GE2025 Bila CHADEMA, CCM wanaenda kupiga 100% - 0%, sioni nafasi ya ubunge wa kupewa wanaouota ACT na CHAUMMA

GE2025 Bila CHADEMA, CCM wanaenda kupiga 100% - 0%, sioni nafasi ya ubunge wa kupewa wanaouota ACT na CHAUMMA

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
If they will parade right candidates for right place and people, why not?
Sheikh Ponda ndo naona ni right candidate, ila kwa jimbo analogombea, atachezea za uso tu.

Huko kwenye majimbo mengine wamejaa wajasiriasiasa, hawapo genuine kabisa, na ni fair kutabiri wao kupigwa kama ngoma.

Kama ulimsikiliza Peter Madeleka, utaona ni kiasi gani hawa wajasiriasiasa walivyo na akili mbovu.

Bila Chadema, ni mustakabali wa taifa CCM kupiga 100% kwa 0% na sio kukaribisha wapinzani wa kupandikiza, itakuwa dissaster
 
Sahiv Mwinyi abakubalika Zanzibar na ndo turufu ya kwanini upinzani utatepeta. Zamani ilikuwa CUF/ACT wanachukua Pemba yote na kuna majimbo Unguja na CCM wakichukua Unguja, ila huu mwaka naamini itatokea tofauti kidogo, CCM imepata nguvu sana Zanzibar, na urais wa Samia umechangia pakubwa

we jamaa bana, CCM hawawezi shinda zaidi ya majimbo 15 Zanzibar nzima kihalali, kinyume na hapo waibe tu. na hata hiyo kuiba kura bado wanapigwa, njia nyepesi ni kuja na matokeo yao mfukoni na kutangaza bila ya kuzingaia uhesabuji wa kura kama walivyofanya 2020.
nimewahi kufanya kazi katika kuripoti uchaguzi Zanzibar chaguzi za nyuma.
 
..ACT wana uwezo wa kushinda majimbo yote ya Pemba, baada ya hapo mbide huwa ni kushinda jimbo 1 au 2 upande wa Unguja.

..Kikwazo kilichoko mbele yao ni utaratibu wa kura ya siku 2. Zanzibar uchaguzi unafanyika siku mbili. Siku ya kwanza wanapiga kura Polisi, Tume, etc. Siku ya pili wanapiga wananchi wote. Sasa kura zinaibiwa siku ya kwanza.

ACT wana uwezo wa kushinda mpaka majimbo 15 Unguja bila ya tabu yoyote, ishu ipo kwa CCM kuachia hayo majimbo. Mana siku hizi wana style ya kuja matokeo mfukoni bila ya hata kuzingatia uhisabuji wa kura.
Kwa Pemba CCM hata Udiwani mmoja hawawezi kupata bila ya kuja na matokeo mfukoni.
 
..uchaguzi wa Znz ni mrahisi sana kujua matokeo yake ukizingatia udogo wa nchi hiyo.

..vyama vya Ccm na Act vinafahamu ngome zake zilipo hivyo kuweza kutabiri matokeo kwa urahisi.

..Nadhani tukienda kwenye matokeo ya 2015 yaliyopinduliwa na Mzee Jecha tunaweza kufahamu nini kitatokea mwaka huu.
 
Matokeo yaliyopinduliwa na Jecha yaikuwa ni baada ya CCM kuweza kuiba majimbo karibu 10 Unguja, ndipo ngoma ilipoishia pale wakaona kilichabaki watie mpira kwapani tu mana hawana njia nyengine tena.

ALichofanikiwa maalim Seif kipindi kile aliwapa darasa ya kutosha wasimamizi wake kuwa wawaache CCM waibe vya kutosha ila wao wahakikishe tu wanarudi na fomu za matokeo makao makuu. ALikuwa na uhakika CCM hata waibe vipi bado angewanshinda tu. Na ndilo lililotokea.
 
..asante sana kwa elimu hii.

..kwa kweli unanifungulia uhalisia wa chaguzi za Zanzibar.

..wakati mwingine namlaumu Maalim kwa kuwa muungwana kupita kiasi kwa Ccm.
 
