Mikopo Consultant
JF-Expert Member
- Oct 28, 2024
- 2,375
- 4,784
Ubunge wa kupewa, kama ambavyo iliotwa na NCCR Mageuzi mwaka 2020, ni kitu kisichotekelezeka; japokuwa ahadi yake huwa ni tamu sana masikioni mwa vyama vya upinzani visivyotaka kuchutama ili kuokota vya chini.
Sababu kubwa ya ni kwanini hichi kitu ni kigumu kutekelezeka ni kwamba, ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa miaka ya karibuni, imekuwa ni changamoto sana mwakilishi kuipata nafasi ya kugombea. Wanatumia rasilimali nyingi sana, kuna watu mpaka sasa wameweka mezani zaidi ya 500 Milioni kwa ajili ya kuupata ubunge. Na wengine yaweza kuwa hata Bilioni 1 kabisa. Ubunge ni dili.
Kwa mazingira kama hayo, na kwasababu Chadema itakuwa haipo kwenye boksi la kura, na wengi wetu hatutapiga kabisa; maana yake ni kwamba kura zitapigwa na wanaCCM ambao ni lazima watawapa CCM wenzao.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Sasa ule usiku wa kuamkia tarehe 26, hawa wagombea wote waliowekeza mamia ya mamilioni watakuwa wapo bize sana kujihakikishia ushindi, na sidhani kama kuna yeyote atataka kusikia na kukubali jimbo lake lipewe mtu wa Chaumma au ACT ambao kwanza kura zao zitakuwa ni chache. Halafu wagombea wa hivi vyama (ACT na Chaumma) ni kama wanacheza bahati nasibu ya siasa (uwekezaji sufuri halafu wanategemea kuamka matajiri) ki uchumi, hai make sense.
Na kwasababu majimbo ni mengi, kila mgombea wa CCM atakuwa na mawazo kwamba "Aaah!! hao wapinzani walioahidiwa ubunge wa bwerere, wataupewa huko kwenye majimbo mengine na sio hili jimbo langu nililowekeza mamia ya mamilioni".
Matokeo yake ni kwamba, nchi itaamka tarehe 26 ikiwa na wabunge wote wa CCM (100%) na wale waliotegemea kuteleza kwenye ganda la ndizi wakiambulia 0%.