Wanachezea chumbani, wizi kabisa! Mi Mara ya mwisho kucheza kamari ya karata tatu ilikuwa 1995, nilipewa Tsh.500 kununua mazaga sokoni. Nikakuta kamari ya bahasha ipi yenye barua, nikaona simpo ila hela sina. Eti wakanipa mtaji wa buku, nikacheza nikapatia. He! Eti weka buku upate buku mbili, nkawaambia nina Jero! Wakaniambia weka hiyohiyo! Kuweka tu, nikaliwa! Nilipatwa na kizunguzungu kikali. Nikawa nazungumka mjini bila kuskia sauti za magari wala za watu. Hapo natafuta cha kudanganya home! Ila baadae nikaamua kwenda kusema kuwa hela imedondoka. Na uwongo wangu uliniokoa. Na hadi leo sijawasimulia. Ila nikaapa kamari hizi za kishenzi ni marufuku.