Bila dini sisi Waafrika tusingeishi?

Dini zipo kisiasa tu.
Ni njia ya wajanja wachache kushika akili za wajinga wengi, zombification.

Hata hiyo miungu inayohubiriwa na hizo dini ni ujinga mtupu.
 
Umeongea ukweli mtupu kabisa, na sio kwamba babu na bibi zetu waliwapokea wazungu kiroho safi, kuna maeneo vilipigwa vita sio mchezo. Vita vya majimaji ni mfano mmojawapo. Na inasemekana babu na bibi zetu wengine walibatizwa kwa upanga na risasi.

Kinachojibu maombi yetu sio jina la Yesu wala la Muhammad, kinachojibu maombi yetu ni kule kuamini kwamba tukiomba hivi tutapokea. Ko hata tukiomba kwa jina la MUNGU mmoja kama Waafrika maombi yetu yatajibiwa tu, kwani babu na bibi zetu hawakuwa wakiomba kabla ya ujio wa wazungu? Jibu ni hapana, waliomba kwenye misitu mikubwa kama ilivyo kwa Wazanaki na majibu ya matatizo yao waliyapata.
 
Dini zipo kisiasa tu.
Ni njia ya wajanja wachache kushika akili za wajinga wengi, zombification.

Hata hiyo miungu inayohubiriwa na hizo dini ni ujinga mtupu?
🤣🤣🤣hii ni FACT kabisa, umeongea hoja makini sana!
 
Hawa watu walituvuruga kweli kweli kwa kauli mbiu zao potofu.

Watasemaje walituletea Mungu wa kweli, wakati huyu Mungu tulikuwa naye hata kabla ya kuja kwao? Inatia sana hasira.

Kabla ya wao kuja kwetu, shetani hakuwa na nafasi kubwa katika jamii zetu. Alikuwa hakatishi mtaa. Upendo na maadili meema vilikuwa tele katika jamii.

Tulivurugwa kweli kweli!
 
DINI
Moja ya vitu vilivyoipumbaza Afrika dini ni mojawapo,dini imeleta ubaguzi,leo hii Mtanzania kuoa ama kuolewa na Mtanzania mwenzake anawekewa kigezo cha dini.
Mtanzania mkristo anajiona ni bora kuliko Mtanzania muislamu ama Mtanzania muislamu anajiona ni bora kuliko Mtanzania mkristo cha ajabu unaweza kuta wote ni kabila moja.
Unakuta dini inafundisha kuwa ombaomba kuliko kufanya kazi mwishowe unaambiwa asiefanya kazi asile huu ni zaidi ya upumbavu.
Leo hii ukitaka kujadili kiundani mambo ya dini utaitwa kafiri au mpagani mimi nawaambiaga niiteni tu kafiri lakini sio mniite kondoo.
Kuna watu walimwaga damu zao kwa ajili ya Tanzania hii akina Mtemi Isike,Mtwa Mkwawa,Mtemi Milambo,Kinjeketile Ngwale n.k lakini hata hawatajwi wanatajwa wengine,ngoja nikupe siri moja mtu pekee aliemwaga damu kwa ajili yako ni mama ako mzazi na hakuna mwingine zaidi yake.
Aliekuzaa kazaliwa lakini aliekuumba hakuumbwa hivi mizani ipo sawa hapo au ni riba tu.
TUAMKE.
 
Utasikia kijana naoa unatafuta kupotea,

Ila ukweli haujifishi ipo siku itakuwa kweli.....

Mbaya zaidi kila mtu anaona dini yake ndio bora.
 
Huyo mama anaeuza Shamba akatoe sadaka ni ujinga wake wa kutoyajua maandiko, sema kakutana na wajasiliadini wamempiga.
Hakuna Ukristo nje ya maandiko.
Eti sadaka ya kujimaliza sijui sadaka ya kujiteketeza huu ni wizi kabisa na uongo mkubwa.
Maandiko yanakataa hili utoi sadaka Ili uumie, ukiumia utanung'unika ambapo ni kumkosea MUNGU.
Tutoe kwa moyo na sio kwa shuruti. MUNGU sio masikini.
Toa kwa nia maalumu, toa pasipo kuumia, toa kile unachoweza.
Pana mtume na Nabii wa uongo mmoja alimdalalia mama mjane nyumba ikauzwa KWA milioni 150,pale pale akakata milioni 15 eti fungu la kumi then akamkopa huyo mjane milioni 3 eti akamilishe mambo ya kanisa. Alipopata hizo pesa kesho kaingia showroom kavuta toyota crown ya milioni 17.
Huu ni wizi mkubwa kabisa. Wanawachezea Sana wajinga.
 
Dini haina tatizo, Ingekuwa ni tatizo tungeyaona ilipoanzia,mbona wao wapo fresh tu.
Pili nani kakuambia Mwafrika anafata dini,angefata dini asingekuwa masikini.
Wengi ni wanafiki wanaingia nyumba za Ibada kama desturi na pia kuwaridhisha watu.
Kuoana na mtu wa dini tofauti ni hatari kimahusiano subiria upendo uishe ndo utaelewa madhara yake.
Njia sahihi ni mmoja abadili dini amfate mwenzake.
Hakuna miongozo miwili ya kiimani ndani ya nyumba moja ni heri muwe wapagani.
 
Dini ni mpango wa Mwanadamu kumtafuta MUNGU na sio mpango wa Mungu kumtafuta mwanadamu, dini zimetengenezwa na wanadamu ambao wao ndio uamua kipi waongeze kipi wapunguze.
We mtafute Mungu na sio kufuata dini utapotea
 
Wewe ni dhehebu gani mkuu?
 
Mimi nina MUNGU ambaye ndio hunipa punzi na baraka za hapa duniani...

Wewe kama huna MUNGU ni sawa pia.
Dini ya ukristo na uislam zimesaidia kuwafanya waafrika kuwa wastaarabu.Manake Babu na bibi zetu walikuwa hawana maarifa makubwa na pia hawakuwa na standard yoyote,, walikuwa hawajui nguo ni nini,sabuni ni nini,,usafi ni nini,,kuzika ni nini,,kuwa na jamii Moja ili pamoja ni nini,, kusoma,,elimu,,teknolijia hawakujua.Tulikuwa kama wabarbaig au wahadzabe.Na ushirikina ulikuwa mwingi kwa sababu ya kuabudu miti na milima.
 
Misri ipo wapi mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…