Kwa hakika serikali ya awamu ya sita imedhamiria kwa vitendo kutuvusha salama. Wimbi la tatu si la kufanyia mzaha hata kidogo.
Kongole kwenu serikali ya mama Samia.
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imesema kuanzia kesho Jumatano Juni 23, 2021 itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuingia eneo la hospitali hiyo au kutoa huduma bila kuvaa barakoa na mgonjwa...
www.mwananchi.co.tz
Bila Barakoa kuanzia leo haingii mtu Muhimbili. Hili ni la kheri sana kwani kinga ni bora zaidi kuliko tiba.
Hii ni habari njema kabisa. Wigo na uongezwe sasa, kufika kote kuliko na mazingira hatarishi yaani kuliko na mikusanyiko mikubwa ya watu.
Kwenye usafiri wa umma, masokoni nk kusiachwe bila usimamizi.
Inapobidi kutumia kiwango fulani cha nguvu kama hivi kwa wasiotaka kuelewa kwa hakika ni sawa kabisa.
Pole pole, kwa pamoja mbona tutavuka tu?