Nchi inahitaji nabii kuikomboa hii !! Baba JPM nakuomba geukia unahubiri kila siku watu wafanye kazi lakini nchi imebadilika kuwa ya wacheza kamari
1. Wanafunzi wanatafuna ada kwa betting
2. Vijana vikaratasi vya betting vilivyo tikiwa na baadaye kuchanwa vimezagaa kwenye mageto yao
3. Watumishi wa umma unawalipa fedha nyingi Baba lakini siku moja tuu zinachezwa kamari na kuisha
4. Mpaka wazee, wanawake na watoto wote wamejiingiza humo ijapokuwa wanadanganya ni over+18 lakini vitoto vya shule ya msingi vinagonga mikeka kama dawa
4. Kuna football betting
6. Kuna TATU KICHAA
7. Kuna BEKO
8. Kuna mashine za kichina zimejaa kila kona
9. Kuna FOREX
Haya yote ni majini KAMARI ambayo yanatafuna hela za wananchi wako, ijapokuwa unapata kodi kutoka kwao lakini kiasi kikubwa wananchi wako wanazikabidhi kwa hiari yao wenyewe kwenye makampuni haya ambayo mengi ni ya ncje ya nchi na fedha watazipeleka kwao uchumi wetu utakuwaje? Huu ni ugonjwa mkubwa sana umeingia.