Bila kocha kumpunzisha Mwamnyeto Yanga ingepoteza kwa coastal Union

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Mechi ya final ya Azam FA Bakari Mwamnyeto alikuwa uchochoro wa wazi kwa Wana Tanga coastal Union. Kulikuwa na mpango Mwamnyeto acheze chini ya kiwango kwa kupewa kadi ya njano mapema.
 
Mechi ya final ya Azam FA Bakari Mwamnyeto alikuwa uchochoro wa wazi kwa Wana Tanga coastal Union. Kulikuwa na mpango Mwamnyeto acheze chini ya kiwango kwa kupewa kadi ya njano mapema.
Ule mfumo wa mwalimu wa 3 5 2 nao ulichangia kwenye kutengeneza uchochoro upande wa pembeni wa Juma Shaban/Kibwana Shomari, na pia Farid Musa.

Ukijumlisha sasa na hayo madhaifu ya Bakary Mwamnyeto na Dickson Job! ya kujisahau, kuzubaa na kutokuziba mianya inayoachwa na mabeki wa pembeni waliokuwa wanapanda muda wote mbele kwenda kuongeza mashambulizi.

Hivyo kwa mimi, naona mfumo wa mwalimu haukufanya kazi kwenye mechi ya jana.
 
Ile game ilikuwa mwiba kwetu kilichotuokoa ni quality ya players na akili ya Nabi
 
Hata utopolo wenzako wanajua pale Hamna beki halafu unaleta utopolo kadi ya njano ya nini
Beki Yuko pale, SEMA TU mechi Ile ilikuwa na hadhi kubwa na muhimu sana katika siasa za mkoa wa Tanga
 
Kaka coastal Union ilipigwa na Yanga ndani na nje msimu huu, coastal Haina uwezo wa kufunga beki ya Yanga magoli 3 kwenye mechi moja. Nabi ndiye aliyetibua mipango kwa kimtoa Mwamnyeto.
 
Kuna mechi zingine huzingua ni kawaida kwa soka.
Sio kwa Yanga hii ya unbeaten kufungwa goli 3. Sopu huyu mmempa ujiko bila sababu kabisa. Mtaona ligi ikianza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…