Bila capital inflow na FDI hatuwezi kutoboa, hata S.Korea, Malaysia n.k wasingetoboa

Bila capital inflow na FDI hatuwezi kutoboa, hata S.Korea, Malaysia n.k wasingetoboa

Tozo

Senior Member
Joined
Aug 23, 2021
Posts
101
Reaction score
202
Watanzania tulidanganywa sana, nimemaliza Master Degree in Development Economics (MDE), nimesoma cases nyingi za nchi zilizokuwa maskini kama sisi wakati tunapata uhuru lakini sasa zimeshaingia nchi zilizoimarika kiuchumi.

Ukiachilia mbali S.Korea, Malaysia n.k. Hata nchi za Afrika zilizoimarika kiuchumi kama Nigeria, SA, Botswana, Kenya n.k ukiangalia kiasi cha capital inflow, na Foreign Direct Investment (FDI) ni kikubwa mno ukilinganisha na nchi yetu.

Maprofesa wa Uchumi kama akina Lipumba, Ngowi (MZUMBE), Temu White (SUA), Mlambiti ( SUA), Masanyiwa (IRDP) wanajua, hata Kabudi profesa wa sheria anajua, Dr. Mpango anajua, Dr. Mmasa wa UDOM anajua, Prof. mstaafu Mbwiliza wa historia ya siasa (UDSM) anajua, Dr. Kimei (CRDP) anajua.

Unafiki wa wasomi wetu kuogopa kushauri tofauti na mawazo aliyonayo kiongozi mkuu ndiyo yametufanya kuendelea kuwa maskini. Masharti ya mikopo siyo kuibiwa madini yetu, riba kubwa wala kukusanya kodi wenyewe kwenye miradi kama tunavyodanganywa bandari ya Bagamoyo.

Ni UONGO wa wanasiasa wetu. Dhana ya kujitegemea na kuwa donar country ilikuwa kuogopa kubanwa na masharti ya mikopo inayotaka utawala wa sheria, demokrasia na uhuru wa kufanya siasa. Mama unaupiga mwingi achana na akina Mbowe na Tundu Lissu watoe mawazo mbadala.

Nakuona kuweka rekodi zako za kukumbukwa na kuthibitisha wanawake wanaweza. Tekeleza masharti ya IMF, WB na nchi wahisani tutoke kwenye umaskini. Boresha elimu yetu, nidhamu ya matumizi serikalini, ruhusu wapinzani waibue wala rushwa na wezi serikalini.

Bunge liwe imara ili kuishauri serikali achana na kuchagua vyama na tuchague mtu mwenye uelewe na weledi wa kuishauri serikali. Uko sahihi kuimarisha mahusiano ya kimataifa. Leo Rais Kenyatta yuko white house US, hata wewe ukiitwa nenda.
 
Back
Top Bottom