hapa nilimaananisha serikali iliyopo ni ya CCM - incumbent party. samahani kama sikueleweka.
2. Mkulu, sikusema kama issue ya ufisadi ndiyo ili-play katika kutoa final results. Nilikuwa na-imply tu namna issue hiyo ilivyohamasisha wananchi hadi kuwazomea wapiga debe wa mgombea wa CCM.
*************
Muhimu ni hilo swala la upinzani kusimamisha mgombea mmoja.
Hilo haliwezi kusaidia katika chaguzi ndogo labda Tarime na Karatu kwani ccm inahamishia raslimali zote za taifa kwenye jimbo moja. Mfano mzuri ni Busanda. 2010 inawezekana kwa sababu, Magufuli, Masha, Chiligatiwa, Malechela(japo ni mbunge wa maisha wa jimbo la Mtera na wengineo watakuwa majimboni mwao wakihangaika.
Muhimu ni hilo swala la upinzani kusimamisha mgombea mmoja.
Muhimu ni hilo swala la upinzani kusimamisha mgombea mmoja.
Matokeo yatakuwa yale yale kama tutakayoyashuhudia Busanda hivi karibuni, watagawana kura nyingi hivyo kumpa mwanya mgombea wa CCM kushinda kwa kura chache na mwisho wa yote, "The winner takes it all".
Kwa wapinzani kutoungana na kumsimamisha mgombea mmoja, ni CCM Busanda, CCM Biharamulo na 2010 ni CCM kwa kwenda Mbele.
Kwa mtazamo wangu, naamini wengi ambao hawakupiga kura ni wafuasi wa CUF na UDP ambao walisoma dalili za nyakati kuhusu uwezekano wa vyama vyao kushinda, walipoona hawawezi kushinda, wengine wakasusa na wengine wakaichagua CCM katika ule mtindo wa adui wa adui wako ni rafiki yako. CCM na Chadema ndio maadui, kwa CUF waliokubali kushindwa kuna waliiona kuwa badala ya kuwaacha Chadema washinde, bora waipigie kura CCM.Asante Pasco kwa kuwa mstari wa mbele kutuhabarisha kuhusu hizi chaguzi ndogo. Natumaini mchango wako utakuwa mkubwa kama Busanda.
Kwenye nukuu hapo juu sikubaliani na hitimisho na utabiri unaofikia kutokana na hitimosho hilo. Nakubali umoja ni nguvu, ila inategemea kama vinavyoungana vinafanana au vinalingana walau kidogo. Mfano Busanda, hata ukichukua kura 900 na kitu za CUF ukachanganya na za UDP bado CCM wanashinda. Pili hakukuwa na kugawana kura nyingi. CHADEMA elfu ishirini na zaidi, CUF na UDP hata elfu moja hawakufikia, sasa huko kugawana kura nyingi kuko wapi?
Kuna mifano mingi kuonyesha swala sio kuungana tu. Mfano mwaka 2005 Jimbo la Ulanga magharibi alisimama Prof. Mlambiti (TLP) peke yake na Prof. Ngasongwa (CCM). lakini CCM walishinda sio kwamba Prof. Mlambiti alikuwa hakubaliki ila kona za CCM ni nyingi.
Swala sasa ni vyama vya upinzani kupitia upya sera zao, kujijenga katika ngazi za chini na kupigana zaidi. Siamini katika kuunganisha nguvu bila walua kuwa na uwezo, mwelekeo na nia zinazoshabiihana.
Tatizo sio vyama kuungana, tatizo ni bado mwamko wa mageuzi haujawagusa wengi. Hili linakuja. Njaa zetu zinavyozidi tutaanza kujiuliza kama kweli huyu baba ni wetu au wa wengine.
je ni nani ni Mtz halisi?? si wengi asili yetu ni Wabantu toka kule Kongo?