Bila Barakoa, Muhimbili huingii kuanzia leo. Msindikizaji mmoja tu

curie

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2020
Posts
699
Reaction score
1,600
Twende na sayansi

IMG_20210622_180309.jpg
 
Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imesema kuanzia kesho Jumatano Juni 23, 2021 itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuingia eneo la hospitali hiyo au kutoa huduma bila kuvaa barakoa na mgonjwa atatakiwa kuwa na msindikizaji mmoja tu.

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne Juni 22, 2021 na mkuu wa kitengo cha mawasiliano kwa umma wa MNH, Amaniel Aligaesha inaeleza kuwa hatua hizo zinatokana na maagizo ya waziri wa afya kwa taasisi mbalimbali akizitaka kuchukua tahadhari ili kujikinga na kuwakinga wananchi dhidi ya wimbi la tatu la ugonjwa wa Uviko-19 (Covid-19).

“Tunawaomba wananchi kuunga mkono hatua hizi ili kuongeza tahadhari ya kujikinga dhidi ya ugonjwa huu wa Covid-19. Utekelezaji wa maelekezo haya unaanza rasmi tarehe 23 Juni, 2021 (kesho).”

“Tunawaelekeza wafanyakazi, wanafunzi, ndugu na jamaa wa wagonjwa wote wanaoingia eneo la hospitali kunawa mikono kwa kutumia sabuni na maji tiririka yaliyopo katika maeneo mbalimbali ya hospitali au vipukusi (sanitizer),” amesema.

Mbali na hayo MNH imeelekeza kwa wagonjwa waliolazwa wodini wataruhusiwa kuonwa na ndugu zao watano tu, asubuhi wataruhusiwa ndugu wawili, mchana ndugu mmoja na jioni ndugu wawili.
 
Hatua njema mdogo mdogo tutaelewana tu.

Kuna kada zilioshwa bongo na bwana mmoja alikwenda:

“Tunawaomba wananchi kuunga mkono hatua hizi ili kuongeza tahadhari ya kujikinga dhidi ya ugonjwa huu wa Covid-19. Utekelezaji wa maelekezo haya unaanza rasmi tarehe 23 Juni, 2021 (kesho).”

Kuweza kusikia hadi damu iwatoke masikioni.

Cc: mjingamimi
 
Hakuna corona nyie semeni ni ntu za dill mnataka kupiga ela za IMF

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app

Wanaodai kuwa ugonjwa huu haupo si kwetu tu bali hata kwao wapo:

Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imesema kuanzia kesho Jumatano Juni 23, 2021 itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuingia eneo la hospitali hiyo au kutoa huduma bila kuvaa barakoa na mgonjwa atatakiwa kuwa na msindikizaji mmoja tu.

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne Juni 22, 2021 na mkuu wa kitengo cha mawasiliano kwa umma wa MNH, Amaniel Aligaesha inaeleza kuwa hatua hizo zinatokana na maagizo ya waziri wa afya kwa taasisi mbalimbali akizitaka kuchukua tahadhari ili kujikinga na kuwakinga wananchi dhidi ya wimbi la tatu la ugonjwa wa Uviko-19 (Covid-19).

“Tunawaomba wananchi kuunga mkono hatua hizi ili kuongeza tahadhari ya kujikinga dhidi ya ugonjwa huu wa Covid-19. Utekelezaji wa maelekezo haya unaanza rasmi tarehe 23 Juni, 2021 (kesho).”

“Tunawaelekeza wafanyakazi, wanafunzi, ndugu na jamaa wa wagonjwa wote wanaoingia eneo la hospitali kunawa mikono kwa kutumia sabuni na maji tiririka yaliyopo katika maeneo mbalimbali ya hospitali au vipukusi (sanitizer),” amesema.

Mbali na hayo MNH imeelekeza kwa wagonjwa waliolazwa wodini wataruhusiwa kuonwa na ndugu zao watano tu, asubuhi wataruhusiwa ndugu wawili, mchana ndugu mmoja na jioni ndugu wawili.
Wimbi latatu tena Covid-19! lakini tusitishike sisi makabwela, uzuri wa CORONA hapa kwetu tz inafyeka kigogo tu na kuwachapa wanyonge.
 
Inafahamika kuwa huyu mwana kharam alenga zaidi wanaume, wenye umri mkubwa na pia wenye magonjwa mengine.

Isije kuwa hao vigogo ni watu tu wanaotokea kuwa pia kwenye makundi pendwa haya? Isije pia kuwa wasio na majina yatokea tu kuwa wao si habari kuweza kusikika?

Cha kukumbuka pia wimbi la tatu linasongeshwa na kirusi kipya delta. Hiki kutoka India yasemekana kina tabia mpya ya kuwapenda wote. Si wanawake si wanaume. Si vijana si wazee. Si vijana si watoto. Wote ni abiria wake.

Bado haipo sababu ya kujali?
 
Kwa hakika serikali ya awamu ya sita imedhamiria kwa vitendo kutuvusha salama. Wimbi la tatu si la kufanyia mzaha hata kidogo.

Kongole kwenu serikali ya mama Samia.

Bila Barakoa kuanzia leo haingii mtu Muhimbili. Hili ni la kheri sana kwani kinga ni bora zaidi kuliko tiba.

Hii ni habari njema kabisa. Wigo na uongezwe sasa, kufika kote kuliko na mazingira hatarishi yaani kuliko na mikusanyiko mikubwa ya watu.

Kwenye usafiri wa umma, masokoni nk kusiachwe bila usimamizi.

Inapobidi kutumia kiwango fulani cha nguvu kama hivi kwa wasiotaka kuelewa kwa hakika ni sawa kabisa.

Pole pole, kwa pamoja mbona tutavuka tu?
 
Back
Top Bottom