..asante sana kwa elimu hii.

..kwa kweli unanifungulia uhalisia wa chaguzi za Zanzibar.

..wakati mwingine namlaumu Maalim kwa kuwa muungwana kupita kiasi kwa Ccm.

Tutamlaumu bure, Watu wa nchi hii hawajawa tayari kupambana na CCM, sisi ni waoga sana, wanasiasa waliojitoa kisawasawa na wanaoendelea kujitoa wanapoteza mda wao tu.
 
ACT Kwa upande wa znz wanayo majimbo tena watagawana nusu kwa nusu na CCM
Labda mgombea wa urais wa Jamuhuri awe mtu wa bara LAKINI kama ni mama, I don't think so. Wazanzibari ni wazalendo sana kwa nchi yao kuliko watu wa bara. Wabara ni wajinga kuliko hata wale nyumbu wa Serengeti
 
Tutamlaumu bure, Watu wa nchi hii hawajawa tayari kupambana na CCM, sisi ni waoga sana, wanasiasa waliojitoa kisawasawa na wanaoendelea kujitoa wanapoteza mda wao tu.

..Wazanzibari walikuwa tayari kupambana ili kutetea ushindi wa CUF, tatizo lilikuwa Maalim Seif kutokuwa tayari.

..Salmin Amour, Amani Karume, Ali Shein, walikuwa tayari kutetea wizi wa kura, wakati Maalim Seif akiwa muoga kulinda ushindi wake.
 
Ubunge wa kupewa, kama ambavyo iliotwa na NCCR Mageuzi mwaka 2020, ni kitu kisichotekelezeka; japokuwa ahadi yake huwa ni tamu sana masikioni mwa vyama vya upinzani visivyotaka kuchutama ili kuokota vya chini.

Sababu kubwa ya ni kwanini hichi kitu ni kigumu kutekelezeka ni kwamba, ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa miaka ya karibuni, imekuwa ni changamoto sana mwakilishi kuipata nafasi ya kugombea. Wanatumia rasilimali nyingi sana, kuna watu mpaka sasa wameweka mezani zaidi ya 500 Milioni kwa ajili ya kuupata ubunge. Na wengine yaweza kuwa hata Bilioni 1 kabisa. Ubunge ni dili.

Kwa mazingira kama hayo, na kwasababu Chadema itakuwa haipo kwenye boksi la kura, na wengi wetu hatutapiga kabisa; maana yake ni kwamba kura zitapigwa na wanaCCM ambao ni lazima watawapa CCM wenzao.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Sasa ule usiku wa kuamkia tarehe 26, hawa wagombea wote waliowekeza mamia ya mamilioni watakuwa wapo bize sana kujihakikishia ushindi, na sidhani kama kuna yeyote atataka kusikia na kukubali jimbo lake lipewe mtu wa Chaumma au ACT ambao kwanza kura zao zitakuwa ni chache. Halafu wagombea wa hivi vyama (ACT na Chaumma) ni kama wanacheza bahati nasibu ya siasa (uwekezaji sufuri halafu wanategemea kuamka matajiri) ki uchumi, hai make sense.

Na kwasababu majimbo ni mengi, kila mgombea wa CCM atakuwa na mawazo kwamba "Aaah!! hao wapinzani walioahidiwa ubunge wa bwerere, wataupewa huko kwenye majimbo mengine na sio hili jimbo langu nililowekeza mamia ya mamilioni".

Matokeo yake ni kwamba, nchi itaamka tarehe 26 ikiwa na wabunge wote wa CCM (100%) na wale waliotegemea kuteleza kwenye ganda la ndizi wakiambulia 0%.
NO REFORMS NO ELECTION, Watanzania wanajua vyama vingine nje ya CHADEMA ni Mali ya CCM hivyo uchaguzi bila CHADEMA tafsiri yake ni kwamba CCM inasimama peke yake kwenye uchaguzi na kujipigia kura.NO REFORMS NO ELECTION Hesabu zetu tunazifungia hapo.
 
Back
Top Bottom