Kuna watu walinotisi mara moja mabadiliko ya kutoka kutumia jina la "Mukasa" kwenda kwa "Rwegasira"... well
Na Frederick Katulanda, Mwanza (Mwananchi)
WAKATI kampezi za uchaguzi mdogo wa kiti cha ubunge katika Jimbo la Biharamulo Magharibi zikiwa zimeanza, mgombea wa CCM katika kinyanganyiro hicho, Oscar Rwegasira, amewekewa pingamizi kwa madai kuwa si raia wa Tanzania .
Habari kutoka Biharamulo na ambazo zimethibitishwa na Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Zuberi Mbyana, zilisema pingamizi hilo limewekwa na mgombea wa Chadema Dk. Anthony Mbassa.
Mgombea huyo wa CCM, aliteuliwa baada ya kuwashinda wapinzani wake katika kura za maoni kwa kupata kura 309.
Walioshindwa katika hatua hiyo ni na kura zao katika mabano ni, Agricola Magotto (120), Mwajemi Mustapha (23), Hassan Rwabudongo (15), Mussa Matata (10) na Nitibihora Burchard (5).
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Mbyana alikiri kupokea pingamizi hilo na kwamba tayari ofisi yake imekwishamwandikia mgombea wa CCM, kumtaka kujibu pingamizi hilo.
Alisema katika pingamizi hilo, mgombea wa Chadema anadai kuwa mgombea wa CCM, hana sifa za kuwania nafasi hiyo kwa sababu si raia wa Tanzania.
Alisema kwa mujibu wa mweka pingamizi, mgombea wa CCM ni raia wa Uganda na kwamba wazazi wake wote wa wawili walitoka Uganda.
Msimamizi huyo alisema mgombea huyo wa Chadema anadai kuwa wazazi wa mgombea mwenzake, hawajawahi kuomba uraia hapa nchini.
Barua tuliyomwandikia mgombea wa CCM ni yenye kumbukumbu namba BBC/30/3/Vol. X/114 ya Juni 10, 2009 ambayo nimemtaka ajibu tuhuma za pingamizi alilowekewa na Chadema alisema msimamizi huyo.
Mkuu wa operesheni ya uchaguzi wa Chadema, John Mrema, alisema katika pingamizi hilo, Chadema wamebaini kuwa mgombea wa CCM, ameshindwa kueleza mahali alikozaliwa.
Baada ya kubaini hilo na kufuatilia uhamiaji na kwingineko, wamebaini kwamba wazazi wake mgombea huyo walingia nchini mwaka 1971 wakitokea Bunyoro nchini Uganda na kuishi eneo la Misenyi, alidai Mrema.
Alidai kuwa mgombea huyo wa CCM, alizaliwa Uganda mwaka 1970 na si katika kijiji cha Rukalagata Biharamulo kama anavyodai.